Trump asitisha misaada yote ya kijeshi ya Marekani kwa Ukraine

Rais Donald Trump ameagiza kusitishwa kwa usafirishaji wa msaada wa kijeshi wa Marekani kwa Ukraine baada ya mvutano mkali kati yake na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, wiki iliyopita katika Ikulu ya White House, afisa wa Ikulu ameiambia CNN Jumatatu.

Hatua hii, iliyokuja baada ya Trump kufanya mikutano kadhaa na maafisa wa juu wa usalama wa taifa, inaweza kuwa na athari kubwa kwa uwezo wa Ukraine wa kupambana vitani, kwa mujibu wa maafisa na wachambuzi. Kusitishwa kwa msaada huo kutaendelea hadi Trump atakapojiridhisha kuwa Zelensky amejitolea kuanzisha mazungumzo ya amani, hatua ambayo inamlazimisha Rais wa Ukraine kwenda kwenye meza ya mazungumzo kwa hofu ya kupoteza msaada zaidi wa kijeshi.

“Rais amekuwa wazi kuwa anazingatia amani. Tunahitaji washirika wetu pia waonyeshe dhamira hiyo. Tunasitisha na kupitia upya msaada wetu ili kuhakikisha kuwa unachangia katika kutafuta suluhisho,” afisa wa Ikulu alisema.

Baada ya zaidi ya wiki moja ya uhasama wa wazi kati ya Washington na Kyiv, kusitishwa huku kwa msaada ni dalili dhahiri ya kuzorota kwa uhusiano kati ya nchi hizo tangu Trump alipoingia madarakani.

Katika wiki za hivi karibuni, Trump ameonyesha msimamo unaofanana na Rais wa Urusi, Vladimir Putin, kwa madai ya uongo kuwa Ukraine ilianzisha vita na kumshutumu Zelensky kuwa dikteta. Hata hivyo, uamuzi wake wa kusimamisha msaada wa kijeshi unaweza kuwa na athari kubwa kwenye mwelekeo wa vita na kumpa Putin nguvu zaidi.

Msaada huo utasitishwa kwa vifaa vyote vya kijeshi ambavyo bado havijaingia Ukraine, maafisa wamesema, na hii ni hatua ya moja kwa moja kutokana na kile Trump anachokiona kama “tabia mbaya” ya Zelensky wiki iliyopita.

Maafisa wa Magharibi wanasema Ukraine inaweza kuendelea kupambana kwa wiki chache — labda hadi mwanzoni mwa majira ya joto — kabla ya kusitishwa kwa msaada huo kuanza kuwa na athari kubwa. Utawala wa Biden ulikimbilia kuisambazia Ukraine silaha nyingi katika siku zake za mwisho, ukiiwezesha nchi hiyo kupata hifadhi kubwa ya silaha za hali ya juu.

Ni silaha hizo za kisasa — zikiwemo makombora ya masafa marefu ya ATACMS — ambazo zimeiwezesha Ukraine kushambulia ndani ya ardhi ya Urusi. Mkakati huu unaweza kudhoofika ikiwa silaha hizo zitasalia kusitishwa.

Source: CNN
Usa ilichelewa kupata Rais kama huyu zile
Nimeanza kumdharau
Ukiwa huwezi kufikiri utamdharau tu
 
Hapa sio swala la miaka mingapi hapa ni suala la kuona kuwa hivi vita tuliyo jiingiza imeenda nje ya matarajio yetu , hivyo tutafute namna ya kuondoka ili mwisho wa siku tusipate aibu.
Na kujitoa kwenye misaada na mashirika ya kidunia walipanga lini? Mkuu, hapa ni Trump kaja na maono yake.
 
Zile kelele za USA mifumo ndo inaendesha nchi, wenzetu wanalolifanya leo lilishapangwa miaka 20 iliyopiya na raisi ni mzimamizi tu tuziache sasa.

Tumeshajionea.
Trump kapindua meza aisee..
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
ARV za bure naona zimefika mwisho hata kabla ya miezi 3
 
Nadhani hata kabla ya Mabishano hayo Trump alikusudia muda kusitisha misaada ya kijeshi kwa Ukraine! Hata Marekani ingeendelea kuipa msaada Ukraine hakuna uwezekano wa kuishinda Russia na kurejesha maeneo iliyoyateka.
 
apo a
Rais Donald Trump ameagiza kusitishwa kwa usafirishaji wa msaada wa kijeshi wa Marekani kwa Ukraine baada ya mvutano mkali kati yake na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, wiki iliyopita katika Ikulu ya White House, afisa wa Ikulu ameiambia CNN Jumatatu.

Hatua hii, iliyokuja baada ya Trump kufanya mikutano kadhaa na maafisa wa juu wa usalama wa taifa, inaweza kuwa na athari kubwa kwa uwezo wa Ukraine wa kupambana vitani, kwa mujibu wa maafisa na wachambuzi. Kusitishwa kwa msaada huo kutaendelea hadi Trump atakapojiridhisha kuwa Zelensky amejitolea kuanzisha mazungumzo ya amani, hatua ambayo inamlazimisha Rais wa Ukraine kwenda kwenye meza ya mazungumzo kwa hofu ya kupoteza msaada zaidi wa kijeshi.

“Rais amekuwa wazi kuwa anazingatia amani. Tunahitaji washirika wetu pia waonyeshe dhamira hiyo. Tunasitisha na kupitia upya msaada wetu ili kuhakikisha kuwa unachangia katika kutafuta suluhisho,” afisa wa Ikulu alisema.

Baada ya zaidi ya wiki moja ya uhasama wa wazi kati ya Washington na Kyiv, kusitishwa huku kwa msaada ni dalili dhahiri ya kuzorota kwa uhusiano kati ya nchi hizo tangu Trump alipoingia madarakani.

Katika wiki za hivi karibuni, Trump ameonyesha msimamo unaofanana na Rais wa Urusi, Vladimir Putin, kwa madai ya uongo kuwa Ukraine ilianzisha vita na kumshutumu Zelensky kuwa dikteta. Hata hivyo, uamuzi wake wa kusimamisha msaada wa kijeshi unaweza kuwa na athari kubwa kwenye mwelekeo wa vita na kumpa Putin nguvu zaidi.

Msaada huo utasitishwa kwa vifaa vyote vya kijeshi ambavyo bado havijaingia Ukraine, maafisa wamesema, na hii ni hatua ya moja kwa moja kutokana na kile Trump anachokiona kama “tabia mbaya” ya Zelensky wiki iliyopita.

Maafisa wa Magharibi wanasema Ukraine inaweza kuendelea kupambana kwa wiki chache — labda hadi mwanzoni mwa majira ya joto — kabla ya kusitishwa kwa msaada huo kuanza kuwa na athari kubwa. Utawala wa Biden ulikimbilia kuisambazia Ukraine silaha nyingi katika siku zake za mwisho, ukiiwezesha nchi hiyo kupata hifadhi kubwa ya silaha za hali ya juu.

Ni silaha hizo za kisasa — zikiwemo makombora ya masafa marefu ya ATACMS — ambazo zimeiwezesha Ukraine kushambulia ndani ya ardhi ya Urusi. Mkakati huu unaweza kudhoofika ikiwa silaha hizo zitasalia kusitishwa.

Source: CNN
hapo anaepoteza ni USA , miaka 10 mbele tutakuja elewa , Ukraine haiez poteza sababu UKRAINE ni mwanamke ambae alikuwa anagombaniwa , yaan UKRAINE ndo ilikuwa reference nan ni mbabe wa dunia , Urusi kajiongezea ushawishi duniani kwa kusimamia msimamo wake licha ya kukosea , hakuna taifa lenye kiongoz timamu litakuja msikiliza USA tena
 
Asee hii point kubwa sana. Baada ya hii U turn iliyopigwa na US ni uhakika kwamba raisi aliyepo madarakani ndio anaamua afuafe uelekeo gani hakuna cha system wala nini.
hayo maamuz ya Trump kujitenga na west , yatamcost muda si mrefu , nasikia anapambana atawale kama Putin , ila akijichanganya akatoka madarakani wamarekani hawatamwacha salama , nmeona platform za wamarekan wakimlaumu Trump kwa haya maamuz yake anayafanya tangu kuingia madarakani
 
Aliyeanza kumchokoza mwenzie ni Zelenskyy mwenyewe - kwa kufunga safari kutoka Ukreni na kwenda kumpigia kampeni Kamala Harris dhidi ya Trump.

Kwa maneno mengine alikuwa anautangazia umma kwamba Trump hafai hata jino moja.

Kwa mantiki hiyo, Trump naye anamjibu - inakuwaje mtu asiyefaa leo awe bora?

Zelenskyy ni kibaraka, na daima anaburuzwa na mabwana zake wanaompangia nini afanye, lipi aachane nalo.

Jamaa anashikiwa akili, hana maamuzi yake mwenyewe.
Dah zele kipande hiki aliyumba,Bora angekausha tu
 
Trump anafanya kazi kama mwanamke Kila kitu visasi
Tatizo la Trump siyo kisasi kwa Ukraine bali tatizo lake ni kutaka kumfurahisha Putin.

Kosa analofanya Trump sasa ni marudio ya makosa aliyofanya George Bush ya kuivamia Iraq, na Putin ya kuivamia Ukraine. Putin na George bush walikuwa na kichwa kikubwa kuamini kuwa majeshi yao yana nguvu sana yanaweza kufanya lolote. Kosa la Trump sasa hivi ni kuamini kuwa Marekani ina nguvu sana inaweza kufanya lolote. Kama ambavyo Bush na Putin walivyojutia (japo kimya kimya) makosa yano, ndivyo trump pia atakavyojutia makosa yake ingawa yeye ana ego ya kutotaka kukukubali makosa.
 
Back
Top Bottom