TTCL ina deni la bilioni 403 ilhali mtaji bilioni 243

TTCL ina deni la bilioni 403 ilhali mtaji bilioni 243

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imesema Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limelemewa na deni la Sh403 bilioni ilhali mtaji ilionao ni wa Sh243.

Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Japhet Hasunga amesema hayo jana Jumatano Oktoba 20, 2021 baada ya kuipitia ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2019/20 ambapo amesema wamebaini kuna viashiria katika Shirika hilo kutofanya vizuri kwakuwa lina mtaji hasi wa Sh132 bilioni na madeni makubwa kuliko mtaji wake.

“Hicho ni kiashiria kuwa bado shirika haliendi vizuri. Shirika letu linalipa hadi kodi lakini mapato yao hayajaingizwa katika vitabu vyao,” amesema Hasunga.

=====

Pamoja na nia njema ya JPM, mashirika ya umma yamekuwa yanakula pato la Taifa bila kuleta tija. Tubaki na Tanesco yenye maslahi mapana ya Taifa, haya mengine tukihitaji uzalendo tuwape wafanyabiashara wazawa wajaribu bahati yao.

TTCL ndio ina mkongo wa Taifa wa Data, pamoja na advantage hiyo kibiashara wameshindwa kabisa kutawala soko la internet, yaani mwingine ananunua kutoka kwao halafu anawagaragaza sokoni, tumeshindwa.

TTCL hawauzi data kwa faida wakiamua kufanya biashara bando la internet utakua unapita ukiangalia
 
Simlisema rudini nyumnani kumenoga? hii nchi miyayusho sana , mtandao ukivuka maji kwenda kigamboni haupatikani unategemea kupata faida? masiasa kibaao ni kama ATCL tu hakuna kitu, mnadai mnaupiga mwingi
 
Mazingaombwe ya CCM hayo. Nakumbuka enzi za Magufuli hili ndo shirika la umma lililokuwa linapigiwa mfano kwa kujiendesha kwa faida na kuongoza ktk kutoa gawio. Sasa kiko wapi? Hayo mazingaombwe ya umaarufu wa kisiasa yalikuwa ysnafanyika kwa faida ya nani?
 
Simlisema rudini nyumnani kumenoga? hii nchi miyayusho sana , mtandao ukivuka maji kwenda kigamboni haupatikani unategemea kupata faida? masiasa kibaao ni kama ATCL tu hakuna kitu, mnadai mnaupiga mwingi

wakianza kupata faida we data hutaweza kununua
 
Hii nchi ina matatizo mengi aisee hadi unachoka kabisa. Jana nasikia tena Mfumo wa jamii unaidai serikali yetu 4.8 Trillion..aisee
 
Just like ATCL another loss making government run corporation. Annual loss 73 billions and total debt 429 billions.

hakuna shirika la serikali linapata loss inclusive, report za siasa ni tafauti na uhalisia wa uchumi wa mashirika ya serikali, ni kama useme zile hospitali za vijijini wananachi wanaojifungua bure ukaandike loss report
 
Hii nchi ina matatizo mengi aisee hadi unachoka kabisa. Jana nasikia tena Mfumo wa jamii unaidai serikali yetu 4.8 Trillion..aisee

subiri samia akimaliza upokee ripoti ingine
 
Heheh,

Hivi hawa si ndio walikuwa wanatoa gawio la faida kwa serikali...

Ama kweli mbio za sakafuni huishia ukingoni...

na ela walitoa wap ya kutoa gawio ilihali wanapata hasara na wafanya kazi wakalipwa na bado shirika liliweza kununua hisa zote zilizokua znamilikiwa na china zirudi tanzania, na mpaka leo bado inadunda
 
Tulipokuwa tunasema serikali ya Magufuli ilikuwa inaendeshwa kwa kupika data, wapambe wake walikua wanateka watu wanaosema ukweli. Wajinga walipokuwa wanaona yale maigizo, walikuwa wanasema tuna bonge la rais maana mashirika ya umma yamefufuka. Ile sheria ya takwimu kuwa ni lazima uzipate serikalini, lengo lake ilikuwa ni kuzuia watu kujua ukweli ili watawaliwe kama makondoo.

Mifuko ya jamii inadai zaidi ya shilingi 4.t+, na hizo pesa zote zimechotwa kihuni ili kwenda kwenye white elephant projects ili kusaka political millage. Nenda sasa kaangalie wakuu wa hayo mashirika walivyo na mapato makubwa, huwa wanufaika wakipata tabu za ajabu kwenye madai yao .

samia akimaliza mda wake subiria ripoti ingine
 
Back
Top Bottom