TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

Nashangaa sana na kujiuliza line za TTCL zitapatikana lini? Mpaka maofisin kwenu hakuna. Wako mawakala anakwambia akusajilie kwa 10000 line moja. Jaman Tanzania ni nini hiki #Waziri nape, #Mkurugenzi mkuu Kampuni??
Unahangaika na laini zao zina maajabu gani?natamani ingekua laini anaweza kupewa mtu bure ningekupa bure
 
Unahangaika na laini zao zina maajabu gani?natamani ingekua laini anaweza kupewa mtu bure ningekupa bure
Naomba tu tutabadili usajili nina kitambulisho cha nida. Hata leo hii nimepita pale ofisi yao makumbusho.
 
Hivi kwa nini ninyi mmekosa ubunifu kiasi hiki aisee?
Mtategemea hadi lini kwamba huo Mkonga wa mawasiliano ndio 80% ya revenue zenu, Why can't come na other creavity mpige hela mbona mnaweza, whats problem?

Staring with...
1. Facilitate internet kwenye mashule yote nchini kwa kuanza muanze na Tech. Sec school, baadae shule nyingine na kuhakikisha kila mwezi wanalipia hiyo huduma kwa shule zilivyo nyingi Bongo mbona kuna hela ya nje nje?

2. Hakikisheni walimu wamegaiwa vishkwambi, good, why cant u come up na bando lao hata la 500 wapate GB hata 1 mbona mtapiga hela sana hadi hvy vishkwambi vipitwe na wakati.

Mna fursa nyingi ila hamzitumii....... shirikianeni na eGA na CoStech mnaweza toboa..

By the way hivi mnajipangaje na Ujio wa Starlink, jitahidi hata muwe agency wa ku supply device zake or else mtakosa kbs kitu cha kfanya na shirika kwa mara nyingine inaenda kufa kwa uzembe wenu!!
TTCL lilishakuwa debe tupu, sijui kama kuna mwekezaji anaweza kulinunua.
 
Hivi hii kampuni Ina shida Gani?
Mkoa wa Iringa tangu mwezi wa 9 mwaka Jana (2022),hakuna line za ttcl !
Na wanaoingia ofisini Kila siku na mishahara wanapata!
Wanasema Mpk makao makuu ,dar?
 
Hivi hii kampuni Ina shida Gani?
Mkoa wa Iringa tangu mwezi wa 9 mwaka Jana (2022),hakuna line za ttcl !
Na wanaoingia ofisini Kila siku na mishahara wanapata!
Wanasema Mpk makao makuu ,dar?
Ucjisunbue juz tu hapa nimetka kurudisha lain pale kijitonyama Sayansi HAWANA KITU wakaniandikia rufaa niend makao makuu kule posta mpya yaan kule napo ndo bure kabisa hawana hata lain.
Inackitisha mpak makao mkauu hawana hata lain
 
Nimeomba huduma ya fiber internet nimejaza form kila kitu ila mwezi unakata hamna cha fundi kupiga simu wala nini
 
Watu wnaa majib ya ovyo
Screenshot_20230407-174609.jpg
 
Nimeomba huduma ya fiber internet nimejaza form kila kitu ila mwezi unakata hamna cha fundi kupiga simu wala nini
Aisee.....kama mimi licha ya kujaza form ya maombi na kufika ofisi zao za Kibo Complex mara kadhaa majibu niliyokutana nayo yanasikitisha na watu kila iitwayo siku wanatoka makwao wanaenda kazini eti naambiwa nisubiri miezi 3 vifaa vichache kweli kama sio uzwazwa ni nini hiki? Kwanza picha linaanza hata hiyo survey hawajanifanyia na mtaani kwangu huduma ya fiber internet ipo Jirani kabsa na marazi yangu hata mita 50 hazifiki . Hili shirika kwa akili za wafanyakazi waliopo haliwezi kenda popote ni wazembe na hawajali kitu customer care mbovu kuliko.
 
Back
Top Bottom