Trump anataka Marekani, China na Urusi zipunguze nusu ya bajeti zao za ulinzi. Pia anapenda Urusi irudishwe kwenye G7

Trump anataka Marekani, China na Urusi zipunguze nusu ya bajeti zao za ulinzi. Pia anapenda Urusi irudishwe kwenye G7

"Moja ya mikutano ya kwanza ninayotaka kufanya ni pamoja na Rais Xi wa China, Rais Putin wa Urusi, na ninataka kusema, tupunguze nusu ya bajeti zetu ya kijeshi na nadhani tutaweza kufanya hivyo."
Trump

Huu ndio utamu wa kwenda naye kibabe Marekani. Marekani ni superpower kwa mataifa dhaifu ila sio kwa China na Urusi.

Sasa hivi Marekani level yake ni kuyafokea mataifa ya Ulaya. Wiki hii mataifa ya Ulaya yamesemwa na kudhalilishwa na mawaziri wa Marekani. Alianza waziri wa ulinzi wa Marekani akaja waziri wa mambo wa nje wa Marekani.

Ukitaka uone raha ya kwenda kibabe na Marekani, kwenye mkutano wa kuzungumzia muafaka wa vita vya Ukraine ambapo Trump amepanga kukutana na Putin hakuna taifa lolote la Ulaya wala Ukraine yenyewe haijaalikwa. Wababe tu watakaa mezani.

Akielezea maono yake ya kutetereka kwa world order Trump pia alisema:

"Ningependa kurejeshwa kwa Urusi katika G7, ambayo ilisimamishwa mwaka 2014 baada ya Moscow kutwaa rasi ya Crimea ya Ukraine. Nadhani lilikuwa kosa kumtoa nje ya G7 (Putin)"
– Trump
  • Kwa nini Trump anataka China, Urusi na Marekani zipunguze nusu ya bajeti zao za ulinzi?
  • Kupunguzwa kwa bajeti na matumizi ya hivi majuzi nchini Marekani ina maana kuwa haiwezi kumudu bajeti yake ya kijeshi?
  • Kwa nini Marekani imechachamaa kuzitaka nchi za NATO kutumia 5% ya GDP zao kwenye masuala ya ulinzi? Je, Marekani imelemewa?
Dunia inahitaji sana balance of power sio nani superpower
Huyu jamaa kaka kivingine tofauti na mwanzo, Dunia itamuelewa Kwa urahisi sana
 
makadirio ya wataalamu wengi wanaoifuatilia China ni kwamba bajeti yao halisi ni mara mbili ya ile ambayo serikali huwa wanaisema
Acha uongo hizo ni propaganda China wanatumia sana mfumo wa stimulus measures kuboost consumption
 
China wanapika takwimu zipi?
Screenshot_20250216-020444_X.jpg
 
Pia fahamu kwamba ukiwa huna barabara za lami ukijenga utaonekana zaidi kuliko mwenye lami ambaye anahitaji kurekebisha mashimo tu.
"China's progress in advanced infrastructure is more than 100 times faster than the US."
Elon Musk (Feb, 2018)
 
Ni kawaida kwa serikali ya China kuzipa ruzuku kampuni zilizowekeza China it doesn't matter ni domestic au foreign companies

Kwa hiyo usidhani ni Elon Musk pekee ndiye aliyefaidika au anayefaidika na Chinese govt subsidies

Kwa kufanya comparison ya modern infrastructures kati ya China na Marekani bila kubishana China imeiacha kwa mbali Marekani
 
Mabepari wanakimbilia kuweka viwanda China na Asia kwa sababu ya Sweatshops ambazo ni ngumu kuweka US au Ulaya. Wamarekani hata kazi ngumu za mashambani wamewaachia immigrants, kwenye call centres za makampuni ya US nako Wahindi makapuku wamejaa.
Acha kupotosha watu China ndiyo inaongoza mwa mataifa yaliyowekeza nchi za Asia kwa wingi.

Angalia hapo kwenye mfg investment

Umeona gap ambalo China amempiga Marekani, South Korea na Japan?

20250216_025425.png

Kwa hiyo Mchina ni bepari sio?
 
Wamarekani hata kazi ngumu za mashambani wamewaachia immigrants, kwenye call centres za makampuni ya US nako Wahindi makapuku wamejaa
Unajua sera ya Trump ya MAKE AMERICA GREAT AGAIN inalenga nini hasa?

Kuirudisha tena Marekani kwenye uchumi unaotegemea mfg industries badala kutegemea tu financial service

Mfg industry ndiyo ilifanya Marekani na nchi za Ulaya ziwe na uchumi mkubwa tangu kipindi cha industrial revolution

Later mfg Industry ndiyo imefanya uchumi wa China, Japan, South Korea uwe mkubwa. Mfg Industry ndio real economy

Ndiyo maana hata kiwango cha ukuzi wa uchumi wa Marekani na Ulaya ni kidogo sana

Mr MAGA anatamani sana arudishe uchumi wa viwanda ila sio jambo la overnight process inahitaji kuandaa supply chain, skilled personnel n.k

Achana na hizo blaah blaah zako sijui Wahindi mara immigrants
 
Humu kuna kulishana matango pori. Ninachojua hii ni tecnic nyingine USA anataka kutumia kuzidhoofisha Urusi na China. Lkn najua hawatamkubalia . Mengine tusidanganye hunu . Hakuna mwenye taarifa kamili juu ya bajeti ya kijeshi ya nchi husika zaidi ya kilee kinekuwa reported au kutumia google kama source ya taarifa au media nyingine. Hakuna kitu kinaitwa Balance of Power, chenye ukweli, kila nchi inatamani kuwa super power kwa nyanja zote za maisha. Ukisikia mgomvi wako anasema tuache kupigana jua mkao aliokuwepo haukuwa rafiki, ila akikaa vzr ataanza ugomvi. USA ameona kwa sasa dunia itamfanya fukara kuliko kwa kuwa technolojia imepanuka hata nchi za kawaida zinaweza kumletea madhara maana zinapata support toka China au Urusi.
USA ni wajinga tuu. Mbona Afrika haji na sera za economic sharing ili kuzikwamua nchi hizi ambazo zimewekewa mtego wa mikopo ili ziendelee kuwa tegemezi? Ameleta Demokrasia ilia kwa ujinga qa Qaafrika wabaki wanakimbizana na utamaduni wasioujia na kuiba mali zao wenyewe kwa kutumia madaraka vibaya? Mbona hasimamii hili. Mfano ni DRC hapo wapo kuiba na hawana hata huruma.
Rubbish idea
 
Back
Top Bottom