Trump atoa onyo la mwisho kwa Hamas. Atangaza kuipa Israel kila aina ya msaada ili kuimaliza vita ya Gaza!

Trump atoa onyo la mwisho kwa Hamas. Atangaza kuipa Israel kila aina ya msaada ili kuimaliza vita ya Gaza!

Trump kasema anaitaka Greenland, Canada, Panama Canal, Gaza n.k kote huko kaangukia pua.

Executive orders zake za mihemko kila kukicha zinapigwa chini na mahakama.

Soon Wamarekani wataanza kumpuuza.
 
Kwa maneno aliyoyaandika raisi wa Marekani Donald Trump kwenye mtandao wake wa kijamii ni rasmi kwamba Hamas inapigana na madola mawili makubwa duniani bila silaha na wakiwa wamezingirwa.
Raisi huyo wa Marekani amesema Hamas iwaachie mateka wote ilionao pamoja na maiti za mateka anaodai iliwaua.Iwatoe leo na wala si kesho.
Kutokufanya hivyo Hivyo Hamas ni kwamba wajihesabu wao ndio basi tena na dunia.Sambamba na onyo hilo kwa Hamas Trump akaongeza kwa kusema tayari ameshawapa Israel kila wanachotaka ili wamalize kazi.

Trump issues 'last warning' to Hamas as US confirms direct hostage talks

na iran haina kitu sasaivi, hamas msaada watapata wapi? hezbollah haipo, syria haipo. iran wanahaha maisha yameshaanza kuwa magumu hadi makamu wa rais kajiuzulu na rais anatamani kujiuzulu kwa sababu ayatola amegoma kuongea na marekani kuomba pooo na bila hivyo wanasema maisha yanakuwa magumu na pesa hakuna. walimchezea sana biden aliyeondoa vikwazo ndio maana walipata pesa nyingi za kuwapa hamas, hezbollah na huthi, na sasaivi wahuthi hawapumui, muda wowote lolote linaweza kutokea.
 
Hana cha ziada anachoweza kukifanya kuzidi alichokwishafanya Biden.
Sio kweli. Biden hakuwa mkurupukaji kivile. Huyu mwamba ataishangaza sana dunia. Kaanza na wahamiaji eti ni wahamiaji haramu, kafuta ufadhili na misaada yake yote nchi mbalimbali, kaongeza tozo kwa majirani zake Mexico na Canada, kesha gombana na swahiba wake Zelensky, kesha anzisha mchakato wa kujitoa umoja wa NATO n.k. na sasa anavikoromea vikundi vya kigaidi e.g. ameanza na Hamas bado Hezbollah n.k.....Dah! jamaa kaja mbio kweli.
 
Rais wa Marekani, Donald Trump, ametoa onyo la mwisho kwa Hamas kuachilia mateka walioko Gaza, akisisitiza kuwa Marekani inaiunga mkono Israel kumaliza suala hilo.

Hii inakuja muda mfupi baada ya Ikulu ya Marekani kuthibitisha kuwa inafanya mazungumzo ya moja kwa moja na Hamas, kinyume na sera yake ya awali ya kutozungumza na makundi iliyoainisha kama ya kigaidi.

Trump ameonya kuwa kutakuwa na madhara makubwa ikiwa mateka hawataachiliwa mara moja, huku akiwataka viongozi wa Hamas kuondoka Gaza. Pia ameonya raia wa kawaida kuwa mustakabali wao unategemea kuachiliwa kwa mateka.

View attachment 3260793

Hii si mara ya kwanza kwa Trump kutoa vitisho dhidi ya Hamas, kwani alitoa matamshi kama hayo Desemba mwaka jana. Ujumbe wake wa hivi karibuni umetolewa baada ya kukutana na mateka waliokuwa wameachiliwa chini ya makubaliano ya kusitisha mapigano.
Anachuna uso baada ya habari za kuongea na Hamas kisirisiri kuenea
 
Wacha we! Ewoooomi! ya kweli hiyo? ni majan au unga?
Ila magaidi wapumbavu sana. Wanakaa na maiti za watu kweli..ni mtu mwenye shida ya akili tu anaekaa na maiti aliyoiua.
Na najua kiburi chao watadharau na ndio hapo naona vifo vya watu 60 elfu kuongezeka mara mbili..yatabaki magofu tu
 
Ila magaidi wapumbavu sana. Wanakaa na maiti za watu kweli..ni mtu mwenye shida ya akili tu anaekaa na maiti aliyoiua.
Na najua kiburi chao watadharau na ndio hapo naona vifo vya watu 60 elfu kuongezeka mara mbili..yatabaki magofu tu
Kama walivyoshindwa kwa zaidi ya mwaka palipobaki ni kushindwa kwao moja kwa moja kwani watu wa Gaza kufa kunatisha lakini si jambo geni tena kwao katika kulinda heshima na dini yao.
 
Back
Top Bottom