Naomba kujuzwa, kwa nini jimbo moja lipewe point 3 na lingine liwe na point 5, kwa nini yote yasiwe na usawa wa hao wajumbe/point
Hiyo ni kwa sababu ya idadi ya watu waliopo kwenye majimbo.
Majimbo yenye watu/wakazi wengi, electoral college votes zake nazo ni nyingi.
Electoral college votes zinatolewa kulingana na idadi ya wabunge waliopo kwenye chemba mbili za bunge la Marekani: senate na House of Representatives.
Kila jimbo lina maseneta wawili. Hiyo ni bila kujalisha idadi ya watu waliopo kwenye majimbo.
Marekani kuna majimbo 50, hivyo ina maseneta 100.
Kwenye House of Representatives ndo idadi ya wawakilishi hutokana na idadi ya watu/ wakazi waliopo kwenye majimbo wanayoyawakilisha.
Kwa mfano, jimbo la Florida lina wawakilishi 28 kwenye House of Representatives.
Kwa hiyo, kwenye electoral college votes, linazo 30.
Hiyo 30 inatokana na hao wawakilishi 28 ukijumlisha na maseneta wake wawili [2].
Mfano mwingine:
Jimbo la Georgia lina wawakilishi 14 kwenye House of Representatives.
Kwa hiyo kwenye electoral college votes, Georgia inazo 16.
14 kutokana na hao wawakilishi 14 ukijumlisha na maseneta wake wawili [2].
Ili mgombea urais aweze kuzipata electoral college votes za jimbo, ni lazima ashinde popular votes za jimbo.
Iko hivyo kwenye majimbo 48. Majimbo ya Nebraska na Maine, yenyewe huzigawa votes zake kutokana na congressional districts.
Marekani uchaguzi huendeshwa na majimbo. Kila jimbo lina sheria zake za uchaguzi.
Kwa hiyo, Marekani hakuna uchaguzi wa kitaifa.
Chaguzi zilizopo ni za kimajimbo.
Na ndo moja ya sababu kwa nini national popular votes haziamui mshindi wa urais.
Lakini huwezi kushinda electoral college votes bila ya kushinda state popular votes.
Cha msingi ukitaka kuelewa vizuri, ielewe tofauti ya state popular vote [ambayo ndo inatoa electoral college votes] na national popular vote ambayo haitumiki kuamua mshindi.