6 Pack
JF-Expert Member
- Apr 17, 2022
- 3,952
- 8,807
Niaje waungwana
Kabla ya biashara ya utumwa, pamoja na ukoloni kuanza hakuna mwafrika hata moja aliekuwa na ndoto au fikra za kwenda kuishi Ulaya.
Ni wazungu ndio walioanza kutufuata sisi kwetu Afrika ili kutuibia, kututesa, kutudhalilisha na hata kutuua.
Kama hiyo haitoshi wazungu hao hao waliamua kuwachukua mababu zetu kwa nguvu na kuwapeleka Ulaya na Marekani ili kuwafanyisha kazi ngumu zisizokuwa na malipo.
Baada ya vuguvugu la waafrika kudai uhuru kwa njia mbali mbali, na kukomeshwa maswala ya mababu zetu kupelekwa Ulaya kwa nguvu. Ulaya ilitoa uhuru butu kwa nchi zetu, huku wakiwa wametengeneza mazingira ya kuendelea kutunyonya na kututawala kupitia mlango wa nyuma.
Jinsi miaka ilivyokwenda ndio waafrika tuliendelea kufungua macho na kugundua njia zinazotumiwa na wazungu kutuibia. Wazungu baada ya kugundua hilo wakaiona hatari mbele yao, hivyo wakatengeneza mazingira ya kuanzisha vita katika nchi zetu ili iwe rahisi kutuibia wakati sisi tukiwa tunapambana na fupa la kupigana wenyew kwa wenyew.
Hapo ndio waafrika walipoamua kutoka kwa wingi katika nchi zao na kukimbilia Ulaya, Marekani, Asia na kwengineko ili kutafuta sehemu salama ya kuishi baada ya wazungu kutengeneza mazingira ya kuchafua nchi zao.
Bila wazungu kuvamia Afrika hakuna mtu ambae angekuja kwenu. Tungeishi kama walivyoishi mababu zetu kabla ya ukoloni.
Tukija kwa waarabu nao. Hii ipo wazi kwamba miaka ya 90s kwenda chini waarab hawakuwa wanaifikiria Ulaya kama sehemu yao ya kuishi. Bali wengi walienda Ulaya kwa sababu za kibiashara, kusoma, kutembea nk.
Mwaka 2003 baada ya Marekani kuivamia Iraq kwa lengo la kwenda kuwaibia mafuta yao kwa nguvu, hapo ndio uhamiaji wa waarabu ulipoanzia. Maana vita haikuwa ni ya jeshi peke yake bali mpaka raia wa kawaida waliuwawa.
Kama hiyo haitoshi Marekani ikaanzisha vikundi vya kigaidi vya kuchinja watu hovyo katika ardhi ya Iraq ( hii ni kwa mujibu wa Hillary Clinton ) mtu ambae anaijua Marekani zaidi kuliko mtu yeyote ataekuja kupinga. Vikundi hivyo vikaratibiwa na kupewa msaada wa silaha na Marekani ili kuyumbisha usalama katika eneo lote la mashariki ya kati. Hii huenda ilikuwa na malengo mawili.
1. Lengo la kwanza kuja kuyatumia hayo makundi baadae kuivamia Iran ambae ndio adui mkuu wa Marekani.
2. Na pili kuyatumia kuvuruga usalama wa nchi ili vyombo vya usalama vya serikali visiweze kufika katika maeneo ambayo Marekani na washirika wake wanajichotea mamilioni ya mapipa ya mafuta kila siku bila kudhibitiwa na serikali.
Sasa katika mazingira kama hayo Trump alitegemea raia wangeishi vipi kama sio kutoka na kukimbilia huko kwa wapanga mipango ya kuvuruga amani katika nchi zao ili na wao wakaitafune cake yao ya taifa huko huko kwa waibaji wa rasilimali zao!!
Marekani kwa kuamini yeye yupo mbali amekuwa akivamia na kuvuruga nchi za watu akiamini kuwa waathirika wa uvamizi huo hawawezi kuifikia nchi yake kiurahisi. Sana sana watakimbilia Ulaya kupitia Italy, Spain, Uturuki, Mayotte nk.
Hivyo hawakuona hatari kuivamia Afghanistan, Syria, Libya nk.
Halafu leo hii anawalaumu Ulaya kwa kushindwa kuzuia watu aliowavamia yeye mwenyew katika nchi zao.
Hata hivyo Ulaya washukuru Mungu Iran ni Super Power alieweza kuvidhibiti visuper power uchwara vya Marekani na Israel kupindua meza katika nchi yake. Kama wangekuwa dhaifu basi leo hii Ulaya ingepokea maelfu na malaki ya wakimbizi wengine kutoka Iran baada ya serikali yao kuangushwa na Marekani. Ila uzuri hilo limeshindikana na wairani wameendelea kubaki kwao.