TTCL ina deni la bilioni 403 ilhali mtaji bilioni 243

TTCL ina deni la bilioni 403 ilhali mtaji bilioni 243

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imesema Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limelemewa na deni la Sh403 bilioni ilhali mtaji ilionao ni wa Sh243.

Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Japhet Hasunga amesema hayo jana Jumatano Oktoba 20, 2021 baada ya kuipitia ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2019/20 ambapo amesema wamebaini kuna viashiria katika Shirika hilo kutofanya vizuri kwakuwa lina mtaji hasi wa Sh132 bilioni na madeni makubwa kuliko mtaji wake.

“Hicho ni kiashiria kuwa bado shirika haliendi vizuri. Shirika letu linalipa hadi kodi lakini mapato yao hayajaingizwa katika vitabu vyao,” amesema Hasunga.

=====

Pamoja na nia njema ya JPM, mashirika ya umma yamekuwa yanakula pato la Taifa bila kuleta tija. Tubaki na Tanesco yenye maslahi mapana ya Taifa, haya mengine tukihitaji uzalendo tuwape wafanyabiashara wazawa wajaribu bahati yao.

TTCL ndio ina mkongo wa Taifa wa Data, pamoja na advantage hiyo kibiashara wameshindwa kabisa kutawala soko la internet, yaani mwingine ananunua kutoka kwao halafu anawagaragaza sokoni, tumeshindwa.
Kwanza huku niliko ttcl naisikia kwa majirani
 
Bwana yule ameiingiza hii nchi hasara kubwa

Hivi wale waliopokonywa koroshow zao tayari washalipwa ama bado uhakiki wa mashamba unaendelea kule kaburini Chato
Nyie watu hata mkipigwa sababu mmefeli kuwahudumia waume zenu vizuri mtasingizia bawana yule.
 
Just like ATCL another loss making government run corporation. Annual loss 73 billions and total debt 429 billions.

Kwa Service Ipi waliyokuwa wanatoa....

Yaani Expensively Run and Underperforming....
 
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imesema Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limelemewa na deni la Sh403 bilioni ilhali mtaji ilionao ni wa Sh243.

Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Japhet Hasunga amesema hayo jana Jumatano Oktoba 20, 2021 baada ya kuipitia ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2019/20 ambapo amesema wamebaini kuna viashiria katika Shirika hilo kutofanya vizuri kwakuwa lina mtaji hasi wa Sh132 bilioni na madeni makubwa kuliko mtaji wake.

“Hicho ni kiashiria kuwa bado shirika haliendi vizuri. Shirika letu linalipa hadi kodi lakini mapato yao hayajaingizwa katika vitabu vyao,” amesema Hasunga.

=====

Pamoja na nia njema ya JPM, mashirika ya umma yamekuwa yanakula pato la Taifa bila kuleta tija. Tubaki na Tanesco yenye maslahi mapana ya Taifa, haya mengine tukihitaji uzalendo tuwape wafanyabiashara wazawa wajaribu bahati yao.

TTCL ndio ina mkongo wa Taifa wa Data, pamoja na advantage hiyo kibiashara wameshindwa kabisa kutawala soko la internet, yaani mwingine ananunua kutoka kwao halafu anawagaragaza sokoni, tumeshindwa.
Wameanza tena wezi hawa wa umma. Mwanzo mlijaribu kuuza ikaishia kuitia serikali hasara kubwa na kuporwa kampuni yake ya celltel. Ttcl ni sawa idara ya serikali. Kinachotakiwa ni kudhibiti ubadhilifu na kuweka watu weledi na wenye uzalendo. Tunajua nini kinaendelea baada ya kupita utawala wa magufuli. Tuko chonjo kuzuia fisadi.
 
Bwana yule ameiingiza hii nchi hasara kubwa

Hivi wale waliopokonywa koroshow zao tayari washalipwa ama bado uhakiki wa mashamba unaendelea kule kaburini Chato
Mpaka wa leo tani 4.8 nimelizwa
 
..Deni hili limetoka wapi wakati ktk awamu ya 5 TTCL walikuwa wanatoa gawio kwa serikali?

Haya mashirika ya serikali shida yake kubwa ni wafanyakazi, wamekaa kipigaji pigaji, hawajali, hawajibiki, hawana ubunifu wala hawana uchungu na mali uma...Una mpa mfanyakazi ajira ya kudumu unategemea nn?ana uhakika wa ajira till death do him/her apart...siku akitokea kichaa akabadili utaratibu wa ajira serikalini ukawa wa mikataba na KPI then kutakua na mabadiliko makubwa sana.
TTCL pale wamejaa wazee wanakwenda mwendo wa kinyonga, na ht vijana wakiajiriwa miezi michache nao wanazeeka.
Fukuza wafanyakazi wote tuanze upyaa na mikataba ya muda mfupi.
 
Shirika kuwa madeni kuliko mtaji SiO ajabu na SiO kwamba inaashiria shirika linaelekea kufa.
Biashara inaendeshwa na either mtaji or debts au vyote. Ukienda kwenye makampuni ya madini, Karibia yote yanaendeshwa na madeni. Cha msingi ni je TTcl Ina madeni ambayo imeshindwa kuyalipa? Kama jibu ni ndio, hicho ndio kiashiria namba moja kwamba going concern yake inatia shaka.
 
Si walikuwa wanatoa gawio kwa serikali kuwa wanapata faidi au siyo TTCL hii? Wajinga sana acha life
 
Heheh,

Hivi hawa si ndio walikuwa wanatoa gawio la faida kwa serikali...

Ama kweli mbio za sakafuni huishia ukingoni...
 
Back
Top Bottom