TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

TTCL sihitaji hata kuwasikia Mana walinikata hela yangu T pesa bila ridhaa yangu..nikawapigia huduma kwa wateja wanaongea shit..waendelee tu kutumia wao wenyewe...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio siri ngoja niende kwenya mada moja kwa moja.

Huu mtandao una matatizo mengi sana kama yafuatayo:

1. Huduma ya T PESA
Aisee huu mtandao kama utatuma hela siku ya Ijumaa usiku ghafla litokee tatizo wallah utakuja kuhudumiwa siku ya Jumatatu.

Hili tatuzo limenipata juzi hapa Ijumaa tarehe 7 yaani nilitamani kulia wallah.

2. Vifurushi
Hawa majamaa ukitaka uende nao sawa kwenye masuala ya MBs nakushauri tafuta kitambulisho cha chuo.

Aisee yaani GB 5 kwa Tsh 5000 mwezi mzima.

3. Vocha
Asikwambie mtu, TTCL hawana vocha aisee. Jana nimeenda pale Makao Makuu niliulizia vocha ya 500 hakuna wanasema zipo za 1,000.

Aisee ukienda kuulizia madukani yaani muuzaji anaweza akashangaa maana hiyo vocha ya TTCL ndiyo kwanza anaisikia kwako.

Kilichonipata jana
Nilijiapiza nikaonane na Afisa Masoko pale Makao Makuu pale Posta ili nimshauri kitu kimoja tu. Yaani nikafika mapokezi nikaonana na mama ana sura ngumu.

Yule mama wa mapokezi aliongea sana mpaka wakati naondoka nikamtukana kwa sauti ya chini. Maana shida yangu nilitaka kuonana na Afisa Masoko au CEO wao.

Nilichotaka kumwambia afisa masoko
Nilitaka nimwambie kama vocha mtaani ni ngumu basi katika option ya kununua bando mteja achague alipe upitia T PESA au salio la kawaida.
TPESA
Huduma ya TPESA changamoto ziko ila zinashughulikiwa, changamoto za kimtandao zipo kwa operators wote ila la kupata tatizo Ijumaa kushughulikiwa ndani ya siku za kazi ni kweli, TPESA wanahitaji kubadilika

Vifurushi
TTCL wanahuduma nzuri sana kulinganisha na other operators, linganisheni vizuri and fairly

Vocha
Kunachangamoto ya upatikanaji wa vocha za kukwangua lakini unaweza pata vocha kupitia selcom, tingApp, tigo, voda airtel, CRDB, NMB etc, sometime unajiongeza

Kilichokupata jana
sometime Lugha za matusi sio heshima, Mungu kila mtu kampa sura yake kutukana mama zetu sio jambo zuri. je baharia wa buza nikikuambia mama yako anasura NGUMU utajisikiaje????

Kumbuka udada zako, unashangazi zako, una mama wadogo.
 
Hawa majamaa ni wahuni sana hawa yaani nimejiunga GB 10 ili nipakue vitu vangu chaajabu network ipo slow kama kinyonga.

Kesho asubuhi alfajiri na mapema naivunjavunja laini yao kwa meno yangu.
Uzi tayari.
TTCL
KWELI MABORESHO TUMEYAONA KUTOKA KIFURUSHI CHA MB600 KWA 500 HADI KWENDA BUKU.
MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA

#NyumbaniNASEPA
#NyumbaniKUMEROGWA
#NyumbaniKUMEINGIAVICHAA
haaaaaaa babuuuu unapenda kulalamika sana, wamekuongezea dk za kupiga mitandao yote, wamekuongezea SMS bado unalalamika.
 
Back
Top Bottom