Ferruccio Lamborghini
JF-Expert Member
- Apr 15, 2020
- 1,667
- 2,595
Pole kwa changamoto hiyo,tunaomba utufahamishe unapatikana maeneo gani ili tufuatilie na kutatua.Ni kwel nadhani awajawekeza kwenye minara ya kutosha so baadhi ya maeneo inakua shida sana kwenye network sasa inatemea mfano mimi dar sehem nilipokua nakaa line zote zinasoma kwa kasi kubwa sana bila shida leo niko geita sehem niliyopo nikikaa ndani ya nyumba voda aisomi network alafu watu siku izi si wanakimbizana na bando nafuu hapo ndo shida ahahahahahahaha swala la network sio bongo hata ulaya
Pole kwa changamoto hiyo,tunaomba utufahamishe unapatikana maeneo gani ili tufuatilie na kutatua.Dah nilijua ni mm peke yangu imenikuta hii juzi tu hapo aseeh nilikasirika mnoo mpaka asubuhi hakuna nilichokamilisha kupakuwa
[emoji35][emoji35][emoji35][emoji35][emoji35]
Pole kwa changamoto hiyo,tunaomba utufahamishe unapatikana maeneo gani ili tufuatilie na kutatua.Hovyo kabisa. Namaanisha hovyo. Nashangaa wao ndo wauzaji wa internet kwa makampuni mengine ya simu vipi wenyewe wanashindwa kutoa huduma inayoeleweka ata katikati ya miji ukiachana na vijijini. Ningekuwa nauwezo ningewatumbua wote waliipo maofisini.
Pole kwa changamoto hizo,tumepokea na tunafanyia kazi.Natumia TTCL kama mwaka hivi umepita.
Vifurushi vyao sio vizuri sana na havina options nyingi.
Menu yao mfano tu ya kuangalia Salio la Bundle dah ipo ovyo. Yaani ukitaka kuangalia meseji unaangalia peke yake, ukitaka MB peke yake, dakika peke yake.
Speed ya internet sasa. Ikifika jioni hakuna kitu itasoma LTE ila speed ya 2G.
Mzee mbona unatoa povu kama ni kitu personal vile?
TTCL sio mtandao wa kutegemea kwenye intaneti, spidi yake haitabiriki, yaani ni mtandao wa hovyoo
Mimi nilikuwa natumia voda, mb 500 shs 2000, nikahamia TTCL GB 1 tshs 1500
Nikatumia mwezi mmoja tu nikatupa ile line, nikarudi voda japo ni gharama.
Halafu naishi Dar sasa, sijui mkoani inakuaje
Sent using Jamii Forums mobile app
ishu ni spidi sio gharama, mi nilirudi voda jäpo ni ghali ila spidi yao nzuri
Naishi Nkapanya na huku ni kama Newyork vile na huu mtandao wa TTCL.
Hii inawezekana vip kam mtu yupo mbali n ww?Pole kwa changamoto iyo, namba ya TTCL unayo tayari, nikusaide special number??
Unafiki unakusumbua.Mkuu acha kupotosha, binafsi natumia mtandao wa TTCL kupata internet, sijawahi jutia.
Halafu kama salio limeisha mbona hamtumi sms kutoa taarifa?
Sasa mtu unabaki kujiuliza ni salio limeisha au ni mtandao umekorofisha?
Sent using Jamii Forums mobile app
AiisseSio siri ngoja niende kwenya mada moja kwa moja.
Huu mtandao una matatizo mengi sana kama yafuatayo:
1. Huduma ya T PESA
Aisee huu mtandao kama utatuma hela siku ya Ijumaa usiku ghafla litokee tatizo wallah utakuja kuhudumiwa siku ya Jumatatu.
Hili tatuzo limenipata juzi hapa Ijumaa tarehe 7 yaani nilitamani kulia wallah.
2. Vifurushi
Hawa majamaa ukitaka uende nao sawa kwenye masuala ya MBs nakushauri tafuta kitambulisho cha chuo.
Aisee yaani GB 5 kwa Tsh 5000 mwezi mzima.
3. Vocha
Asikwambie mtu, TTCL hawana vocha aisee. Jana nimeenda pale Makao Makuu niliulizia vocha ya 500 hakuna wanasema zipo za 1,000.
Aisee ukienda kuulizia madukani yaani muuzaji anaweza akashangaa maana hiyo vocha ya TTCL ndiyo kwanza anaisikia kwako.
Kilichonipata jana
Nilijiapiza nikaonane na Afisa Masoko pale Makao Makuu pale Posta ili nimshauri kitu kimoja tu. Yaani nikafika mapokezi nikaonane na bwana Kindamba lakini nikazuiliwa.
Yule mama wa mapokezi aliongea sana mpaka wakati naondoka nimeinamishwa kichwa chini kwa masikitiko. Maana shida yangu nilitaka kuonana na Afisa Masoko au CEO wao.
Nilitaka niwambie kama vocha mtaani ni ngumu basi katika option ya kununua bando mteja achague alipe upitia T PESA au salio la kawaida.