Trump anataka Marekani, China na Urusi zipunguze nusu ya bajeti zao za ulinzi. Pia anapenda Urusi irudishwe kwenye G7

Trump anataka Marekani, China na Urusi zipunguze nusu ya bajeti zao za ulinzi. Pia anapenda Urusi irudishwe kwenye G7

Xi Jinping

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2023
Posts
3,651
Reaction score
11,548
"Moja ya mikutano ya kwanza ninayotaka kufanya ni pamoja na Rais Xi wa China, Rais Putin wa Urusi, na ninataka kusema, tupunguze nusu ya bajeti zetu ya kijeshi na nadhani tutaweza kufanya hivyo."
Trump

Huu ndio utamu wa kwenda naye kibabe Marekani. Marekani ni superpower kwa mataifa dhaifu ila sio kwa China na Urusi.

Sasa hivi Marekani level yake ni kuyafokea mataifa ya Ulaya. Wiki hii mataifa ya Ulaya yamesemwa na kudhalilishwa na mawaziri wa Marekani. Alianza waziri wa ulinzi wa Marekani akaja waziri wa mambo wa nje wa Marekani.

Ukitaka kuona matokeo ya kwenda naye kibabe Marekani, kwenye mkutano wa kuzungumzia muafaka wa vita vya Ukraine ambapo Trump amepanga kukutana na Putin hakuna taifa lolote la Ulaya wala Ukraine yenyewe haijaalikwa. Wababe tu watakaa mezani.

Akielezea maono yake ya kutetereka kwa world order Trump pia alisema:

"Ningependa kurejeshwa kwa Urusi katika G7, ambayo ilisimamishwa mwaka 2014 baada ya Moscow kutwaa rasi ya Crimea ya Ukraine. Nadhani lilikuwa kosa kumtoa nje ya G7 (Putin)"
– Trump
  • Kwa nini Trump anataka China, Urusi na Marekani zipunguze nusu ya bajeti zao za ulinzi? Je, Marekani imeoma haiwezi kucompete na mataifa hayo 2 kwenye military tech na capability?

  • Kupunguzwa kwa bajeti na matumizi ya hivi majuzi nchini Marekani ina maana kuwa haiwezi kumudu bajeti yake ya kijeshi na ulinzi?

  • Kwa nini Marekani imechachamaa kuzitaka nchi za NATO kutumia 5% ya GDP zao kwenye masuala ya ulinzi? Je, Marekani imelemewa na michango inayotoa NATO kama mfadhili mkuu?
Dunia inahitaji sana balance of power sio nani superpower
 
Yeye USA Ni nani mpk anitake nipunguze bajeti ya pesa nilizotafuta kwa jasho langu.
Anasema anataka kumwambia Xi na Putin kuwa mabilioni wanayotumia kwenye bajeti za ulinzi na kuunda mabomu ya nyuklia yanaweza kutumika katika matumizi mengine mazuri

Kweli leo Marekani yenye bajeti kubwa ya kijeshi, ulinzi na muuzaji mkubwa wa silaha duniani imekuwa ya kusema hivi?

By the way ni kama Marekani imeanza kuyumba
 
Hujui Historia,
Jielimishe kuhusu The Strategic Arms Reduction Treaty (START) na INF treaty.
 
Maelekezo anayowapa C,C,M anawapelekea warusi 😀
Natamani kwenye huo mkutano Xi na Putin wamshauri tu afunge military bases zake 750 zilizo katika mataifa mbalimbali

Halafu ajionee jinsi atapunguza bajeti ya ulinzi ya Marekani na kufanya mambo mengine ya maana kwa Wamarekani wanaokabiliwa na inflation, gharama kubwa za afya, homelessness, kuondoa recession kwenye industrial production n.k
 
Bajeti ya ulinzi ya Marekani ni 4% ya GDP na 13% ya bajeti. Ukubwa wa bajeti ya Marekani ndio unaowachanganya. Matatizo ya Homelessness na Inflation hayana uhusiano sana na bajeti, hakuna recession kwenye industrial production ya Marekani.
 
Hujui Historia,
Jielimishe kuhusu The Strategic Arms Reduction Treaty (START) na INF treaty.
China haijawahi kuwa sehemu ya START na INF ilikuwa ni mikataba ya Marekani na Soviet Union then Urusi

Na tangu zianzishwe hazijawahi kufanikiwa kufikia malengo yake

Na kwa alichosema Trump hakihusiani kabisa na START wala INF na ndio maana ameitaja na China ambayo haipo kwenye mikataba hiyo miwili

hakuna recession kwenye industrial production ya Marekani.
Unaelewa maana ya recession?

Unapolinganisha industrial production ya Marekani miaka ya 1970/1980 na sasa

Je, uzalishaji unaenda ukiwa unaongezeka au ni increasing at decreasing rate? Why now U.S aint a leading mfg powerhouse and replaced by China?

Statistics never lie kafanye homework yako ujionee jinsi industrial output imeshuka

Kosa lililofanywa na Marekani ni kuwekeza zaidi kwenye finance capitalism na kupunguza uwekezaji kwenye industrial capitalism
 
Unaelewa maana ya recession?

Unapolinganisha industrial production ya Marekani miaka ya 1970/1980 na sasa

Je, uzalishaji unaenda ukiwa unaongezeka au ni increasing at decreasing rate? Why now U.S aint a leading mfg powerhouse and replaced by China?

Statics never lie kafanye homework yako ujionee jinsi industrial output imeshuka

Kosa lililofanywa na Marekani ni kuwekeza zaidi kwenye finance capitalism na kupunguza uwekezaji kwenye industrial capitalism
Ni hivi,
Recession ni kitu tofauti kabisa,

Gharama za wafanyakazi Marekani ni kubwa sana kuliko China kwa sababu ya standard ya maisha, usalama kazini na haki za wafanyakazi. Hapo ndipo China inapoipita Marekani kwa uzalishaji. Hata hivyo manufacturing sector ya Marekani imekuwa kwa 80% tangu miaka ya 1980s, haijawahi kudumaa.

Kingine serikali ya Marekani haifanyi biashara kama vile serikali ya China inavyomiliki makampuni na kufanya biashara.
 
Bajeti ya ulinzi ya Marekani ni 4% ya GDP na 13% ya bajeti. Ukubwa wa bajeti ya Marekani ndio unaowachanganya. Matatizo ya Homelessness na Inflation hayana uhusiano sana na bajeti
Marekani inatumia billions of dollars za walipa kodi wake kwenye unnecessary wars and conflicts na ku-operate overseas military bases hizo pesa zinafanya defense budget kuwa 4% ya GDP.

Ikipunguza matumizi ya kijeshi inaweza kufanya ya muhimu zaidi. Imagine hata kuboresha miundombinu imekuwa changamoto Marekani

Mfano China inatumia 1.6% tu ya GDP yake kwenye defense budget lakini bado inamchallenge Marekani na wakati huohuo inafanya makubwa kwenye economic devpt na economic growth tofauti na Marekani
 
Ni hivi,
Recession ni kitu tofauti kabisa
An industrial recession is a decline in industrial production that occurs during a broader economic recession

Nikupe mifano 2 miaka ya 1970 na 1980 Marekani ndiye ilikuwa mzalishaji mkuu wa chuma duniani kwa tani na ilikuwa inaongoza kwenye ship building

Lakini kwa sasa Marekani imekuwa kituko kwenye hizo sekta mbili haipo hata katika orodha ya nchi 5 zinazofanya vizuri kwenye hizo sekta

China imeizidi Marekani kwenye uzalishaji wa chuma mara 40

China imeizidi Marekani kwenye uzalishaji wa meli zaidi ya mara 230

Hiyo ni industrial recession

Marekani inatumia billions of dollars za walipa kodi wake kwenye unnecessary war and conflicts na ku-operate overseas military bases hizo pesa zinafanya defense budget kuwa 4% ya GDP. Ikipunguza matumizi ya kijeshi inaweza kufanya ya muhimu zaidi. Imagine hata kuboresha miundombinu imekuwa changamoto Marekani

Mfano China inatumia 1.6% tu ya GDP yake kwenye defense budget lakini bado inamchallenge Marekani na wakati huohuo inafanya makubwa kwenye economic devpt na economic growth tofauti na Marekani
Tatizo unaamini kila propaganda za CCP na MAGA. China wanapika takwimu, makadirio ya wataalamu wengi wanaoifuatilia China ni kwamba bajeti yao halisi ya ulinzi ni mara mbili ya ile ambayo serikali huwa wanaisema. Pia fahamu kwamba ukiwa huna barabara za lami ukijenga utaonekana zaidi kuliko mwenye lami ambaye anahitaji kurekebisha mashimo tu.
 
Gharama za wafanyakazi Marekani ni kubwa sana kuliko China kwa sababu ya standard ya maisha, usalama kazini na haki za wafanyakazi. Hapo ndipo China inapoipita Marekani kwa uzalishaji.
Suala sio gharama za wafanyakazi suala ni supply chain. Marekani haina supply chain ya kuizidi China kwenye industrial production

Kinachofanya China iwe na gharama nafuu ya uzalishaji hasa ni uwepo wa manufacturing ecosytem iliyo complete na bora zaidi ya Marekani. Na ndio maana hata makampuni ya West yanavutiwa kuwekeza China.

Kama suala lingekuwa ni gharama za wafanyakazi mbona mataifa mengine kama ya Latin America, ASEAN, Africa, Middle East yenye cheap labour hayafanyi vizuri kwenye mfg industry kama China
 
An industrial recession is a decline in industria production that occurs during a broader economic recession

Nikupe mifano 2 miaka ya 1970 na 1980 Marekani ndiye ilikuwa mzalishaji mkuu wa chuma duniani kwa tani na ilikuwa inaongoza kwenye ship building

Lakini kwa sasa Marekani imekuwa kituko kwenye hizo sekta mbili haipo hata katika orodha ya nchi 5 zinazofanya vizuri kwenye hizo sekta

China imeizidi Marekani kwenye uzalishaji wa chuma mara 40

China imeizidi Marekani kwenye uzalishaji wa meli zaidi ya mara 230

Hiyo ni industrial recession

Kwa nini kampuni za Marekani kama Nike, Adidas, Apple, Tesla na nyingine nyingi zinafungua viwanda zaidi China na nchi nyingi za Asia kuliko Marekani au Ulaya??
 
Suala sio gharama za wafanyakazi suala ni supply chain. Marekani haina supply chain ya kuizidi China kwenye industrial production

Kinachofanya China iwe na gharama nafuu ya uzalishaji hasa ni uwepo wa manufacturing ecosytem iliyo complet na bora zaidi ya Marekani. Na ndio maana haya makampuni ya West yanavutiwa kuwekeza China.

Kama suala lingekuwa ni gharama za wafanyakazi mbona mataifa mengine kama ya Latin America, ASEAN, Africa, Middle East yenye cheap labour hayafanyi vizuri kwenye mfg industry kama China
Nenda kwanza kajifunze kuhusu sweatshops, hujui mengi.
 
Back
Top Bottom