Tuacha upotoshaji wa kudhani kuteseka sana mwishowe huwa ni kufanikiwa, watu wengi huteseka mpaka kifo bila kufanikiwa.

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Utaskia..

"Diamond aliteseka sana leo kafanikiwa" - hapa mtu anasahau kwamba kwenye muziki kuna ma elfu ya wasanii wameanza kuimba 2005 huko ila mpaka leo bado wanteseka.

"Bakhresa alianzia chini kwa kujiajiri leo katoboa" - katika kundi hili kuna watu wengi sanaaa waliojiajiri kila siku alfajiri mpaka usiku hata iwe sikukuu wapo wana haso ila bado wanateseka, wanatamani waajiriwe serikalini wapate hata laki 5 kila mwezi na waweze kupumzika weekend.

"Samata aliteseka sana ila leo yupo ulaya" hapa kuna vijana wanacheza vizuri sana lakini mpaka leo hata timu za ligi ya daraja la pili wanazisikia bmbani.

Nadhani tuache kufanya maamuzi ama kujihakikishia kitu flani kupitia watu wachache sana walioweza kufanikiwa, huwa kuna lundo kubwa sana la watu ambao bado wanateseka katika kundii flani ila watu humtazama mtu moja au wahache waiofanikiwa katika hilo kundi.

JIAMINI WEWE MWENYEWE UNAWEZA, USIANZE KUFIKIRIA WATU WALIOFANIKIWA ILI KUFANYA KITU

Jiamini wewe unaweza kufanya unachotaka, usifanye maamuzi asilimia yote mpaka uone kuna flani kafika mbali,

Diamond angewaza kwamba aimbe kwasababu tu ya kufikia levo za wasanii wa enzi hizo, sidhani kama angenunua gari yake ya bilioni 1, kujenga mjengo wake madale, kuwa ceo wa wasafi, kuwa na levo yake , n.k
 
Sasa tufanyaje....

Hivyo tu basi
 
Labda hii

20220416_232716.jpg
 
Back
Top Bottom