TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

Nyumbani kumenoga!
 
Ilibidi uweke na siku kinazodumu, pia hii ni yakwako tu kwahiyo sio kila mtu atapata kama wewe kwa bei hiyo, halafu wanaangalia speed yako kwenye kukitumia wakiona speed yako kubwa wanakupandishia bei
Yah!ni kweli mwanzo nilikua natumia mtandao wa Tigo,nimeona hawana huruma hata kidogo,Kwa sasa naweka pozi Voda wakizingua nitahama tena.
 
Mkuu mimi nilikua na lain moja kwa zaidi ya miaka 12,nimeona baadhi ya mitandao wanafanya kama ndio kigezo cha kunikandamiza,mwezi uliopita nimeenda kununua simu nyingine,Lain ya zamani nitatumia kupokea simu tu,nitakua nanunua line mpya yenye ofa,wakipandisha bei natupa nanunua mtandao mwingine,hivo hivo mpaka tutafika,Tanzania mambo mengi sio rafiki kwa watumiaji wa hali ya chini,naona shida iko kwenye serikali yetu
 
Habari ndugu nilinunua data ya 2GB ya mwezi lakini kila nikiwasha data on hata msg za whatsapp haziingii. Yaani mnaboa sana
 
TTCL wana nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwenye soko kama safaricom ya kenya, ila sijui wanakwama wapi, wajiri wakurugenzi wenye uzoefu na uwezo kwenye telecom industry, haya mambo ya kuchaguana kikada kada ndio yanapelekea kushindwa kusonga mbele.
TTCL kwa namna ilivyo ni kama Tanzania ilivyo kama nchi ina rasilimali ya kila aina lakini bado tupo kwenye wimbi la umaskini.
 
Sasa hapa mtashindana na nani?

Mie nina laini yenu,toka nimeikea hela hata sioni niitumiaje.

Wekeni vifurushi shindani hata huko mnapopatikana tuwatumie vizuri.

Data ndiyo mpango.. Turudi nyumbani.

Panogesheni nyumbani sio maneno maneno tu.
Hicho kifurushi kitakuwa mahususi kwa dakika, mie sijawahi kukitumia sababu wana vifurushi vingi sana na ni nafuu hakuna mtandao unaofikia TTCL kwa unafuu wa vifurushi vyote ikiwemo vya data.
 
Kwa nini ukimpigia mtu mwingine simu mfano, TTCL Kwenda VODA au AIRTEL au TIGO ukimaliza kuongea ile namba ya simu ya mtu uliyempigia kwa TTCL code number inafutika kwa hiyo ukitaka tena kumpigia mtu huyo huyo inabidi tena uende kwenye CONTACT?

Mfano, Mimi nina line ya TTCL huwa naitumia muda wote, nikimpigia mtu mwingine wa VODA au TIGO au AIRTEL nikimaliza kuongea naye ile +255 0....inafutika nikitaka kumpigia tena mtu huyo huyo inabidi tena niende kwenye contact kutafuta namba yake, na hili tatizo ni kwa TTCL tu wengine hawana....ni kwa nini?
 
TTCL, internet yenu ina katakata sana.Nilinunua MB za mwezi mzima lakini unaweza kuweka laini kwenye modem mtandao ukawa haupatikani,ikabidi niendelee kulinufaisha libeberu HALOTEL.Pia mtandao wenu huwezi kununua salio kutoka mitandao mingine, hata kununua salio kutoka mabenki mtandao wenu haukubali.Ukiishiwa na salio hadi utembee sana kutafuta vocha,na mkumbuke wanaojitolea kuuza vocha zenu ni wachache sana.Nilienda kwenye ofisi zenu kuuliza juu ya hili tatizo nika jibiwa kwa kifupi tu kuwa ni kweli huwezi kununua salio kwa njia ya mtandao, nilipouliza kwanini yule mama alijiumuma wala sikumwelewa nikaona nisimchoshe mama wa watu bure.

Huwa nasikia kuwa ninyi ndio mnasimamia internet ,kama ni kweli, basi ama mnahujumu mtandao wetu makusudi au mmenunuliwa na mabeberu.Inakuwaje beberu halotel ukienda vijijini na ukifika kwenye kamji kalikochangamka kasiko na hadhi hata ya makao makuu ya wilaya lakini unakuta wana huduma ya 3G.Ninyi hata makao makuu ya mikoa mtandao haueleweki.Tunajaribu kurudi nyumbani lakini mnatuvunja moyo kwa huduma zenu.Mabeberu wanavuna faida kubwa wakati tunamtandao wetu .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…