Mrejesho kwa changamoto yangu... Leo imeishia wiki ya 3 sasa Vodacom Supakasi ndo wameniletea Router yao.
Kwanza kabisa nililipia 5g kwa shilingi 240,000/= badala yake kufungua mzigo kumbe wameniletea wa 4g (nimeshapeleka malalamiko sijui itachukua siku ngapi kunijibu kama tu kuleta huduma wame delay siku 18)
Hawa wajinga nime wa-mind sana afu hata iyo 4g yao ipo slow inapanda na kushuka kwanye ku download ipo around 2MB to 5KB per second na sometimes hakuna network kabisa. Speed ni nzuri ila kwa kazi niliotaka kufanyia kama mteja nilietegemea walau 10Mb/s au 5Mb/s wameniangusha sana.
Nilicho jifunza kuusu delay ni hawa ma agent sio waaminifu nilichogundua wanasubilisha order yako ili tu wafanye timing ya kamishen yao hawana lolote wanasingizia vifaa havipo kama vile wao ni tanesco wakati watu tunatoa hera nyingi. Kwa ufupi huduma ya Vodacom supakasi ni ovyo tofauti na hera unayolipia [emoji2961][emoji2961][emoji2961]