Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 7,899
- 10,415
- Thread starter
-
- #81
ThanksPamoja na maelezo yako mazuri huko nyuma, hapa naongeza yafuatayo;
Kiasili gesi asilia Ina pressure kutoka ardhini (visima vina msukumo wa kutosha). Compressor hutumika tu pale ambapo gesi imepungua (kuelekea kuisha) na hivyo pressure iliyokusudiwa kuendesha mitambo kutoka kwenye kisima kutofikiwa.
Gesi asilia huundwa baada ya matabaka ya masalia ya viumbe wadogo wa baharini kuvunjwavunjwa kikemikali pasipo uwepo wa hewa ya okjeni kutokana na kugandamizwa zaidi ya miaka millioni katika mazingira ya joto na pressure chini ya ardhi. Ile nishati ambayo viumbe hao hasa mimea ya majini huipata kutoka kwenye jua kupitia photosinithesis huhifadhiwa kama nishati ya kikemkali kwenye molekyuli ya methane na kampaundi zingine za kihaidrokaboni.Kwani hiyo gesi asilia inatokana na Nini?
Haiwezekani kuiunda maabara.??
Shukrani kwa ufafanuzi.Hiyo gesi inayotumika kufua umeme Kinyerezi Dar es Salaam ni gesi asilia pia inayozalishwa katika vitalu vya Songo Songo na Mnazi Bay.
Kitalu cha Mnazi Bay kinasimamiwa na kampuni inaitwa PanAfrican Energy Tanzania Ltd lakini pana ubia makampuni mengine.
Na kitalu cha Mnazi Bay kinamilikiwa na Maurel & Prom (hisa 48.06%), TPDC (hisa 20%) na Wentworth Resources PLC (hisa 31.94%). Hivi vitalu viwili viligunduliwa zamani kidogo na gesi yake inapatikana kwenye maji ya kina kifupi na nyingine nchi kavu kabisa.
Lakini gesi inayozungumziwa kuwa itabadilisha uchumi wa Tanzania ni ile iliyogunduliwa kwenye maji ya kina kirefu katika kitalu cha Block 2 Offshore Field. Hiyo ndio gesi nyingi ambayo haiwezi kuzalishwa bila uwepo wa kiwanda cha kuibadilisha hiyo gesi nyingi kuwa kimiminika (LNG) ili isafirishwe kuuzwa nje ya nchi.
karibuShukrani kwa ufafanuzi.
Kwani ni uongo kwamba visima vya gesi vimeuzwa Enzi zake?Usiwaseme viongozi kwa mambo usiyoyajua rafiki. Ni vyema tujikite kuelimishana tu na sio kusambaza taarifa tusizo zijua.
Kama ni uongo waweke wazi mikataba waliyoingia na wawekezaji kwenye secta ya gesi.Usiwaseme viongozi kwa mambo usiyoyajua rafiki. Ni vyema tujikite kuelimishana tu na sio kusambaza taarifa tusizo zijua.
Kama ni ukweli wewe tuwekee huo mkataba ili tuthibitishe hayo madai yakoKama ni uongo waweke wazi mikataba waliyoingia na wawekezaji kwenye secta ya gesi.
Una ufahamu mdogo sana wa masuala ya gesi ila ni kwa vile unaowaelekeza hawana kabisa , jifunze kwanza uongeze maarifa Google haitoshi pekee mtafute expert wakeInaitwa gesi asilia (Natural Gas).
Mtwara tuna aina moja ya gesi asilia yenye kiwango kikubwa cha kampaundi ya methane. LNG sio aina ya gesi. Kwanza tambua kwamba LNG kirefu chake ni Liquefied Natural Gas (Gesi asilia iliyo badilishwa kuwa kimiminika).
Tambua kwamba ni gesi iliyobadilishwa kuwa kimiminika ili iwe rahisi kuifadhi na kuisafirisha kwa wingi katika umbali mrefu sana sana nje ya nchi. Ukiibadilisha gesi kuwa kimiminika ndipo unaweza kuisafirisha kwa wingi zaidi. Kipimo kimoja cha gesi asilia kinakua mara 600 ikiwa katika hali ya kimiminika.
Bado LNG haijaanza kuzalishwa Mtwara. Ili kuizalisha LNG kinatakiwa kijengwe kiwanda kinacho gharimu Trillion 70 Tsh.
Hivyo kazi kubwa ya kiwanda hicho itakua ni kuibadilisha gesi asilia kuwa LNG.
CNG kirefu chake ni compressed natural gas yaani gesi asilia iliyo kandamizwa au shindiliwa. Nayo bado ni gesi asilia ila yenyewe imeshindiliwa kwa kutumia mashine ili itumike kwenye magari.
LNG na CNG zote ni gesi asilia na zote zina kampaundi ya methane. Isipokua LNG ipo katika katika mfumo wa kimiminika na CNG katika muundo wa kukandamizwa. Lengo kuu ni kuweza kuifadhi na kusafirisha.
Boss kama unaufahamu mzuri zaidi kwenye masuala ya gesi tunakuomba uandike chochote hapahapa kweni uzi ili tupate knowledge zaidi. Karibu boss.Una ufahamu mdogo sana wa masuala ya gesi ila ni kwa vile unaowaelekeza hawana kabisa , jifunze kwanza uongeze maarifa Google haitoshi pekee mtafute expert wake
ThanksAngalau nimepata cha maana cha kuwaelekeza wezangu kupitia wewe.
Hatutaki wahuni kama wewe kwenye mada hii. Ungekuwa wa maana ungeongezea kinachopungua. Duniani ufahamu kuhusu kitu haujawahi kwisha, bali watu huendelea kushirikishana ili kupata ufahamu ulio mpana zaidi. Kudos kwa mleta mada.Una ufahamu mdogo sana wa masuala ya gesi ila ni kwa vile unaowaelekeza hawana kabisa , jifunze kwanza uongeze maarifa Google haitoshi pekee mtafute expert wake
Kwanini wafiche hizo mikataba?kwanini wasituoneshe watanzania?ujue Tu tushaliwa wawekezaji wanamikili hiyo gesi Kwa asilimia 100Kama ni ukweli wewe tuwekee huo mkataba ili tuthibitishe hayo madai yako
Bora Meneja wa Makampuni anayetushirikisha huo unaouita "ufahamu mdogo", kuliko wewe mwenye ufahamu mkubwa unaobaki nao peke yako.Una ufahamu mdogo sana wa masuala ya gesi ila ni kwa vile unaowaelekeza hawana kabisa , jifunze kwanza uongeze maarifa Google haitoshi pekee mtafute expert wake
Boss najua unaufahamu mzuri zaidi kwenye masuala ya gesi asilia tunakuomba uandike chochote hapahapa kweni uzi ili tupate knowledge zaidi. Karibu boss.Una ufahamu mdogo sana, na pia kwenye Uzi huu unadhihirisha watu wengi walivyo na ufahamu mdogo sana pia.
Na hawa ndio watu kutwa kutukana serikali na viongozi ikjwa mambo madogo Kama haya hawalewi kabisa.
Nchi hii aisee
Hii nayo ni Hadithi yakuaminiwa nawagonjwa hakiri.Kwa hiyo Kikwete ameshauza maeneo au visima vyenye gesi na inasemekana pia Katoa mengine kwa wachina ili amuokoe kijana wake alipokamatwa na madawa ya kulevya.
Sijui hata nianzie wapi kwa aina hii ya ufahamu ulionao na hao wengine pia.Boss najua unaufahamu mzuri zaidi kwenye masuala ya gesi asilia tunakuomba uandike chochote hapahapa kweni uzi ili tupate knowledge zaidi. Karibu boss.