Trump atangaza kutoshiriki tena midahalo ya urais

Kama Obama mwenye asili ya watu kutoka Africa ameweza kuwa raisi wa USA, basi sina shaka na Kamala kuwa raisi pia, marekani imefikia hatua ya kutoangalia rangi/jinsia hasa kwenye nafasi nyeti kama hii.
 
Kama Obama mwenye asili ya watu kutoka Africa ameweza kuwa raisi wa USA, basi sina shaka na Kamala kuwa raisi pia, marekani imefikia hatua ya kutoangalia rangi/jinsia hasa kwenye nafasi nyeti kama hii.
Dunia ipo kwenye mapigano,
Kama wanaume wenyewe ndio hao wakina Trump, wamarekani watakuwa sahihi zaidi kuchagua mwanamke.
Hapo umekosea,Akili ya waMarekani walio wengi wanaweza kama Trump,ndiyo maana anaenda kushinda uchaguzi tena,kwanza ahadi alizoziahidi kwamba anaenda kuzitekeleza atakaposhinda uraisi,waMarekani wote wenye hali za kawaida wanaenda kumpigia kura,ila ukisoma au kusikiliza media zilizopo ambazo ni asilimia 90 zinamchukia Trump utadhani Trump anapoteza,lakini kiuhalisia Camala anaenda kuburuzwa siku ya tarehe 5 November.
 
Kaka hakuna chombo Cha habari kimeonyesha kumchukia Trump, na bahati nzuri madahalo unafanyika hadharani wala sio chumbani wala vichochoroni, alafu kumbuka wamarekani wengi wanaunga mkono misaada inayotolewa kwenda Ukraine, Trump kashindwa kueleza atamaliza vipi hiyo vita. Trump kiasili ni dicteta,
 
Tena trump ni dikteta kweli! Kuhusu Harris anashinda mchana kweupe,kwanza trump alivyokuwa anaingia tu ukumbini alionekana kumhofia sana Harris,swala la marekani kutokuongozwa na mwanamke hayo yalishapitwa na wakati, ukiongelea kuhusu Clinton unakosea kipindi Kili huyo trump alikuwa hajulikani tabia zake
 
Tena hata Mimi napenda sana anavyo cheka wanaomkataa rudieni mahojiano yake na wakuu wa vyombo vya usalama walivyokuwa anawahenyesha,huyo ndio Kamala Harris
 
Namna ambavyo atatatua mgogoro wa Ukraine hawezi kuutangazia ulimwengu na adui akiwa anasikia, Trump ana akili sana, hilo swali hata mimi siwezi kujibu ni siri yangu. Kama amepanga kuingia vita na Rusia ili ashnikize vita uishe mnalitaka asema mzozo huo ataumaliza kwa mbinu gani? Putin alipata kiburi na kuona kuwa USA na NATO wanamuogopa, ilitakiwa tangia mwanzoni kila silaha anayotumia Rusia kumpiga Ukraine na Ukraine anatumia hiyo hiyo silaha, kama ni long or short range, missiles, herpersonic na ngede na wao wanajibu mashambulizi hivi hivi/
 
Wali moto mchuzi moto, Midahalo inampaisha sana Harris na Trump akikataa tena kufanya naye mdahalo pia ni msala mwengine kwanini anakataa? haya yoote ni maswali ambayo wazungu watagundua nani anafaa.

Ule mdahalo wa juzi Trump aliongea uongo mara 31+ na kusema Springfield wageni wanakula mbwa na paka jambo ambalo Meyor wa mji amekataa na kusema ni uongo uliokubuhu na sasa wazungu wana mock Trump kwa viji clips vya kuchekesha chekesha vya mbwa na paka mitandaoni
 
Mwana mama alivaa hereni za kisasa ambazo ni earphone hivyo kuna uwezekano wa kituo kilichoendesha mdaharo kikachunguzwa. Isitoshe alikuwa anakatishwa mara kwa mara kumtoa kwenye mstari.
Hii ni propaganda nyengine haipo kwenye chanzo chochote, nafkiri ni sadiki ukipenda
 
Baada ya uchaguzi, tutarudi kwenye huu uzi. Panapo uzima.. Trump ataukwaa tena Uraisi. Sitajibu mpaka uchaguzi upite.
Mimi sina mengi ila kwa ninavyoijua Marekani hilo la Trump kuukwaa tena uongozi sidhani. Sumu haionjwi mara mbili na kosa si kosa ila kurudia kosa.
 
πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜† Harafu Chadema watalaumu CCM kukataa midahalo.
 
hayo yote mimi pia niliyaona nilipenda ...sana sauti ya yule mama very calm ..anatema fact and logic

lakini sidhani kama atashinda uyu mama maana wengi wetu hatuamini sana kwamba mwanamke anaweza kuwa kiongozi ikiwemo na mimi
 
Kumbe tatizo lako si herufi L wala R, tatizo lenu (Tlaatlaah. chiembe na wewe ChoiceVariable) ni lile lile moja...U tatu, Uchawa, Utumwa na Ujinga!
ni muhimu kuwa wangwana kidogo,
ni uonevu na kwakweli nadhani inaweza pia kua udhalilishaji kwa rais kushindanishwa na makamu wa rais m myonge na asie na uhakika sana na anachozungumza...

hata ifanyike midahalo 100,
Kamala Haris hawezi kumshinda Donald Trump kwenye midahalo wala kwenye sanduku la kura....

Ushindi wa Donald Trump utakua ni mkubwa zaidi na wa uhakika zaid ya alivyo mshinda Hilary Clinton katika awamu ya kwanza ya urais....

vijana wamarekani wasaka ajira weupe kwa weusi pamoja na ambao hawakua wameamua bado wamchague nani uchaguzi wa Nov.wameshaamua kwenda na Trump kutokana na sera yake muhimu sana ya uhamiaji na kwahivyo atashinda uchuzi huo kirahisi sana dhidi ya Kamala Haris...

Infact ,
Mdahalo wa Donald Trump na Kamala Haris, ni kama ule wa Dr. Nchimbi na watu dhaifu kama vile akina Myika, Ado na wenzao. sasa wangejadili nini kwa mfano? anaejua mengie muhumu na mwenye majukumu mazito anaejua masuala mazito anaenda kufanya mdahalo au mazungumzo na watu wenye malalamiko na wasiejua kitu, wanaenda kuzungumza nini?πŸ’
 
Na huyu ana asilimia kubwa sana ya kushinda katika uchaguzi ujao na atamuacha mbali Kamala.
Tupe facts zako katika hayo maoni yako. Nini kitapelekea Trump kushinda na sio kushindwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…