Trump hatashinda japo na Kamala Harris hatauweza urais wa Marekani kipindi ambapo taifa hilo linadidimia

Kuna uwezekano hujui mfumo wa uchaguzi wa USA. Jifunze uelewe kuliko Kukulupuka. Mfumo wao ni Bora Sana Ukielewa. Tena Bora Sana
 
Na akishinda itakuwaje?
 
Hata upige albadili, qurujuwan, hata allah ashuke kamwe Kamala hashindi😅😆🤣😂, na waislam si lolote wala chochote kwenye kuamua nani ashinde urais US.
 
Mtoa mada kaa ukijua kuwa USA wananchi pekee hawatoshi kumpigia kura mgombea wa uraisi na akashinda.

Kuna kura zingine special ndo zinaamua nani awe raisi.
 
Mtoa mada kaa ukijua kuwa USA wananchi pekee hawatoshi kumpigia kura mgombea wa uraisi na akashinda.

Kuna kura zingine special ndo zinaamua nani awe raisi.
Nyie watu ni wajinga kweli!

Na hata hamuelewi electoral college ni kitu gani na electors wanapatikanaje.

Kwa ufupi, ingawa sidhani kama una uwezo wa kiakili wa kuelewa, ni kwamba, mgombea anayeshinda popular vote ya jimbo, hao electors wa jimbo wanakuwa wa kwake pia.

Mfumo uko hivyo nchi nzima ukiacha baadhi ya congressional districts katika majimbo ya Nebraska na Maine.

Mgombea hawezi kupata hao electors bila ya kushinda popular vote ya jimbo.

Na hao electors wakikutana ni lazima waakisi matokeo ya kura ya majimbo wanayoyawakilisha.

Najua hii ni rocket science kwa wengi wenu. Hivyo sitarajii uelewe hiki nilichokiandika.

Nevertheless, it’s worth a try.
 
Tuambie
Maana humu wanatudanganya mno🤣
 
Hujapenda maelezo yake?
Maelezo yake Yana uongo mwingi sana. Eti uchumi wa marekani unajua kwa Kasi....mwambie atoe takwimu.

Pia mwambie alinganishe na China aone jinsi anavyompumulia marekani kisogoni.

Eti uchumi wa Urusi unashuka....angalie katika nchi 20 tajiri(G20) ni uchumi upi umekuwa kwa Kasi zaidi mwaka Jana.

Uongo ni mwingi mno
 
Hata upige albadili, qurujuwan, hata allah ashuke kamwe Kamala hashindi😅😆🤣😂, na waislam si lolote wala chochote kwenye kuamua nani ashinde urais US.
🤣🤣Alla ashuke
 
Umeanza na uislamu wakati mimi katika mambo yatakayomuweka Kamalla kwenye kiti cha uraisi nimeutaja mwisho kabisa.Pamoja na hivyo kura za waislamu nazo katika hesabu kila mgombea atazihitaji na kuzipuuza ndio kushindwa katika mbinu za kupata ushindi.
Kura ni za watu hakuna kura za udini kwa sababu hatafutwi mufti mkuu ila anatafutwa rais ambaye ataongoza kwa mujibu wa katiba na hatafuata maandiko ya msaafu wowote.

Remember United States is a secular state just like Tanzania therefore the voting pattern is not based on the people's religious inclinations but party's policies.
 
Huko marekani kura haziamuliwi na waislamu hivyo mkuu usitulishe matango pori hapa.

Hizi mada kuna mahali pake huko nadhani kwenye madrasa zinafaa zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…