Trump anataka Marekani, China na Urusi zipunguze nusu ya bajeti zao za ulinzi. Pia anapenda Urusi irudishwe kwenye G7

Deni la taifa lina shida gani kwa Marekani?
Marekani bado ina afford kuwa na deni la taifa la ukubwa wowote ili mradi halichochei inflation ya kupitiliza, debt servicing ya kupitiliza na dollar bado ni sarafu ya kimataifa. Hiyo ni faida ya wao kumiliki sarafu ya dollar($). Hata hivyo hii ni mada ngumu sana ambayo huwezi kuilewa kirahisi.
 
Ni nani alikwambia Marekani ina afford? Kila mwaka wanafikia ukomo wa kukopa (debt ceiling) ila wanaona hawana namna wanakopa tena

Deni la Marekani liko katika mfumo wa bonds na wanawalipa kwa interest rate billions of dollars waliowakopesha

Na hata bunge la Marekani limekuwa likisema gharama wanazotumia kulipa madeni zingeweza kutumika kwenye mambo mengine ya economic devpt ila inaishia kuwalipa creditors

Ingekuwa Marekani inamudu deni tungesikia wamemaliza deni na halikui na tusingesikia kuhusu debt ceiling

Unajua kila mwaka Marekani inawalipa kiasi gani creditors wake?
 
Debt ceiling ni jambo la kisiasa tu kudhibiti executive na sheria tu za kuongoza matumizi ya serikali wala haina maana yoyote kiuchumi. US wanatumia 3% tu ya GDP kulipia deni.
Kila mara unarudia wangetumia hizo pesa hivi na vile kufanya hiki na kile kama vile hawazitumii hivyo. Nusu ya bajeti ya Marekani inatumika kwenye Social Security na Medicaid. Serikali kuu ya Marekani inatakiwa kutoza kodi vizuri tu mabilionea kama hao kina Elon Musk na wenzake na makampuni yao. Nusu ya deni la US ni kutokana na tax cuts za Republicans kwa mabilionea na Corporations.
 
Ushajiuliza kwa nini viongozi wanaapa? Unayajua yale maneno wanayo yatamka yana maana gani....?Maana kiapo kimoja wapi ni kutunza siri cha nchi.

Huwezi kujua wala kuambiwa kila kitu na hasa kwenye maswala ya ulinzi, ndio kabisa cha kukuambia wanakichagua wao.
 
Kupunguza bajeti za kijeshi sio rahisi wakati kuna vita vinaendelea huko Ukraine.
 
Super power sio mbwembwe na kujitutumua tu. Ni kuwa na influence ya uchumi, jeshi, utamaduni na soft power katika sehemu kubwa ya dunia.
Ndio maana Usupa-pawa wa Urusi tuliuita wa 'mchongo' ila Warusi wa JF walitupinga Sana.
 
Kitu ambacho watu hawakifahamu humu ni kwamba huku tunakoelekea lazima tu Russia itajiondoa ndani ya Ukraine na Ukraine itarejea kwenye mipaka yake ya kabla ya 2014.

Russia imeshatambua kwamba faida itakayopata kwa kunyakua ardhi ya Ukraine ni ndogo sana kuliko faida itakayopata ikirejea kwenye umoja na wazungu wenzao.

Na inaonekana hili ni swala ambalo Trump na Putin tayari wameshalizungumzia na kukubaliana kabisa sasa wanatafuta tu ni namna gani litatekelezwa.

But because of the myopic nature of many people and coupled with the passion for harbouring fanatical sentiments, this issue proves evasive to most of them to realize although it's the reality that will happen in not so distant future.
 
Kitu ambacho watu hawakifahamu humu ni kwamba huku tunakoelekea lazima tu Russia itajiondoa ndani ya Ukraine na Ukraine itarejea kwenye mipaka yake ya kabla ya 2014.
Ndoto za mchana
 
Russia imeshatambua kwamba faida itakayopata kwa kunyakua ardhi ya Ukraine ni ndogo sana kuliko faida itakayopata ikirejea kwenye umoja na wazungu wenzao
Ilikuwa Ukraine ijiunge NATO na kuwekwa kambi za kijeshi za NATO kinyume na makubaliano au mikataba iliyosaniwa awali

Sasa iko wazi baada ya Russia kuivaimia Ukraine hakuna Ukraine kuwa member wa NATO ameshasema waziri wa ulinzi wa Marekani
 
Kupunguza bajeti za kijeshi sio rahisi wakati kuna vita vinaendelea huko Ukraine.
Yeah hakuna taifa lolote kati ya hayo matatu litapunguza bajeti yake.

China naye inazidi kujiimarisha katika eneo la Indo-Pacific huku lengo lake kuu ni kukirudisha kisiwa cha Taiwan (ROC) chini ya PRC
 
Debt ceiling ni jambo la kisiasa tu kudhibiti executive na sheria tu za kuongoza matumizi ya serikali wala haina maana yoyote kiuchumi. US wanatumia 3% tu ya GDP kulipia deni.
Debt celing sio jambo la kisiasa, iko hapo iki uonyesha mwelekeo wa deni la taifa. Kutambua mwelekeo wa deni la taifa ni siasa?

Unafikiri kutumia 3% ya GDP kulipa madeni ni pesa ndogo? Hiyo ni highest ratio tangu 1996 na inazidi kuongezeka

Thats why wakaja ma debt ceiling wewe unasema siasa wakati wenzako wameona mbali kuwa mwelekeo wa deni kuongezeka utazidi kupandisha ratio ya malipo na crisis
 
Unafikiri Marekani hawakusanyi kodi? Mzee kodi wnakusanya ila tatizo matumizi ya serikali yanazidi mapato
 
Kuna ndoto za alinacha alafu kuna alinacha... Sasa wewe ndio alinacha mwenyewe 😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…