Kuna jamaa hapo juu mbishi sana sisi watu wa camera licha ya kutizama mpira lakini kwakua camera ndio fani yetu ikitokea changamoto lazima tufanye udadisi wa vitu vidogo vidogo. Wakati wa mechi ya yanga kunamuda camera zilikua zinaonekana kabisa na aina ya camera zile ni NX 100 kwa wale wahudhuriaji wa masherehe utakua unaelewa zile camera zinazotumika kushutia harusi ndizo zilikua zikitumika.
Camera zile hazitoi Quality ya HD yani ukishoot wide angle uwanjani wachezaji hutowatambua sura maana yenyewe itachukua movement tu za wachezaji.
Camera zinazotumiwa na Azam zinaitwa SONY UHD (ULTRA HIGH DEFINITION) ambazo ndizo zinazotumika na DSTV na hata EPL wanatumia hizohizo.