Trump atishia kusitisha misaada ya Marekani nchini Afrika Kusini kwa kunyakua ardhi kutoka kwa baadhi ya watu

Trump atishia kusitisha misaada ya Marekani nchini Afrika Kusini kwa kunyakua ardhi kutoka kwa baadhi ya watu

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Rais wa Marekani, Donald Trump, ametishia kusitisha ufadhili wa Marekani kwa Afrika Kusini, akidai kuwa "tabaka fulani za watu" nchini humo wanatendewa vibaya sana.

Katika chapisho lake kwenye mtandao wake wa kijamii Truth Social siku ya Jumapili, Trump amesema kuwa Afrika Kusini "inanyakua ardhi" na kwamba Marekani haitanyamaza kwa hilo.

"Marekani haitanyamaza kwa hilo, tutachukua hatua. Pia, nitakata ufadhili wote ujao kwa Afrika Kusini hadi uchunguzi kamili wa hali hii utakapokamilika!" ameandika Trump, kulingana na shirika la habari la Reuters.

Haijafahamika wazi ni nini kilichomsukuma Trump kutoa kauli hiyo, na ubalozi wa Afrika Kusini mjini Washington DC haujatoa tamko lolote rasmi kuhusu suala hilo.

Kwa mujibu wa takwimu za serikali ya Marekani, Afrika Kusini imepokea msaada wa karibu dola milioni 440 kutoka Marekani mwaka 2023.

Soma pia: Trump asitisha misaada ya ARV na dawa za Malaria kwa muda

Kwa sasa, Afrika Kusini inashikilia urais wa G20, nafasi ambayo baadaye itachukuliwa na Marekani.

Mwezi uliopita, Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alisema hana wasiwasi kuhusu uhusiano wa nchi hiyo na Trump. Alisema alizungumza na Trump baada ya ushindi wake wa uchaguzi na anatarajia kufanya kazi na utawala wake.

Trump South Africa.png

=================================================================

US President Donald Trump has asserted South Africa is “confiscating” land and “treating certain classes of people very badly” as he announced he was cutting off all future funding to the country pending an investigation.

The land issue in South Africa has long been divisive, with efforts to redress the inequality of white-rule drawing criticism from conservatives including Elon Musk, the world’s wealthiest person, who was born in South Africa and is a powerful Trump adviser.


South African President Cyril Ramaphosa last month signed a bill that stipulates the government may, in certain circumstances, offer “nil compensation” for property it decides to expropriate in the public interest.

“South Africa is confiscating land, and treating certain classes of people VERY BADLY,” Trump wrote on his Truth Social platform on Sunday.

“I will be cutting off all future funding to South Africa until a full investigation of this situation has been completed!” Trump wrote.

Pretoria argues the bill does not allow the government to expropriate property arbitrarily and must first seek to reach agreement with the owner.

However, some groups fear a situation similar to the Zimbabwe government’s seizure of white-owned commercial farms, often without compensation, after independence in 1980.

Later, in a briefing with journalists, Trump said that South Africa’s “leadership is doing some terrible things, horrible things” without giving examples.

Source: The Guardian
 
Huku USAID wanaotusaidia kujenga vyoo, condom, vyandarua nk nao naona wanazidi kukabwa:
View attachment 3223372
Mbona Chapisho hili halihusiani na mada?

Huku USAID wanaotusaidia kujenga vyoo, condom, vyandarua nk nao naona wanazidi kukabwa:

semaga ulijengewa choo mwenyewe na kuvikwa kondomu mwenyewe🤣🤣🤣🤣
 
Mbona Chapisho hili halihusiani na mada?

Huku USAID wanaotusaidia kujenga vyoo, condom, vyandarua nk nao naona wanazidi kukabwa:

semaga ulijengewa choo mwenyewe na kuvikwa kondomu mwenyewe🤣🤣🤣🤣
Jumatatu njema kama hii alafu Una hasira to the maximum, why?
Hujui Elon ni nani kwenye uongozi wa Trump?
 
kuna kasoro sehemu kuhusu taarifa hiyo ya Wazungu kunyanga"nywa mali. Na kwa msingi huo natilia mashaka kama ni kweli Trump ameyasema hayo. na sio hivo tyu huko kwao marekani wameshindwa kuwapa watu wao Punda zao na Mashamba. 40acre and a Mule wanapata wapi kiburi yao?



<>hii ppp itajaleta hayo hayo mbeleni. Nikumbusheni 30 yrs from today
 
Mambo mengine ni kujiendekeza tu Marekani anatoa msaada wa $400milion kila mwaka kwa S.Afrika,sasa kwa ukumbwa wa uchumi wa A.kusini $400milion ni kitu gani?
Yaani sijui waafika kwanini tunajendekeza kipuuzi namna hii.
 
Jumatatu njema kama hii alafu Una hasira to the maximum, why?
Hujui Elon ni nani kwenye uongozi wa Trump?
Elon ni head of DOGE. kwa sasa. Lakin tofauti na taasisi nyingine hii ni body ya ushauri tu, haina mamlaka ya kufanya changes zozote ama kuamrisha jambo kwenye gov ya marekani.
Kwa sababu si official goverment agency so haitambulic na federal laws kama taasisi zingine.
In simpler term ni watoa ushauri tu
 
Jumatatu njema kama hii alafu Una hasira to the maximum, why?
Hujui Elon ni nani kwenye uongozi wa Trump?
Gaslighting.
Ad Hominem.

Ukasilike ww unitupie mm.
Nimeuliza hilo chapisho lina uhusiano gani na mada zaidi ya ww kuja na mapovu hayo ya choo sijui vyandarua?

Unakariri rightwing news, disinformashion and narrative halafu unashupaza shingo? Give me a break bro

#bigot
 
Habari hizi sizo za kweli na hazitokuja kuwa na ukweli.

In short zimeungwa ungwa Lengo?

Kusengenya.

Kikuu hapa ni kufanya psycho analysis ya mleta mada na post ya mwenzake, agitator #2.

The rest is up to you.
 
Tunachosubiri ni kumpiga bit kagame aache kuisaidia M23
 
Taratibu Trump anaanza kulishughulikia Bara la Africa

Hivi Hapa Tanzania hawa Marekani wanafadhili Nini?

Je, wanawazidi China?

Nimekaa pale 🐼
 
wakati nimepigwa risasi ya sikio mlishangilia sana sasa ni muda wenu wa kulia na kusaga meno🥵
Screenshot_20240714-174333~2.jpg
 
Trump anataka kuikomesha Sauth Afrika kwa kitendo chake cha kujifanya inamshitaki Netanyahu kipindi kile yupo vitani kule Gaza. Hiyo sababu ya ardhi ni kipitio tu
 
Taratibu Trump anaanza kulishughulikia Bara la Africa

Hivi Hapa Tanzania hawa Marekani wanafadhili Nini?

Je, wanawazidi China?

Nimekaa pale 🐼
Sisi tunafanya biashara na china, Iran na Russia. Hatuhitaji msaada wa Marekani
 
Rais Trump amesitisha misaada yote ya Marekani kwa Afrika Kusini kwa ajili ya mambo fulani mabaya serikali Ile inayowatendea watu wake wakati magazeti ya mlengo wa kushoto kule yakifumbia macho.
Obviously haya mambo mabaya yamefanywa dhidi ya watu wa mlengo wa kulia.
 
Back
Top Bottom