Trump hatashinda japo na Kamala Harris hatauweza urais wa Marekani kipindi ambapo taifa hilo linadidimia

Ach

Acha ubishi na uvivu , ww mwenyewe kajifunze wikipedia kuhusu ni kura gani zilimpa urais Donald trump.
Najuwa vizuri we nenda kajifunze utaelewa. Rais wa Marekani haamuliwi na watu wachache. Ukielewa electoral votes ni nini na zifanyaje kazi basi hautabishana hapa
 
Naelewa kwamba Kwa kura za jumla Clinton alipata idadi kubwa ya kura kuliko Trump, lakini kitu unachopaswa kuelewa ni kwamba ushindi wa Urais Marekani haupatikani Kwa hesabu hizo. Nikupe simple calculation tu ni kwamba. Mfano Jimbo la California kama Lina point tatu, mgombea anayemzidi mwenzake Kwa kura za jumla yeye ndo anachukua hizo point tatu (Electoral votes), same applies to other states. So suala la Clinton lilitokea hivi: kuna majimbo alikuwa anapata kura nyingi kulingana na idadi ya watu wa pale ila kama hilo au hayo majimbo yana point tatu, tano kinachokuwa considered ni hizo points siyo idadi ya watu waliompigia kura. But ukija kutafuta idadi ya waalipiga kura unaweza kupata zaidi lakini akazidiwa kwenye electoral votes depending na majimbo ambayo Trump alishinda. Kupata mshindi Huwa zinajumlishwa electoral votes (points) siyo idadi ya kura zilizopigwa.
 
Naomba kujuzwa, kwa nini jimbo moja lipewe point 3 na lingine liwe na point 5, kwa nini yote yasiwe na usawa wa hao wajumbe/point
 
Naomba kujuzwa, kwa nini jimbo moja lipewe point 3 na lingine liwe na point 5, kwa nini yote yasiwe na usawa wa hao wajumbe/point
Hiyo ni kwa sababu ya idadi ya watu waliopo kwenye majimbo.

Majimbo yenye watu/wakazi wengi, electoral college votes zake nazo ni nyingi.

Electoral college votes zinatolewa kulingana na idadi ya wabunge waliopo kwenye chemba mbili za bunge la Marekani: senate na House of Representatives.

Kila jimbo lina maseneta wawili. Hiyo ni bila kujalisha idadi ya watu waliopo kwenye majimbo.

Marekani kuna majimbo 50, hivyo ina maseneta 100.

Kwenye House of Representatives ndo idadi ya wawakilishi hutokana na idadi ya watu/ wakazi waliopo kwenye majimbo wanayoyawakilisha.

Kwa mfano, jimbo la Florida lina wawakilishi 28 kwenye House of Representatives.

Kwa hiyo, kwenye electoral college votes, linazo 30.

Hiyo 30 inatokana na hao wawakilishi 28 ukijumlisha na maseneta wake wawili [2].

Mfano mwingine:

Jimbo la Georgia lina wawakilishi 14 kwenye House of Representatives.

Kwa hiyo kwenye electoral college votes, Georgia inazo 16.

14 kutokana na hao wawakilishi 14 ukijumlisha na maseneta wake wawili [2].

Ili mgombea urais aweze kuzipata electoral college votes za jimbo, ni lazima ashinde popular votes za jimbo.

Iko hivyo kwenye majimbo 48. Majimbo ya Nebraska na Maine, yenyewe huzigawa votes zake kutokana na congressional districts.

Marekani uchaguzi huendeshwa na majimbo. Kila jimbo lina sheria zake za uchaguzi.

Kwa hiyo, Marekani hakuna uchaguzi wa kitaifa.

Chaguzi zilizopo ni za kimajimbo.

Na ndo moja ya sababu kwa nini national popular votes haziamui mshindi wa urais.

Lakini huwezi kushinda electoral college votes bila ya kushinda state popular votes.

Cha msingi ukitaka kuelewa vizuri, ielewe tofauti ya state popular vote [ambayo ndo inatoa electoral college votes] na national popular vote ambayo haitumiki kuamua mshindi.
 
Najuwa vizuri we nenda kajifunze utaelewa. Rais wa Marekani haamuliwi na watu wachache. Ukielewa electoral votes ni nini na zifanyaje kazi basi hautabishana hapa
Unajua trump alishinda uraisi kwa kura gani?

Zitaje?
 
Unajitekenya na kucheka mwenyewe.
 
Unajitekenya na kucheka mwenyewe.
 
Huenda leo ikawa mara ya mwisho asee kabla sijapotea kwa muda ntajitahidi kukujibu kabla sijapotea kwa muda

Kuikwepa Americant na system yao waloieka sio rahisi ingawaje watu wanapambania hilo

Nasababu kubwa nikwamba system inayotawala kwasasa duniani ambayo kiongozi mkubwa ni Americant ila inabeba wahusika wakubwa kama uk ger nk

Huo mfumo kuupita pia inahitaji mikakati mizito na kuja kutimia sio jambo la mara moja

Nikikwambia wafanye nini ntakua nakudanganya sababu inaweza ikawezekana ila isiwe rahisi mfumo ulioanza kujengwa miaka zaidi ya 70 sasa kuondolew ghafla

Napia china na russia au brics wanapambania hilo suala ila wao kama wao hawaelewani

Mfano india na china ila kama kungekua na mfumo thabiti baina ya china na india tu basi system nzima ya huo mfumo ungebadilika

China na india ndio mataifa pekee duniani kama yatakua na ajenda moja duniani wanaweza wakaifanya na ikafanikiwa ndani ya muda mfupi sana ila sharti wawe na maelewano mazuri kwa 100%✓ ila mpaka sasa hilo hawana

Haya mambo ya Geo politics pia sio yakuyaamini sanaa ndio maana licha yakua naongea mengi ila hua nna yangu kichwani hao marekani china russia nk sio wakuwaamini sana kwenye haya majambo

Unaweza ukakuta huku nje wanaugomvi mkubwa haswa ila huko nyuma wana ajenda moja ila wanaijua wenyewe

Dunia inaendeshwa na siri sana mzee tunayoyaona nje ni machache sana kati ya mengi yaliopo
 
Ukilala ukiamka unawaza uislamu na nagaidi yake,wasted sperm🚮
 
Hizi systems nazielewa MKUU ingawaje sio sana ila naelewa kama kuna hayo masuala ya points na majimbo fulani yana points kubwa kuliko mengine

Nandio hapo nnapokua na hoja na yaqini kwamba marekani hakuna demokrasia

Sasa kama kura za watu zinakuja kuamuliwa Kwa points hizo za huko kwenye majimbo hapa unaweza ukanambia maoni mawazo namachaguo ya watu wapi yameheshimiwa?

Si tunakubaliana kwamba wananchi ndio waamuzi wa rais ama madiwani ama wabunge kwenye kupiga kura ama hatukubaliani?

Sasa kwanini kama ipo hivyo maamuzi yamwisho yasiwe tu yawananchi kwakua wao ndio wanamtaka raisi

Inamaana uchina nao wana demokrasi safi maana wao wameamua kutowapa shida raia wao kama wanavyopewa raia huko marekani na system yao wanaambiwa wakapige kura ila mwisho electrol ndio wanamaamuzi ya mwisho

Nnachotaka mimi hapa kubishiwa nikunambia tu kama sio kweli kura za wananchi ndio zinazomueka rais madarakani ila ukishakubali kama kuna electrol nawao wanafanya yao huko utakua unaungana nami

Yaani mfano kenya wawe na system yao wananchi wanachagua rais wao halaf mwisho kuwe na baraza fulani tuseme la mahakama ndio wanaamua nani awe rais huu utakua uhuni mkubwa

Marekani hakuna na hakujawahi kua na demokrasia kama ipo inatakiwa kura za wananchi ziwe ndio maamuzi ya mwisho sababu wao ni wengi kuliko hao wengine wajanja 400

Wananchi pekee hawatoshi kua waamuzi wanani awe rahisi hapo marekani nahuu ndio ukweli
 
Hii inazidi kujazia nyama kwamba marekani hakuna demokrasia kuna janja janja

Kwanini zisiheshimiwe kura za wananchi walopiga kura zao kama wana demokrasia

Marekani sawa wanafanya uchaguzi kwa majimbo ila wapiga kura si wananchi

Wangekua na demokrasia kweli wangeshindwa kuchukua kura za kila jimbo wakazichanganya wakampata mshindi alochaguliwa na raia akaingia ikulu

Tunajua mnajaribu kuuficha ukweli ila ndio ukweli kwamba marekani maoni ya raia kupitia boksi la kura hayaheshimiki hata kidogo na yanapuuzwa
 
Sawa mkuu nimekuelewa ila unasemaje kwamba wananchi hawana maamzi wakati ili uchukue hizi points( electoral votes) lazima uwe umechaguliwa na wananchi wengi katika Jimbo husika). Please note that electoral votes zinazungumziwa siyo watu maalumu wanaopiga kura siku ya tarehe 05 Nov nimeamua kujaribu kuzifafanua kama points ambazo zimekuwa asigned Kwa kila Jimbo based on various criterias.
 
Nimekuelewa sana pia

Sasa kwanini matokeo ya mwisho tu kwamba Hillary alimshinda DT kwa kura nyingi yasiwe final say kwamba Hillary aingie ikulu

Kama kweli kura zawananchi pekee zatosha kua mwamuzi
 
Nimerejea tena hapa kukuelewesha kuhusu electoral votes.
Kwa kuwa umetumia mfano wa Hillary Clinton kushindwa na Trump kwenye uchaguzi wa mwaka 2016, basi ngoja nianzie hapo hapo.

Mara baada ya kura za jumla za wamerekani kupigwa (kabla ya kura za wajumbe kupigwa), na Hilary kuongoza kwa zaidi ya kura milioni mbili, alitangaza kushindwa na dunia nzima ikajua tayari Hilary ameshindwa. Kwanini atangaze kushindwa na kila mtu ajue Hilary ameshindwa wakati kura za wajumbe (electoral votes) zilikuwa bado hazijapigwa (zilikuja kupigwa wiki kadhaa baadaye)?
Jibu ni moja tu, kura za wajumbe ni kivuli cha taswira ya maamuzi ya mamilioni ya wamerekani waliyoyafanya kwenye sanduku la kura hapo kabla.

Kwa kumalizia tu, uchaguzi ule uliompa Trump ushindi ulitokana na ushindi wa Trump kupata kura nyingi zaidi kwenye majimbo muhimu yenye nguvu ya kuchangia ushindi wa kiti cha urais. Upigaji wa kura USA upo kimajimbo, na kila jimbo lina mchango wake tofauti na jimbo lingine. Ukielewa hili hauwezi kuja kubisha tena.
 
Wewe sasa ndio unaweza ukawa hunielewi nasidhanii kama hii hoja unanielewa

Kinachoendelea marekani ndio kama kinachoendelea uk wanadanganya watu malkia sijui mfalme sio mwanasiasa wakati huo huo ili uwe PM lazima ipite idhini yake

Moja ya points kubwa inayopewa jimbo fulani kua na nguvu ni uwingi wawatu

Kwanini wapiga kura wasitoshe kua waamuzi wamwisho

Mwisho umerudi pale pale kwenye points yaani mtu anazidi kwakura 2M bado anatangaza kushindwa

Kura zawananchi haziheshimiwi na Hillary alikiri sababu system ishaekwa walivyoamua kuieka lazima ifuatwe Hillary lazima angekiri

Ila ukweli hauondoki wala kubadilika kama maamuzi ya raia zaidi ya 2M hayajaheshimiwa

Huu ukweli hata muupake rangi vipi hauwezi kubadilika wazeee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…