Swali gumu mkuu, ila Kwa Tanzania hakuna Anaemfikia TTCL sababu yeye ndio amepewa Mamlaka na Serikali na makampuni mengi yananunua kwake. Ana uwezo wa kukupa speed hata ya mamia ya GB kwa sekunde.
Wengine Simbanet wapo vizuri hasa kwenye Maofisi, wanatoa Dedicated internet na pia wana intranet incase ofisi zako zipo mahala tofauti tofauti Tanzania.
Raha (liquid) wapo wapo vizuri hasa kama shughuli zako zipo ndani ya Africa jamaa wamejitahidi kusambaza waya maeneo mengi.
Mwisho Zuku kwa Mteja wa kawaida wapo vizuri na customer care yao na offer zao ni nzuri.
Kwa uzoefu wangu mkuu nimetumia Fiber zote hizo kasoro TTCL tu, Fiber Tanzania bado hazijajaa na wateja ni wachache, hivyo yoyote utakayotumia itakupa speed ya maana, mfano hao zuku ukilipa vizuri wana double speed. Hii inaonesha capacity yao haijajaa kabisa.
Hivyo kwa sasa angalia tu mtaa wako fiber gani ipo chukua, ni tech ya kisasa tofauti Na mitandao ya simu ama adsl, haina mambo ya kudrop speed sana.