Trump asitisha misaada yote ya kijeshi ya Marekani kwa Ukraine

Hakuna cha points, issue imekuja baada ya deal la Trump kutaka kufyeka rasimali za Ukraine kuyeyuka.
Mkuu, dili liko pale pale. Hakuna kitakachobadilika. Ni suala la muda mtu.

Trump anakwambia dili liko mezani na litasainiwa katika muda mwafaka.

Ukreni haina namna. Imeshakula vya Marekani, ni muda sasa wa kuvilipa.
 
Kwa nini leo wakati yeye amekuwa hivyo muda wote na sababu inajulikana.
Lingechukuliwa ni kama vazi la kitamaduni tu kama mkuu wa nchi ya Papua new Guinea angevaa sketi
Kuwa hivyo muda wote (mazoea) haina maana kwamba ndiyo kanuni.

Jamii ya watu wanaopenda kuishi kwa mazoea ndio wale wanaoumia na kuathirika zaidi pale kiongozi sahihi anapoingia na kuanza kusimamia utekelezaji wa matakwa ya sheria na taratibu husika.
 
Zile kelele za USA mifumo ndo inaendesha nchi, wenzetu wanalolifanya leo lilishapangwa miaka 20 iliyopiya na raisi ni mzimamizi tu tuziache sasa.

Tumeshajionea.
Subiri Matokeo. Hata JFK alitaka kusimamisha kabisa vita ya Vietnum. And he got all support from gvt.

we know what happened . Wenzetu wapo smart , hawatotumia strategy ile ile ya JFK
 
Tsh umenichekesha.
 
  • Kicheko
Reactions: Tsh

Megalodon, wamarekani ni wanadamu tu kama wewe, wanakosea pia tena wanafanya makosa mengi mno na makubwa. Sio invincible wala sio kwamba kila wanachokipanga kinakuwa kama walivyopanga, wao ni viumbe tu.

Hollywood ni maigizo tu yale, akina Rambo, James Bond na wenzao ni uongo tu. Na hata katika huko kuigiza wanakosea pia, sikuambii maisha halisi.
 
Zile kelele za USA mifumo ndo inaendesha nchi, wenzetu wanalolifanya leo lilishapangwa miaka 20 iliyopiya na raisi ni mzimamizi tu tuziache sasa.

Tumeshajionea.
iiiiii enhee
ingdwry4ibufcrg09j6053964da3c64.jpg
 
  • Kicheko
Reactions: Tsh
Halafu deni liko pale pale bado marekani atamdai ukraine mabilion aliyotumia wakati wa vita. Na je ulaya itamsapoti mpaka aweze kumshinda mrusi? Ulaya ikiungana na ukraine dhidi ya urusi na china itaungana na urus ndo kitaumana wakati huo mmarekani amdkaa pembeni anaangalia hiyo movie,

Hakuna deni. Mikopo yote huwa ina documents zizosainiwa. Hata Trump hajawahi kutamka kuwa Ukraine ilikopa kitu chochote toka USA.

Mnaokoteza maneno yasiyo halisia na kuyapa uzito.

Trump alisema kuwa kama Ukraine haitaki kuipa UZA madini yake, USA inaweza kutaka ilipwe msaada ambao imeisaidia wakati wa vita.

Kama una akili timamu, tangu lini msaada ukadaiwa ulipwe!!
 
Megalodon, wamarekani ni wanadamu tu kama wewe, wanakosea pia tena wanafanya makosa mengi mno na makubwa. Sio invincible wala sio kwamba kila wanachokipanga kinakuwa kama walivyopanga, wao ni viumbe tu.

Hollywood ni maigizo tu yale, akina Rambo, James Bond na wenzao ni uongo tu. Na hata katika huko kuigiza wanakosea pia, sikuambii maisha halisi.
Ndo ukweli wenyewe huo
 
🤣🤣🤣🤣🤣 Utasikia kule mpaka Congress ipitishe, raisi hana maamuzi ya moja kwa moja bila Congress. Funzo: Raisi ndio final say hio mifumo ni porojo tu.

Mifumo yetu ipo tofauti sana na ya kwetu.

Msaada kwa Umraine ulipitishwana Congress, Trump hana uwezo wa kuufuta mpaka apate baraka za kufanya hivyo kwenye Congress. Ndiyo maana amesema kuwa anasitisha upelekaji wa msaada huo Ukraine. Hajafuta, kwa sababu hana uwezo huo.

Ufahamu kuwa maamuzi yakishafanywa na Congress, anayesimamia utekelezaji siyo Congress, bali ni Serikali, na mkuu wa Serikali ni Rais. Ingekuwa huku kwetu, Rais angeweza hata kufuta moja kwamoja, na asiwepo wa kuhoji.
 
Mikakati iliyopangwa miaka mingapi iliyopita mkuu? Tupange.
Ww kama umeanza kufatilia siasa za kimataifa mwaka 2020 unaweza ukawa sawa.
Lakini kama ni mfuatiliaji wa sera ya nje ya Marekani huwezi kushangazwa na yanayo ikuta Ukraine.
Marekani iliikimbia na kuitelekeza serikali ya kipebari ya Vietnam baada ya kuzidiwa kwenye uwanja wa vita na mwishowe Vietnam yote ikangukia kwa wakomonist .
Marekani ali itelekeza serikali ya Afghanistan na mwisho wa siku ikaangukia mikononi mwa Talban ambayo walitumia zaidi ya $4tirion kuiondoa madarakani.
Marekani aliivamia Libya kwa kisingizio cha kupeleka baadae akaitelekeza na mpaka sasa haitawaliki.
Sasa ni kipi kinacho washangaza kwa Ukraine?
 
Subiri Matokeo. Hata JFK alitaka kusimamisha kabisa vita ya Vietnum. And he got all support from gvt.

we know what happened . Wenzetu wapo smart , hawatotumia strategy ile ile ya JFK
Lakini mwisho wa siku Marekani sialiikimbia hiyo vita?
Maana yake kama walimuuwa JFK kwa sababu ya kutaka kusimamisha vita ya Vietnam badae walijiona wajinga maana JFK ilikuwa ameona mbali kusitisha vita kabla ya madhara zaidi kutokea.
 
Kuwa hivyo muda wote (mazoea) haina maana kwamba ndiyo kanuni.

Jamii ya watu wanaopenda kuishi kwa mazoea ndio wale wanaoumia na kuathirika zaidi pale kiongozi sahihi anapoingia na kuanza kusimamia utekelezaji wa matakwa ya sheria na taratibu husika.
Mimi naona hayo sio mazoea ni utaratibu mpya aliyojiwekea kutokqna na hali ya nchi yake. Kwa sababu hayuko utupu Trump anatakiwa amuelewe au wasibgekubali aende maana walijua atakuwa hivyo. Hapo watakuwa na jambo lao tu lingine
 
cha kwanza kabisa Hiyo ni misaada ambayo ilikuwa Poland tayari.
 
Rais Donald Trump ameagiza kusitishwa kwa usafirishaji wa msaada wa kijeshi wa Marekani kwa Ukraine baada ya mvutano mkali kati yake na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, wiki iliyopita katika Ikulu ya White House, afisa wa Ikulu ameiambia CNN Jumatatu.

Hatua hii, iliyokuja baada ya Trump kufanya mikutano kadhaa na maafisa wa juu wa usalama wa taifa, inaweza kuwa na athari kubwa kwa uwezo wa Ukraine wa kupambana vitani, kwa mujibu wa maafisa na wachambuzi. Kusitishwa kwa msaada huo kutaendelea hadi Trump atakapojiridhisha kuwa Zelensky amejitolea kuanzisha mazungumzo ya amani, hatua ambayo inamlazimisha Rais wa Ukraine kwenda kwenye meza ya mazungumzo kwa hofu ya kupoteza msaada zaidi wa kijeshi.

“Rais amekuwa wazi kuwa anazingatia amani. Tunahitaji washirika wetu pia waonyeshe dhamira hiyo. Tunasitisha na kupitia upya msaada wetu ili kuhakikisha kuwa unachangia katika kutafuta suluhisho,” afisa wa Ikulu alisema.

Baada ya zaidi ya wiki moja ya uhasama wa wazi kati ya Washington na Kyiv, kusitishwa huku kwa msaada ni dalili dhahiri ya kuzorota kwa uhusiano kati ya nchi hizo tangu Trump alipoingia madarakani.

Katika wiki za hivi karibuni, Trump ameonyesha msimamo unaofanana na Rais wa Urusi, Vladimir Putin, kwa madai ya uongo kuwa Ukraine ilianzisha vita na kumshutumu Zelensky kuwa dikteta. Hata hivyo, uamuzi wake wa kusimamisha msaada wa kijeshi unaweza kuwa na athari kubwa kwenye mwelekeo wa vita na kumpa Putin nguvu zaidi.

Msaada huo utasitishwa kwa vifaa vyote vya kijeshi ambavyo bado havijaingia Ukraine, maafisa wamesema, na hii ni hatua ya moja kwa moja kutokana na kile Trump anachokiona kama “tabia mbaya” ya Zelensky wiki iliyopita.

Maafisa wa Magharibi wanasema Ukraine inaweza kuendelea kupambana kwa wiki chache — labda hadi mwanzoni mwa majira ya joto — kabla ya kusitishwa kwa msaada huo kuanza kuwa na athari kubwa. Utawala wa Biden ulikimbilia kuisambazia Ukraine silaha nyingi katika siku zake za mwisho, ukiiwezesha nchi hiyo kupata hifadhi kubwa ya silaha za hali ya juu.

Ni silaha hizo za kisasa — zikiwemo makombora ya masafa marefu ya ATACMS — ambazo zimeiwezesha Ukraine kushambulia ndani ya ardhi ya Urusi. Mkakati huu unaweza kudhoofika ikiwa silaha hizo zitasalia kusitishwa.

Source: CNN
Chiiz huyu mwehuu
 
Usa ilichelewa kupata Rais kama huyu zile hela nyingi zilikuwa zinaishia kwenye mifuko ya watu.
 
Safi sana Trump Sasa si mnaona Trump anataka amani ila Volodymyr Zelenskyy yeye anafanya ubishi tu
Mpwa ubishi kusaini mkataba WA bulllshit mpwa pls

UNATAKA aman uchukue madini yanguu

Shenziyakee

.......naaaa
 
Back
Top Bottom