Mtu yeyote anayeongozwa na mihemko na chuki za kidini huwa hana mantiki kabisa hivyo akitaka kushambulia kwa nyuklia atafanya tu, angalia hata juzi kwa namna Iran ilivyokua inashambulia kwenda Israel, ilikua haijalishi mabomu yanalenga wapi, isingekua kwa mifumo ya kiulinzi ya Israel ama kwa hakika hayo madude yangefuta hako kainchi.
Pakistan na India lichaa ya udini ila kidogo wana kaundugu, wakishtuana wao huzingatia umakini....
Tafuta haka kainchi kanakosababisha watu watokwe mipovu na mikanzu yao, katafute kwenye hii ramani, hiyo MAD doctrine haiwezi kusaidia hapa, yaani warhead moja tu ya nyuklia inakafutia mbali hata muda wa kujibu hautapatikana.
MAD ipo kwa mataifa makubwa kama Urusi na Marekani, pale kabla projectile ifike kwenye nchi moja, wao watakua wamepata fursa ya ku-counter launch ya kwao pia zipishane, tufe na nyie mfe.....pia taifa kubwa kama Marekani labda ulipige mfululizo wa manyuklia mengi ndio uwalemaze, lakini ukipiga jimbo moja, wao wana majimbo mengine mengi yatajibu huko, maana manyuklia yao hayapo kwenye jimbo moja.
Sasa Israel kainchi kadogo hata kuliko jimbo la Arusha, bomu moja ya nyuklia ikishatua tu ndio basi wamefutika.
Namna wagaidi wa uislamu akina HAMAS hushambulia Israel, hudhihirisha jinsi wanataka kufuta hako kainchi, wao hufanya scorch earth attacks, haka kainchi kanaishi tu kwa neema za Mungu.
View attachment 3382759