Tuachane na matokeo, Camera za CAF Champions League mbona ni mbovu kiasi hiki?

Mbona mechi kibao za Ligi zinachezwa mchana na muonekano hauwi vile

Kingine mpira wa jana wa Yanga ulichezwa saa 11 jioni saaa za Tunisia na kulikuwa hakuna jua kiwanjani lakini picha zilikuwa mbovu hadi kuna saa mpira wa kuchezea hauonekani
 
Kibanda nilichoangalizia game jana kuna mtu alisema kuhusu ubovu wa picha ila mimi sikuuona kwa kweli. Niliona ni kawaida tu. Basi tuseme operators wa cameras ndiyo hawakuwa makini.
 
Kibanda nilichoangalizia game jana kuna mtu alisema kuhusu ubovu wa picha ila mimi sikuuona kwa kweli. Niliona ni kawaida tu. Basi tuseme operators wa cameras ndiyo hawakuwa makini.
Ukitaka kujua ubovu wake, cheki mechi za EPL au UEFA kisha ulinganishe na za CAF
 
Ukitaka kujua ubovu wake, cheki mechi za EPL au UEFA kisha ulinganishe na za CAF
Nilitaka kusema katika post yangu iliyopita, kama vigezo mnavyotumia ni hivyo vya UEFA mnakosea. Hii Africa bro, unadhani Guinea huko kwenye media zao wana investment kama za EPL au hata AZAM? Uliona hata vyumba vya kubadilishia viko upande wa pili wa uwanja, half time na baada ya game, ilibidi wachezaji wa akiba na benchi la ufundi wacross uwanja. Sijui waliweka mabechi vile kuepuka jua au sababu nyingine.

Hata hapa viwanja vingapi mechi za usiku mwanga hafifu tunalazimisha tu kucheza usiku.
 
Kwani CAF wanapiga picha?
 
Sasa wewe ulisema hukuona shida yoyote kwenye quality ya video, ndio nikaukuambia ili kuona utofauti wa quality kajaribu kuangalia hiyo mifano niliyokupa

Halafu ishu hata wala sio nchi, maana hata ya Tunisia ilikua quality ileile

wanaohusika na hayo matangazo ni CAF wenyewe, ndio wanaompa kampuni tenda ya kurusha mechi zote kama TFF walivyompa AZAM,
Ishu ni CAF kuwapa vigezo hao warushaji wawe wanarusha picha za quality fulani, maana haya ni mashindano makubwa
 
Quality ilikuwa sawa tu mbona.

Punguza kuishi kwa mazoea
 
Dstv wao ilikuwa yaonesha vizuri tofauti na Azam ilionesha kupauka.

Nilikuwepo Kibanda umiza wakaweka zote 2 baada ya mechi ya Arsenal
 
Kwa upande wangu mechi ilikuwa inaangalika bila shida ila ukianza kulinganisha ndiyo hapo utapata shida. Inawezekana kibanda nilichoangalizia game ya jana wanatumia DSTV kama alivyosema mdau hapo juu. Game ya Simba niliangalizia AZAM nilichoona tu mwanga ulikuwa mkali ndiyo maana nikasema jua limechangia lakini pia operators labda hawakuwa wazoefu kuset vifaa kwa quality sahihi.
 
unawachkuliaje azam kwa mfano,wabongo tunapenda sana kujidharau.hivi unajua camera wanazotumia azam cost yake per camera,..sasa nikuambie africa nzima hakuna production team ina camera bora zaidi ya za azam
 
Sasa wapi nimeidharau Azam?
 
Kuna jamaa hapo juu mbishi sana sisi watu wa camera licha ya kutizama mpira lakini kwakua camera ndio fani yetu ikitokea changamoto lazima tufanye udadisi wa vitu vidogo vidogo. Wakati wa mechi ya yanga kunamuda camera zilikua zinaonekana kabisa na aina ya camera zile ni NX 100 kwa wale wahudhuriaji wa masherehe utakua unaelewa zile camera zinazotumika kushutia harusi ndizo zilikua zikitumika.

Camera zile hazitoi Quality ya HD yani ukishoot wide angle uwanjani wachezaji hutowatambua sura maana yenyewe itachukua movement tu za wachezaji.

Camera zinazotumiwa na Azam zinaitwa SONY UHD (ULTRA HIGH DEFINITION) ambazo ndizo zinazotumika na DSTV na hata EPL wanatumia hizohizo.
 
Sasa wapi nimeidharau Azam?
lens tu moja ya ile camera ina kariba mil.500 ivi,azam kawekeza sana tumheshimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…