Mmawia
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 122,494
- 96,074
Tuliwahi kuambiwa kuwa ATCL imeshaanza kupata faida mara baada ya kupata ndege mpya .Hii Nchi inaendeshwa kitapeli,tokea ile awamu ya Chizi.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tuliwahi kuambiwa kuwa ATCL imeshaanza kupata faida mara baada ya kupata ndege mpya .Hii Nchi inaendeshwa kitapeli,tokea ile awamu ya Chizi.
TTCL Customer Care Mkuje kutueleza
Hizi sarakasi ni kwenye mfumo mzima ndiyo maana hawachukuliwi hatua yoyote na wenye mamlaka.Yule DG wao na bodi yao wanatakiwa kujitathmini
Hata kwa nyundo siendiLudi nyumbani kumenoga
Siasa illichanganywa kwenye kila kitu
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imesema Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limelemewa na deni la Sh403 bilioni ilhali mtaji ilionao ni wa Sh243.
Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Japhet Hasunga amesema hayo jana Jumatano Oktoba 20, 2021 baada ya kuipitia ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2019/20 ambapo amesema wamebaini kuna viashiria katika Shirika hilo kutofanya vizuri kwakuwa lina mtaji hasi wa Sh132 bilioni na madeni makubwa kuliko mtaji wake.
“Hicho ni kiashiria kuwa bado shirika haliendi vizuri. Shirika letu linalipa hadi kodi lakini mapato yao hayajaingizwa katika vitabu vyao,” amesema Hasunga.
=====
Pamoja na nia njema ya JPM, mashirika ya umma yamekuwa yanakula pato la Taifa bila kuleta tija. Tubaki na Tanesco yenye maslahi mapana ya Taifa, haya mengine tukihitaji uzalendo tuwape wafanyabiashara wazawa wajaribu bahati yao.
TTCL ndio ina mkongo wa Taifa wa Data, pamoja na advantage hiyo kibiashara wameshindwa kabisa kutawala soko la internet, yaani mwingine ananunua kutoka kwao halafu anawagaragaza sokoni, tumeshindwa.
Shirika linaendeshwa kihasara kwa maslahi ya Mani haswa
Limeshafufuka?jamaa yule yupo smart sana hata ukimsikiliza ana utofauti na ma CEO wengi wa serikali, ni yeye ndiye amefufua hilo shirika,tatizo ni wanasiasa ndio wanaliua
Sasa gawio walikuwa wanatoaje ilinihali wana deni kubwa ivo. Wajuvi wa mambo mtueleze basi
Simlisema rudini nyumnani kumenoga? hii nchi miyayusho sana , mtandao ukivuka maji kwenda kigamboni haupatikani unategemea kupata faida? masiasa kibaao ni kama ATCL tu hakuna kitu, mnadai mnaupiga mwingi
Just like ATCL another loss making government run corporation. Annual loss 73 billions and total debt 429 billions.
Hii nchi ina matatizo mengi aisee hadi unachoka kabisa. Jana nasikia tena Mfumo wa jamii unaidai serikali yetu 4.8 Trillion..aisee
Heheh,
Hivi hawa si ndio walikuwa wanatoa gawio la faida kwa serikali...
Ama kweli mbio za sakafuni huishia ukingoni...
Tulipokuwa tunasema serikali ya Magufuli ilikuwa inaendeshwa kwa kupika data, wapambe wake walikua wanateka watu wanaosema ukweli. Wajinga walipokuwa wanaona yale maigizo, walikuwa wanasema tuna bonge la rais maana mashirika ya umma yamefufuka. Ile sheria ya takwimu kuwa ni lazima uzipate serikalini, lengo lake ilikuwa ni kuzuia watu kujua ukweli ili watawaliwe kama makondoo.
Mifuko ya jamii inadai zaidi ya shilingi 4.t+, na hizo pesa zote zimechotwa kihuni ili kwenda kwenye white elephant projects ili kusaka political millage. Nenda sasa kaangalie wakuu wa hayo mashirika walivyo na mapato makubwa, huwa wanufaika wakipata tabu za ajabu kwenye madai yao .