Trump atangaza kutoshiriki tena midahalo ya urais

Trump atangaza kutoshiriki tena midahalo ya urais

Tupe facts zako katika hayo maoni yako. Nini kitapelekea Trump kushinda na sio kushindwa?
Hadi uzifahamu siasa za Marekani kwa undani zaidi au uwe umeisho Marekani.

Hapa nikikueleza hutaelewa
 
Dunia ipo kwenye mapigano,

Hapo umekosea,Akili ya waMarekani walio wengi wanaweza kama Trump,ndiyo maana anaenda kushinda uchaguzi tena,kwanza ahadi alizoziahidi kwamba anaenda kuzitekeleza atakaposhinda uraisi,waMarekani wote wenye hali za kawaida wanaenda kumpigia kura,ila ukisoma au kusikiliza media zilizopo ambazo ni asilimia 90 zinamchukia Trump utadhani Trump anapoteza,lakini kiuhalisia Camala anaenda kuburuzwa siku ya tarehe 5 November.
Unachokiandika sio halisi na sio sahihi kwa 100%.
Fahamu haya:
1. Huwezi kuchukiwa na 90% ya media za USA na hapo hapo uendelee kuwepo mpaka leo kwenye kinyang'anyiro cha urais. Hatua ya kwanza tu ndani ya chama chako utakuwa umefutwa. Hivyo sio kweli kuwa Trump anachukiwa na media za USA.

2. Media za magharibi zinazoripoti leo kuwa Trump alizidiwa kwenye kinyang'anyiro cha mdahalo wake dhidi ya Kamala ndio media hizo hizo zilisema Trump alifanya vizuri kwenye mdahalo wake dhidi ya Biden. Sasa upendeleo wa media upo wapi?

3. Trump amesikika akisema atakwenda kuimaliza vita vya Gaza na vita vya Ukraine kufumba na kufumbua macho tu ndani ya masaa 24 tu siku akiapishwa kuwa rais wa USA, lakini ameshindwa kueleza kivipi, sasa wamerekani ni wajinga kiasi gani kumpa tu kura kwa ahadi za namna hiyo?
 
Hadi uzifahamu siasa za Marekani kwa undani zaidi au uwe umeisho Marekani.

Hapa nikikueleza hutaelewa
Hakuna siri katika siasa za USA, tuambie hapa sote tujue.

Mimi nimeangalia mdahalo wa juzi, nimeona vitu vingi ambavyo media zote zimechambua kitu kile kile ambacho mimi nimekisema. Kamala alijiandaa vyema na akaweza kuperform vizuri zaidi.
 
Naona humu wengi vichwa maji kwa hiyo mnataka vita viendelee na hamna habari kabisa kuwa hivi vita vinavyoendelea duniani vikiwa vikubwa itakuwa vita ya 3 ya dunia rasmi ina maana hata sisi waafrika tutahusika. Mtu anataka kumaliza vita ninyi mnamuona fala kisa hajawapa maneno matamu wapumbavu sana. Binadamu ni sikio la kufa.
 
Tena hata Mimi napenda sana anavyo cheka wanaomkataa rudieni mahojiano yake na wakuu wa vyombo vya usalama walivyokuwa anawahenyesha,huyo ndio Kamala Harris
Kuna watu wanadhani juzi Kamala Harris alibahatisha kumning'iniza Trump kwenye mdahalo wakati kwa miaka mingi mnoo Kamala amekuwa akiwaning'iniza wanasiasa na watawala mahakamani, kwenye midahalo, mabaraza nk.
 
hayo yote mimi pia niliyaona nilipenda ...sana sauti ya yule mama very calm ..anatema fact and logic

lakini sidhani kama atashinda uyu mama maana wengi wetu hatuamini sana kwamba mwanamke anaweza kuwa kiongozi ikiwemo na mimi
Mwanamama mpaka sasa katushangaza wengi, na kuna kila dalili huenda akazidi kutushangaza zaidi, maana ana kitu kikubwa na anajaribu kukionyesha kwa wamarekani.

Tujipe muda.
 
Naona humu wengi vichwa maji kwa hiyo mnataka vita viendelee na hamna habari kabisa kuwa hivi vita vinavyoendelea duniani vikiwa vikubwa itakuwa vita ya 3 ya dunia rasmi ina maana hata sisi waafrika tutahusika. Mtu anataka kumaliza vita ninyi mnamuona fala kisa hajawapa maneno matamu wapumbavu sana. Binadamu ni sikio la kufa.
Hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kuelewa kauli ya Trump ya kuimaliza vita ya Gaza na Ukraine ndani ya masaa 24 tu siku akiwa rais wa USA. Trump anabanwa aseme atafanya nini kuimaliza vita na sio kuropoka tu kuwa apewe Urais ili aimalize vita. Maana kila mtu anaweza kusema hivyo, hata kichaa anaweza kusema hivyo hivyo.
 
Kipi bora ni yule mwenye nia ya kumaliza vita au aliyeanzisha na kuendeleza? Na pia hamuwezi kuelewa kama ni kichwa maji.
 
Back
Top Bottom