A
Anonymous
Guest
FIDELIS Mutakyamilwa bado ana uchungu wa kuona mama yake akifariki kwa kuwa alikosa huduma ya gari la wagonjwa wa dharura kumfikisha hospitali.
Mama mzazi wa kijana huyo mwenye umri wa miaka 43, akiwa mfanyabiashara wa vinyago, eneo la Mwenge, Dar es Salaam, anasimulia kuwa miaka mitano iliyopita, Gloria Mshemezi (71), alipoteza maisha kwa ugonjwa alioleza kuwa ni changamoto ya kupumua.
Anasema mama yake akiwa nyumbani kwake, Madale, alishindwa kupumua na ghafla akadondoka, hapo ndipo alipiga simu hospitali ya Mwananyamala kuomba huduma ya gari la wagonjwa kumuwahisha hospitali.
Namba aliyopiga; 115 – namba ya dharura kuomba gari la wagonjwa, haikuita kabisa, baada ya muda mfupi alipewa namba na jirani na kupiga +255****, ambayo ilipokelewa na kuambiwa gari litafika kuchukua mgonjwa baada ya muda mfupi.
Hata hivyo, gari lilifika baada ya saa moja na nusu, na kumchukua mgonjwa, ambaye hata hivyo hakufika hospitali. Alipoteza maisha akiwa njiani.
Kilio cha Fidelis, kinabeba hali halisi ya upungufu wa magari ya kubeba wagonjwa nchini Tanzania.
Imebainika kuwa Tanzania ina upungufu wa magari ya kuhudumia wagonjwa (Ambulance) 372, hali inayotishia afya na uhai wa Wananchi wa nchi hiyo.
Upungufu wa magari hayo ya wagonjwa unabebwa kwa gharama za kuwepo kwa magari ya kifahari yanayonunuliwa na serikali kwa ajili ya viongozi zaidi ya 2,513 – kila mmoja akiwa na gari lake na dereva anayelipwa mshahara na serikali.
Hadi sasa, Tanzania ina magari 453 nchi nzima ambayo yameelezwa na Wizara ya Afya kuwa ndiyo yanayotoa huduma za dharura kwa wagonjwa, hasa watoto, wazee, wajawazito na wale wanaokumbwa na ajali mbalimbali.
Imebainika kuwa kati ya magari hayo, 79 hayafanyi kazi kutokana na kuwa mabovu na yameegeshwa maeneo ya hospitali au kuwa matengenezo.
Tanzania ina jumla ya hospitali; kuanzia zahanati hadi Hospitali ya Taifa 825, hivyo yakiondolewa magari 453 yaliyopo, kunabaki upungufu wa magari 372 ambayo yanafanya kazi za kuokoa uhai penye dharura.
Imefahamika kuwa Mwongozo wa Rufaa za Afya wa Mwaka 2022, pamoja na Sera ya Afya ya Mwaka 2007, na kuona kuwa magari ya wagonjwa yanatakiwa kuwepo kuanzia ngazi ya zahanati hadi hospitali ya taifa.
Tanzania, chini ya Mpango Mkakati wa Tanzania Miaka Mitano wa Sekta ya Afya (2021 – 2026), unaeleza kuwa huduma za dharura zinahusisha rufaa kutoka kituo kimoja kwenda kituo kingine chenye huduma inayohitajika kwa ajili ya kuokoa maisha ya mgonjwa.
Mwongozo huo unaeleza kuwa kwa kufuata mlolongo wa rufaa kwa wagonjwa, kutalazimika kutolewa kwa huduma za kitaalamu kwa kutumia magari ya kubebea wagonjwa kutoka vituo vya umma na hata vituo vya watu binafsi.
Aliyekuwa Waziri wa Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa ameeleza kuwa hadi Mwaka jana – Machi, 2024, serikali ilikuwa imesambaza magari ya wagonjwa 316 nchi nzima.
Hivyo basi, tangu kuanza kwa mwaka huu, jumla ya magari ya kuhudumia wagonjwa yaliyosambazwa kwenye maeneo mbalimbali yamefikia 137.
MGAWANYO WA MAGARI YA WAGONJWA
Msemaji wa Wizara ya Afya, Roida Andusamile anasema magari ya wagonjwa, baada ya kununuliwa hugawanywa kwenye vituo vya kutolea huduma katika ngazi zote, lakini kulingana na ufinyu wa bajeti uliopo na tathmini ya uhitaji kimkakati, vituo vilivyopo umbali mrefu kufikia hospitali za rufaa, vinapewa kipaumbele zaidi.
Hivi karibuni, mgao wa magari mapya ulifanyika kwa ngazi za vituo vya kutolea huduma ikiwemo ngazi ya msingi pamoja na ngazi ya rufaa.
“Magari 453 yamepelekwa katika ngazi ya msingi, yaani hospitali za halmashauri, vituo vya afya na zahanati. Magari mengine yamepelekwa katika ngazi ya hospitali za rufaa,” amesema.
Hivi sasa Tanzania ina hospitali moja ya Taifa (Muhimbili), hospitali maalum za kitaifa - 6, hospitali za rufaa za kanda - 4, hospitali za rufaa za mikoa - 28, hospitali za wilaya - 85, na zahanati 701.
UPUNGUFU WA AMBULANCE
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, hadi mwishoni mwa mwaka jana, 2024 ilikuwa ikikabiliwa na upungufu wa magari mawili, baada ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Musoma Mjini, Vedastus Mathayo kukabidhi gari moja Novemba, 2024.
Mganga mfawidhi wa hosptali hiyo, Dkt. Esmund Dyegura, amesema kiutaratibu hospitali za mikoa za rufaa zinapaswa kuwa na magari yasiyopungua sita, ingawa pia hutegemea wingi wa wagonjwa wanaohudumiwa.
Kilio cha Dkt. Dyegura ni sauti ya watendaji wa hospiali karibu zote nchini, kuanzia vituo vya afya hadi hospitali ya taifa, Muhimbili.
Aliyekuwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dkt. Festo Dugange amesema serikali imekuwa ikitenga bajeti kwa ajili ya kununua magari ya wagonjwa na kwamba inafanya hivyo kulingana na bajeti iliyopo.
“Utaratibu wa serikali ni kwamba tunaendelea kuandaa mipango ya kupata magari ya wagonjwa katika vituo vya afya na hospitali za halmashauri kwa awamu kwa kadri ambavyo tutapata fedha,” amesema Dkt. Dugange.
MAGARI YA ANASA Vs AMBULANCE
Ufuatiliaji umebaini bei za magari ya kubeba wagonjwa na kubaini kuwa gari moja la wagonjwa ambalo ni aina ya Land Cruise – hardtop, yenye milango mitano; ikiwa imetumika kidogo kutoka Japan au Dubai, inauzwa hadi Shilingi milioni 127.
Hata hivyo, yapo ambayo yanauzwa kutoka nchi hizo yakiwa yametumika kiasi, hivyo kununuliwa kwa hadi Shilingi milioni 73.
Aina hiyo ya gari la wagonjwa ikiwa mpya – kilomita sifuri, inauzwa hadi Shilingi milioni 240.
Endapo magari ya kuhudumia wagonjwa yaliyopo – 453 yatakuwa yamenunuliwa mapya kabisa, kiasi cha Shilingi bilioni 109 zilitumika kwa ajili hiiyo.
Hata hivyo, wananchi wengi wamekuwa wakilalamikia kukosekana kwa magari ya wagonjwa huku viongozi wengi wakionekana kutumia magari ya kifahari.
Bhoke Malese, mkazi wa Kijitonyama, Dar es Salaam, amedai kuwa serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kujiendesha, huku maisha ya watu yakiachwa kwenye mizani ya rehani.
Anasema kwamba endapo Tanzania ingewekeza kwa kiasi kikubwa kwenye sekta ya afya, huenda idadi ya vifo vinavyosababishwa na kukosekana ama kucheleweshwa kwa huduma, vingepungua.
Bhoke ana hoja; kwamba ni vyema serikali ingenunua magari mengi ya viongozi yenye bei nafuu na kiasi kinachobaki kununua magari ya kuhudumia wagonjwa.
Hivi sasa Tanzania ina sera ya ununuzi wa magari ya viongozi ambayo inaelekeza kununuliwa magari mapya – yakiwa na kilometa zero.
Baadhi ya viongozi ambao wamepewa dhamana kuwa na hadhi ya magari mapya ni pamoja na wakuu wa mikoa – 30, wakuu wa wilaya 139, wakurugenzi wa halmashauri 185, mawaziri 26, manaibu mawaziri 25, majaji wa mahakama kuu 16, wakuu wa vyuo vikuu 29 na wakuu wa idara, viongozi wastaafu, taasisi na wakala wa serikali wanaozidi 300.
Jumla ya wakubwa hao wenye kuwa na hadhi ya kupatiwa magari hayo waelezwa kukaribia 1,513, ambapo kila mmoja ana gari la kifahari lenye thamani inayofikia Shilingi milioni 500.
Endapo magari yote hayo yangenunuliwa kwa pamoja, basi serikali ingelazimika kutumia fedha za kodi za Watanzania zaidi ya Shilingi bilioni 756.
Magari ya viongozi hao, mengi ni kutoka Kampuni ya Japan – ya Toyota ambayo hununuliwa kwa kiasi kisichopungua Shilingi milioni 500 kwa gari moja.
BAJETI HAIGUSI SANA AMBULANCE
Bajeti ya Wizara ya Afya ya mwaka 2024 - 2025, neno ambulance limetajwa mara tatu kati ya maneno 63,680. Ni katika ukurasa wa 294.
Katika ukurasa huo, ambulance imetajwa wakati waziri wake wa wakati huo, Ummy Mwalimu akiwaeleza wabunge na wananchi kuhusu kukamilisha miundombinu kwa ajili ya vituo vya uratibu wa magari ya wagonjwa (ambulance dispatch centers).
Pia wakati akielezea mfumo wa uendeshaji ufuatiliaji na uratibu wa magari ya wagonjwa (ambulance dispatch system) na kutoa mafunzo kwa watoa huduma za magari ya wagonjwa (paramedics) kwa kushirikiana na vyuo vya kati na vyuo vikuu nchini.
Pambazuko limebaini kuwa hakuna mahali palipoainisha kuwa kuna ununuzi wa magari ya wagonjwa kwa ajili ya kuokoa uhai.
Katika bajeti ya Mwaka 2023 - 2024, magari ya wagonjwa yametajwa mara nne (ukurasa wa 70 – imetajwa mara mbili; kwamba wizara imefanya tathmini ya magari ya wagonjwa (ambulance) nchini na kwamba serikali inakamilisha taratibu za ununuzi wa magari zaidi.
Pia magari ya wagonjwa yametajwa kwa kutamkwa kuwa – “Uwepo wa magari ya wagonjwa (ambulance) utasaidia kusafirisha wagonjwa mbalimbali wakiwemo akinamama wajawazito kwa wakati kutoka hospitali moja na nyingine.
Na ukurasa wa 201 (kurudia yale yaliyotajwa katika bajeti iliyofuata ya 2024-25).
Pia, neno hilo limetajwa hapa; Kujenga miundombinu kwa ajili ya vituo vya uratibu wa magari ya wagonjwa (ambulance dispatch centers) katika mikoa mitano ya kimkakati kwa awamu ya kwanza na pia kuanzisha mafunzo kwa watoa huduma za dharura nje ya hospitali na kuandaa kanuni za usimamizi na uendeshaji.
Bajeti ya Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) – ya mwaka 2025-26, haijataja hata mara moja neno gari la wagonjwa katika hotuba ya bajeti ya wizara hiyo yenye kurasa 270, ikiwa na maneno 53,730. Tamisemi ndiyo yenye dhamana ya kuwa na bajeti ya magari ya kuhudumia wagonjwa.
HUDUMA KWA MATENGENEZO
Pamoja na uhaba wa magari ya wagonjwa wa dharura, imebainika kuwepo kwa hujuma kwa baadhi ya maeneo, hasa matengenezo.
Katika uchunguzi uliofanywa na gazeti hili kwa muda, imebainika kuwa wakati serikali na wadau wa afya wakiendelea kufanya juhudi za kupatikana kwa magari ya kutosha kwa ajili ya kutoa huduma kwa wagonjwa wa dharura (ambulance), kuna mwelekeo wa hujuma katika hatua za utengenezaji wa magari hayo.
Utengenezaji wa magari hayo uhusisha mameneja usafirishaji wa vituo vinavyoendesha huduma za magari hayo ya kubebea wagonjwa, Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa), wazabuni walioteuliwa na Temesa katika mikoa na wilaya, na karakana binafsi pale ambapo Temesa imeshindwa kukidhi mahitaji ya matengenezo.
Aliyekuwa Waziri wa Afya wa Tanzania, Jenista Mhagama (sasa marehemu) alilieleza gazeti hili kuwa pamoja na juhudi za kupata magari ya wagonjwa, changamoto kubwa imekuwa katika matengenezo ambapo baadhi ya vituo huchelewa kufanya matengenezo ya magari yaliyoharibika.
Mhagama alibainisha kuwa serikali iko katika mchakato wa kuweka mazingira mazuri ya kuhakikisha kuwa magari ya wagonjwa yanatengenezwa kwa wakati kila yanapopata matatizo ya kiufundi.
Waziri huyo mwandamizi katika serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, alielekeza kutafutwa kwa msemaji wa wizara yake ili kupata ufafanuzi zaidi kwa kuwa alikuwa kwenye majukumu mengine kwa wakati huo.
Msemaji wa Wizara ya Afya, Roida Andusamile amelieleza gazeti hili kuwa jukumu la utengenezaji wa magari hayo ya wagonjwa - kwa mujibu wa utaratibu, limekabidhiwa kwa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (Temesa), ambao ndio wanaotakiwa kuratibu na kusimamia matengenezo ya magari hayo.
“Lakini kumekuwa na tatizo kwa baadhi ya magari kukaa muda mrefu kwenye karakana za Temesa pasipo kutengenezwa, ambako kuna athiri mwendelezo wa utoaji huduma,” ameeleza Andusamile.
Andusamile amesema kuwa magari ya wagonjwa (Ambulances) yaliyopo vituo vya kutolea huduma yanatakiwa kuwa katika hali bora wakati wote ili yaweze kutoa huduma kwa wakati pasipo shida yoyote.
“Hii ni pamoja na kuhakikisha yanafanyiwa matengenezo ya kuzuia na kurekebisha uharibu na kuweka mafuta. Vituo katika ngazi zote vinawajibika kutunza na kufanya matengenezo ya magari hayo katika ngazo zote,” alisema.
Mwongozo wa TEMESA wa mwaka 2012, unataka matengenezo ya magari, pikipiki na mitambo ya serikali kufanywa na wakala huo.
PAMBAZUKO limebaini kuwa hivi sasa kuna karakana 30 tu zilizopo katika mikoa 26 ya Tanzania Bara; kati ya hizo, tatu pekee ndizo zilizopo katika ngazi ya wilaya.
Kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa, ofisi au taasisi ya serikali inayomiliki gari linalohitaji matengenezo, hutakiwa kuwasilisha maombi ya matengenezo ya gari, au kujaza Fomu Na. TMSM.1 ya kuomba kufanyiwa matengenezo kinga au matengenezo makubwa ya gari, dereva kusaini kitabu cha mapokezi kwa kuainisha taarifa muhimu kuhusu matengenezo.
Baada hapo, dereva hukabidhi gari na kuondoka huku akitakiwa kusubiri kukamilika kwa matengenezo hayo.
Hata hivyo, katika maeneo ambako karakana za Temesa ziko mbali, mameneja wakala hiyo ya serikali wa mikoa hutakiwa kuhakikisha wanatumia karakana binafsi teule.
Mameneja hao hutakiwa kukabidhi magari husika kwa karakana teule, kusimamia ununuzi wa spea na vifaa kutoka kwa wazabuni na kufuatilia utaratibu wote wa matengenezo, ikiwemo kudhibiti ubora na gharama.
MABORESHO TEMESA
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Temesa, Alfred Mgweno amelieleza gazeti hili kuwa kwa sasa hakuna ucheleweshaji, kwa sababu utaratibu wa utengenezaji magari umeboreshwa kupitia mfumo wa Tehama.
Amesema gari inapopata matatizo au ikiharibika, ofisa usafirshaji katika kituo husika anatakiwa kuingia kwenye mfumo wa Temesa kupitia tovuti (www.temesa.go.tz) na kujaza maelezo ya gari husika, kisha anaelekezwa kutaja vifaa vinayohitajika.
“Baada ya kujaza, maelezo hayo yanahakikiwa na kutajiwa gharama za vifaa hivyo, kisha kuelekezwa kupeleka kwa mzabuni aliyeteuliwa. Hii inafanyika haraka ndani ya siku hiyohiyo...”
“Kama hakuna vifaa vinavyohitajika kwa mzabuni aliyeteuliwa, na ikishahakikiwa pia kweli hakuna utaalamu wa kufanya matengenezo hayo...”
“Ofisa usafirishaji husika atapewa ruhusa rasmi ya kwenda kutengeneza gari kwenye karakana binafsi teule, lakini hii ni baada ya kuthibitishwa kuwa Temesa haina wataalamu na wazabuni wake hawana vifaa vinavyohitajika,” amesema.
USHIRIKA WA KIFISADI
Katika uchunguzi wa gazeti hili imebaini kuwa kumekuwa na tuhuma za ushirika wa kifisadi baina ya wasimamizi wa magari hayo ambayo kutokana na urasimu uliopo katika matengenezo yanayofanywa na Temesa, wengi wamekuwa wakiyafanyia matengenezo kwa dharura kwenye gereji za kawaida – hata zisizokuwa teule kwa kazi hiyo.
Uchunguzi umebaini kuwa kutokana na kukwepa mlolongo wa utaratibu na magari hayo kukaa muda mrefu yanapofanyiwa matengenezo kupitia Temesa, yamekuwa yakipelekwa katika gereji za mitaani, hivyo kuingia katika mzunguko wa wizi wa vipuri.
Mmoja wa wamiliki wa gereji katika eneo la Sinza, Dar es Salaam, (jina linahifadhiwa) amesema kuwa amewahi kukosa kazi ya kutengeneza magari hayo ya wagonjwa kwa kuwa alikataa kuingia kwenye mpango wa wizi wa vipuri na udanganyifu mwingine.
Amesema kwamba alikuwa akisikia kuwepo kwa mpango huo kutoka kwa baadhi ya mafundi wake ambao walikuwa wakifanya kazi maeneo mengine kabla ya kuanza kazi kwake.
“Mimi sikutaka kuingia kwenye dhambi ya wizi kutokana na imani yangu na kumuogopa Mungu, lakini mchezo huo mchafu nasikia ulikuwepo,” amesema.
Katika uchunguzi wake, gazeti hili lilifanikiwa kumpata mmoja wa madereva wastaafu wa magari hayo ya kubebea wagonjwa Mussa Homeli, ambaye amekiri kufanyika kwa wizi huo kwa ushirika wa madereva na wamiliki wa gereji.
Amesema pamoja na kutoshiriki mpango huo wa wizi – kutokana na imani yake, lakini kuna baadhi ya madereva wenzake ambao anasikia walikuwa wanufaika wakubwa wa wizi huo.
ALAUMU AMBULANCE KUPUUZWA
Kila mwaka wa fedha, serikali hutenga zaidi ya Shilingi bilioni 500 kwa ajili ya ununuzi wa magari mapya ya viongozi, matengenezo kwa yale yaliyopo, ununuzi wa mafuta, pamoja na vipuri.
Kiasi hiki ni kikubwa na kimekuwa kikilalamikiwa na wananchi wengi kwa kueleza kuwa serikali inapaswa kuweka bajeti kubwa kuhudumia wananchi zaidi kuliko viongozi pekee.
Imebainika kuwa hakuna ushahidi wa moja kwa moja, endapo serikali imekuwa ikitwenga fedha za kutosha kwa ajili ya matengenezo ya magari ya dharura kubeba wagonjwa – kama inavyotengwa kwa magari ya “wakubwa.”
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu, ameeleza kusikitishwa kwake kukosekana kwa magari ya kutosha ya kuhudumia wagonjwa wa dharura, huku viongozi wakijipangia bajeti kubwa kwa magari yao ya kifahari.
"Tunashuhudia upotevu mkubwa wa fedha unaofanywa na watendaji wa serikali kwa kutumia magari ya starehe, huku wakisahau kununua magari yenye kuokoa uhai wa watu," amesikitika.
UCHUNGUZI ZAIDI
Uchunguzi wetu ulianza kufuatila baada ya kuwepo madai ya mtandao wa ufisadi kwenye matengenezo ya magari ya wagonjwa (ambulance) baada ya kupata malalamiko kutoka kwa baadhi ya ndugu wa wagonjwa waliotakiwa kupata huduma ya magari hayo haraka.
Mmoja wa watu hao ni Aloyce Massalo, mkazi wa Dar es Salaam, ambaye alipoteza mama yake mzazi baada ya kukosa huduma ya ambulance haraka.
Aloyce ambaye ni mtumishi wa serikali anaeleza kuwa kutokuwepo kwa ambulance – wakati huo, kulisababisha kifo cha mama yake, ambaye endapo angewahishwa hospitali angepona.
Mama yake huyo, Magdalena Massalo (miaka 71 – wakati huo, Mwaka 2021)ambaye ni mwalimu mstaafu, mkazi wa Kawe, Kinondoni, alikumbwa na umauti kwa kukosa huduma ya hewa mapema.
AMBULANCE ZAEGESHWA KWA UBOVU
Katika kutafuta ukweli zaidi, lilitembelea hospitali kadhaa ili kupata hali halisi ya huduma ya magari ya wagonjwa.
Katika Hospitali ya Sinza Palestina, Kinondoni, Dar es Salaam, gari la wagonjwa – lenye usajili SM 5833, lilionekana kuegeshwa kwa muda mrefu likionekana kutofanya kazi kwa muda mrefu kutokana na ubovu.
Hali hii ilivuta udadisi wa kutaka kujua iwapo kuna gari la wagonjwa linalofanya kazi hiyo, uchunguzi ambao bado unaendelea.
Katika Hospitali ya Mbagala Zakhem, yenye hadhi ya Hospitali ya Wilaya ilishuhudiwa magari mawili ya wagonjwa yakiendelea kutoa huduma.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mbagala Zakhem, Dkt. Ally Mussa amesema hawezi kuzungumzia lolote kuhusu magari ya wagonjwa kwa kuwa utaratibu wa kujibu maswali unatakiwa kuelezwa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa.
“Ni kweli tumekuwa tukisimamia uendeshaji wa magari yetu ya huduma kwa wagonjwa, tuna taarifa zote hapa kuhusu utaratibu wa matengenezo na mwenendo mzima wa matengenezo, lakini siwezi kusema lolote. Taarifa hizo zinatakiwa zitolewe na ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa,” amesema.
Katika Hospitali ya Temeke yenye hadhi ya hospitali ya mkoa, ambapo lilishuhudia magari mawili ya wagonjwa aina ya Toyota Land Cruiser (Hardtop) yakiwa yameegeshwa tu, huku moja likionekana kuwepo hapo kwa muda mrefu kutokana na kumea kwa nyasi zilizozinga gari hilo.
IDADI YA VITUO HUDUMA
Takwimu za Wizara ya Afya zinaonesha kuwa hadi Desemba mwaka 2023, vituo vya kutolea huduma za afya vilifikia 9,366, idadi inayoanzia kwenye zahanati, vituo vya afya, hospitali za halmashauri, hospitali za wilaya, hospitali za rufaa za mikoa, hospitali za rufaa za kanda, hospitali maalumu na hospitali ya taifa.
Takwimu hizo zinaainisha kuwa mgawanyo wa vituo hivyo ni vituo vya afya – 1,126 (asilimia 12.02), hospitali za halmashauri – 171 (asilimia 1.83), hospitali zenye hadhi ya wilaya -180 (asilimia 1.92).
Pia, hospitali za rufaa za mikoa – 28 (asilimia 1.3), hospitali zenye hadhi ya mkoa- 34 (asilimia 0.36), hospitali za rufaa za kanda – 5 (asilimia 0.05), hospitali zenye hadhi ya kanda - 11 (asilimia 0.12), hospitali maalumu – 6 (asilimia 0.06) na hospitali ya taifa – 1 (asilimia 0.01).
SERIKALI YAJA NA MAJIBU
Baada ya muda mrefu kupata wahusika, hatimaye Pambazuko liliunganishwa na Mtaalamu wa Menejimenti ya Magonjwa ya Mlipuko na Dharura wa Wizra ya Afya, Erasto Odindo ambaye aliomba kutumiwa maswali ili aweze kuyajibu.
Ufuatao ni mtiririko wa maswali na majibu yake, akiwa anawakilisha serikali.
Swali: Katika hospitali hasa za mikoa, ambulance zinahitajika ngapi na zilizopo ni ngapi?
Jibu: Kwa sasa kila hospitali ya rufaa ina ambulance zisizopungua mbili, lakini idadi ya ambulance kwa kila hospitali inategemea idadi ya rufaa zinazotoka katika hospitali hiyo kulingana na huduma zinazopatikana katika hospitali hizo.
Hivyo, rufaa nyingi zinatoka katika ngazi ya msingi kuja katika ngazi ya rufaa ambapo kwa kila halmashauri ina ambulance zisizopungua mbili pia.
Swali: Kitaifa kwa jumla, zinahitajika ngapi na zipo ngapi?
Jibu: Kiwango cha chini kwa mujibu wa Shirika la Afya duniani ni ambulance 1 kwa kila watu 50,000. Kwa nchi yetu tuliweka idadi ya kuwa na ambulance 1,666 kufikia mwaka 2027.
Mwaka 2022 serikali kupitia Wizara ya Afya ilifanya tathmini nchi nzima na kubaini kuna jumla ya ambulance 540 zinazofanya kazi. Ndani ya miaka 3 serikali imenunua ambulance 727, hivyo kufikisha zaidi ya ambulance 1,267 kitaifa.
Swali: Kuna mkakati gani wa kuhakikisha ambulance zinapatikana za kutosha mahitaji?
Jibu: Serikali inaendelea na mpango wake wa kununua ambulance zingine kila mwaka kutegemea na upatikanaji wa fedha ili kufikia lengo la ambulance zaidi ya 1,600 kufikia 2027.
Ambulance hizi zinaenda kuunganishwa katika mfumo wa kitaifa wa huduma za ambulance na kusaidia kupatikana kwa wakati kwa kuzingatia umbali wa hospitali ya rufaa.
Pia, kuimarisha huduma za dharura na huduma ya kwanza kwa majeruhi na wagonjwa wenye dharura zingine za afya kuanzia eneo walipo na njiani wakati wanasafirishwa.
Kwa sasa huduma hizo zimeanza kwa mama na mtoto na muda siyo mrefu huduma zitapanuliwa na kuanza kujumuisha dharura zingine za afya ikiwemo majeruhi wa ajali kupitia namba ya simu ya kupiga ya 115 ambayo ni bure.
Swali: Kwa mwaka huu wa fedha, 2025/26, bajeti iliyotengwa kwa ajili ya ununuzi wa ambulance ni kiasi gani?
Jibu: Serikali inatarajia kuongeza ambulance 200 au zaidi kutegemea na upatikanaji wa fedha. (Alieleza huku bajeti iliyosomwa haina kifungo cha ongezeko hili la ambulance idadi hiyo)
UWIANO WA AMBULANCE KWA WAGONJWA
Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) inapendekeza kiwango cha gari la wagonjwa moja kwa kila watu 100,000, katika mwongozo wa jumla, ila kwa mujibu wa makala iliyochapishwa na National Institutes of Health, baadhi ya nchi zenye kipato cha chini na cha kati huweza kulenga uwiano wa gari la wagonjwa moja kwa kila watu 50,000 ili kukidhi mahitaji ya usafirishaji wa wagonjwa kwa ufanisi.
WHO halijabainisha kiwango maalumu cha uwiano wa gari la wagonjwa kwa idadi ya watu nchini Tanzania, lakini nchi hii inajitahidi kuboresha huduma za dharura za afya.
Juhudi za hivi karibuni za Tanzania ni pamoja na upatikanaji wa magari ya wagonjwa 40 ili kuimarisha huduma za dharura, kama inavyoeleza Ofisi ya Kanda ya Afrika ya WHO.
Baadhi ya halmashauri nchini Tanzania, ikiwamo halmashauri za Kwimba, Tanganyika, Bunda, zimeripoti uwiano mdogo wa gari la wagonjwa moja kwa kila watu 156,500.
Ripoti ya WHO iliyotolewa Machi 20, 2025 ilieleza kuwa Tanzania kwa sasa inakabiliwa na changamoto kubwa kutokana na kiwango cha juu cha vifo vinavyosababishwa na ajali za barabarani.
Nchi nyingi zilizoko kusini mwa Jangwa la Sahara, Tanzania ikiwamo, ambapo ni vifo 16 kwa kila watu 100,000.
WHO inaelea kuwa vifo na ulemavu vingi vinaweza kuzuilika kwa huduma za haraka za dharura.
Hata hivyo, nchi inakabiliwa na upungufu makubwa katika mfumo wa kukabiliana na dharura, ikiwa ni pamoja na ukosefu wa uratibu ulio na muundo rasmi, kutokuwepo kwa huduma maalumu za dharura za matibabu, na kutokuwa na mfumo wa kituo cha kati cha kuratibu magari ya wagonjwa.
Vilevile, mafunzo duni ya huduma ya kwanza, upungufu mkubwa wa magari ya wagonjwa, na watoa huduma wachache wa magari ya wagonjwa vinakwamisha upatikanaji wa huduma madhubuti za dharura na kuongeza vifo vinavyoweza kuzuilika.