Tuache kudanganyana, Ajira zina afadhali zaidi kuliko kujiajiri, watu wengi waliojiajiri ndio wapo kwenye utumwa

Kila kitu ni mentality na aina ya kazi uliyo jiajiri nayo.
Amna raha kama kazi ya kujiajiri kikubwa tu upende hiyo kazi.....
Uweze kuifanya vizuri hiyo kazi ikue.....
Uwe na time table nzuri ya kazi na mpangilio wa muda kwenye kazi yako.
Hakika ukizingatia huwezi kuwa mtumwa na pesa lazima upate.
 
Jamaa yangu mmoja alipata mtaji na mafanikio ya biashara akiwa muajiliwa akaona muajiliwa kuna mnyima mda wa kufanya mambo yake, akaacha kazi akaenda jiajiri rasmi bwana wee

Uko akakutana na misingi ya kujiajiri, kusanya sana tumia kidogo, fitna, ushirikina, ujanja, jamaa akapambana navyo at the end kabaki jina tu kashindwa mapambano ya mtani

MY TAKE
Ukiwa umeajiriwa na umejiajiri heshimu sana ajira yako kwani mafanikio ya kujiajiri kwako yanabustiwa na ajira yako
 
Shida ya kuajiriwa Kwanza unapoteza mda wako mwingi kumtumikia mtu na wengi tunawaona mtaani wakishaacha kazi wanakuwa Wana maisha magumu Sana na hata wakipewa pensheni hazikai mwisho wa siku anakuwa omba omba maisha halisia ni kujiajiri na unakutana na changamoto nyingi za maisha na mwisho wa siku unazizoea

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Hili lina ukwel kabisaaa..nimeingia kwenye mapambano ya kujiajiri..aisee ni frustrations za kufa mtuuu...ila siachi..i believe this is a real experience of life...
 
Ndio advantage ya biashara ulipo...ikisha kaa stable una enjoy ila before hapo unahenyeka na kumenyeka mpaka unatamani kukufuru
 
Mawazo ya kufilisika
 
Kama kujiajri kwenyewe ndio huku kwa kuendesha boda boda,kibanda Cha mpesa,duka la reja reja,ufugaji wa kuku,kuendesha Tex,kuuza genge,
Huko kote ni stress sana,
Kujiajiri kwenye nafuu ni kwa wale wanaomiriki makampuni,Tena wameajiri watu kadhaa,hata akilala nyumbani,pesa inaingia,hiyo ni level nyingine,lakini una duka la tv,na cm kariakoo,useme hiyo ajira inakupa ahueni,aaah wapi.
Hizi ajira zetu za kujiajiri ni low key,kule Kenya zinaitwa "side hustle"zinakusaidia vijipesa tu,
Ila hako ka side hustle ukikalea kakakua,unaweza ukafika hatua,unalala mambo yanaenda unakuwa umewaweka wakulungwa wengine wakufanyie kazi
 
Wa hivi ni wachache Bwashee usijitoe ufahanu, majority are toiling
 
.
 
Acha uongo salary ya 700k Kwa mtu mwenye nidhamu ya pesa anasevu 200k-300k na sio pungufu ya hapo..

Kumbuka Kuna watu wanaishi Kwa salary za 300-400 na wanakomaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…