TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

- Ni tatizo gani? (T-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)

- Maeneo gani? (Tukifahamu maana ulipo, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate msaada toka kwa wakala wetu aliye karibu nawe)

- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?

- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza.

- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.


Zifuatazo ni ofisi zetu za huduma kwa wateja ndani ya jiji la Dar es Salaam.


1. POSTA
[emoji654][emoji654][emoji654]Mtaa wa Samora, jengo la Extelecom ghorofa la Chini.


2. KARIAKOO
[emoji654][emoji654][emoji654]Mtaa wa Makamba/Msimbazi, jengo la Akamba Bus Service.

3. UPANGA
[emoji654][emoji654][emoji654]Mtaa wa Magole/Maliki, karibu na Diamond Jubilee.


4. MAGOMENI
[emoji654][emoji654][emoji654]Mtaa wa Minaki/Fundiki, karibu na Manispaa ya Kinondoni.


5. KIJITONYAMA
[emoji654][emoji654][emoji654]Kijitonyama Sayansi, barabara ya Ali Hassan Mwinyi/ Rose Garden.


6. OYSTERBAY
[emoji654][emoji654][emoji654]Barabara ya Haile Selassie.


7. UBUNGO
[emoji654][emoji654][emoji654]Jengo la Ubungo Plaza/ Ghorofa la chini.


8. MBEZI BEACH
[emoji654][emoji654][emoji654]Mbezi Makonde/ Jengo la Shamo Tower.


9. TABATA
[emoji654][emoji654][emoji654]Tabata Bima, barabara ya Segerea karibu na kanisa la Romani Katoliki.


10. CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM.
[emoji654][emoji654][emoji654]Jirani na tawi la benki ya NBC, jirani na kilipo kituo cha polisi cha UDSM.


11. BARABARA YA PUGU
[emoji654][emoji654][emoji654]Barabara ya Mwalimu Nyerere, karibu na Sigara.


12. WAGENI
[emoji654][emoji654][emoji654]Uwanja wa ndege.


13. PUGU
[emoji654][emoji654][emoji654]Jengo la Quality Centre, ghorofa la chini.


14. KISUTU
[emoji654][emoji654][emoji654]Mtaa wa Mchafukoge/Libya jengo la Haad Plaza.


15. TEGETA SHOP
[emoji654][emoji654][emoji654]Jengo la Kibo Complex, ghorofa la chini.


16. MWANANYAMALA SHOP
[emoji654][emoji654][emoji654]Mwananyamala A, barabara ya Mwinjuma yalipo makutano ya Mwananyamala A.


17. KURASINI
[emoji654][emoji654][emoji654]Kurasini Exchange Area, jirani na Chuo cha Diplomasia.


Wasiliana nasi:
[emoji337]022 210 0100
[emoji390] 0738 151 511
[emoji273]www.ttcl.co.tz


#RudiNyumbaniKumenoga
View attachment 1529645


Karibu.

Rudi Nyumbani Kumenoga
oya rudisheni social media mnaboa mjue mpaka leo tarehe 1 bado tuu
 
hivi hawa TTCL si wana operate kwa kutumia kodi za Watz, mbona hawapo serious?
 
Nimetumia wifi yao kwa miaka3 nakaa bunju, uzalendo umenishinda nimerudi smile, bure kabisa
 
Ttcl poleni nimevunja line zenu zote ya kwangu ya mke wangu ya mama yangu ya wadogo zangu wawili zote nimezitupa maana hazina faida yoyote uzalendo umenishinda kwa kwel nilijitahidi kuwanunulia line hao nilio wataja lkn badala ya kuheshimu wateja nyie mnaona kama kinyesi
 
TTCL Corporation bandika bandua ya saa mbili ilikuwa sawa, na nightpack ya Gb 10 tena nyie mngefanya unlimited na mngekuwa na vifurushi vizuria sana, sijui mnakwama wapi, kwakweli mnavyoenda nadhani na mara hii kuendesha mtandao utawashinda pia
 
Back
Top Bottom