Trump atoa onyo la mwisho kwa Hamas. Atangaza kuipa Israel kila aina ya msaada ili kuimaliza vita ya Gaza!

Trump kasema anaitaka Greenland, Canada, Panama Canal, Gaza n.k kote huko kaangukia pua.

Executive orders zake za mihemko kila kukicha zinapigwa chini na mahakama.

Soon Wamarekani wataanza kumpuuza.
 
na iran haina kitu sasaivi, hamas msaada watapata wapi? hezbollah haipo, syria haipo. iran wanahaha maisha yameshaanza kuwa magumu hadi makamu wa rais kajiuzulu na rais anatamani kujiuzulu kwa sababu ayatola amegoma kuongea na marekani kuomba pooo na bila hivyo wanasema maisha yanakuwa magumu na pesa hakuna. walimchezea sana biden aliyeondoa vikwazo ndio maana walipata pesa nyingi za kuwapa hamas, hezbollah na huthi, na sasaivi wahuthi hawapumui, muda wowote lolote linaweza kutokea.
 
Hana cha ziada anachoweza kukifanya kuzidi alichokwishafanya Biden.
Sio kweli. Biden hakuwa mkurupukaji kivile. Huyu mwamba ataishangaza sana dunia. Kaanza na wahamiaji eti ni wahamiaji haramu, kafuta ufadhili na misaada yake yote nchi mbalimbali, kaongeza tozo kwa majirani zake Mexico na Canada, kesha gombana na swahiba wake Zelensky, kesha anzisha mchakato wa kujitoa umoja wa NATO n.k. na sasa anavikoromea vikundi vya kigaidi e.g. ameanza na Hamas bado Hezbollah n.k.....Dah! jamaa kaja mbio kweli.
 
Anachuna uso baada ya habari za kuongea na Hamas kisirisiri kuenea
 
Wacha we! Ewoooomi! ya kweli hiyo? ni majan au unga?
Ila magaidi wapumbavu sana. Wanakaa na maiti za watu kweli..ni mtu mwenye shida ya akili tu anaekaa na maiti aliyoiua.
Na najua kiburi chao watadharau na ndio hapo naona vifo vya watu 60 elfu kuongezeka mara mbili..yatabaki magofu tu
 
Na amepania haswa.
Atafanya lakini ndio mwisho wa mchezo wa uonevu duniani.
kumalizika kwa Gaza kutaenda sambamba na kumalizika kwa America na Israel
 
Ila magaidi wapumbavu sana. Wanakaa na maiti za watu kweli..ni mtu mwenye shida ya akili tu anaekaa na maiti aliyoiua.
Na najua kiburi chao watadharau na ndio hapo naona vifo vya watu 60 elfu kuongezeka mara mbili..yatabaki magofu tu
Kama walivyoshindwa kwa zaidi ya mwaka palipobaki ni kushindwa kwao moja kwa moja kwani watu wa Gaza kufa kunatisha lakini si jambo geni tena kwao katika kulinda heshima na dini yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…