TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

Hawa hata wakiongeza data bila network coverage nzuri ni bure, shida wamesharidhika sijui! Wamekazana tu rudi nyumbani rudi nyumbani.
 
Hawa hata wakiongeza data bila network coverage nzuri ni bure, shida wamesharizika sijui! wamekazana tu rudi nyumbani rudi nyumbani.
Wao ndio kila kitu watengeneze network coverage iwepo ya kutosha Kama unavyosema Mkuu kwani hata wasipokuwa na matangazo yeyote wanaohitaji data na zilizo faster ni wengi hao telcom wanauza walikua Kama TTCL walipogundua kuna pesa nje nje wapo serious kweli... TTCL wapo halafu watu wanalipa pesa kupitia mitandao mingine kwa pesa ndefu sijui tatizo lao nini?wangeuza hata wifi za majumbani na ofisini kwa bei nafuu yaani ni tatizo sana hata hawajiongezi kabisaa...
 
Ttcl ofisi zenu za mikoani wekeni wifi bure hapo na iwe ina speed ya kutosha hizo gharama za mabango mtaachana nazo fanyeni vitu kisasa mkifanikiwa mkoani nendeni mpaka wilayani..
 
Wamejaza wazee tu, wao wanahangaika na bills tu za makampuni wanasahau wengi wa buku buku pia tupo [emoji19]
 
Safi sana, ivi mnaweza nipatia namba ya huyu dada aliyefanya hili tangazo?
TTCL Customer Care
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…