Tuache kudanganyana hakuna gesi iliyowahi kuuzwa na kusafirishwa kwa bomba kwenda nje ya Tanzania

Tuache kudanganyana hakuna gesi iliyowahi kuuzwa na kusafirishwa kwa bomba kwenda nje ya Tanzania

Pamoja na maelezo yako mazuri huko nyuma, hapa naongeza yafuatayo;
Kiasili gesi asilia Ina pressure kutoka ardhini (visima vina msukumo wa kutosha). Compressor hutumika tu pale ambapo gesi imepungua (kuelekea kuisha) na hivyo pressure iliyokusudiwa kuendesha mitambo kutoka kwenye kisima kutofikiwa.
Thanks
 
Kwani hiyo gesi asilia inatokana na Nini?

Haiwezekani kuiunda maabara.??
Gesi asilia huundwa baada ya matabaka ya masalia ya viumbe wadogo wa baharini kuvunjwavunjwa kikemikali pasipo uwepo wa hewa ya okjeni kutokana na kugandamizwa zaidi ya miaka millioni katika mazingira ya joto na pressure chini ya ardhi. Ile nishati ambayo viumbe hao hasa mimea ya majini huipata kutoka kwenye jua kupitia photosinithesis huhifadhiwa kama nishati ya kikemkali kwenye molekyuli ya methane na kampaundi zingine za kihaidrokaboni.

Kuiunda gesi maabara inawezekana, unaweza kutumia masalia ya mimea au vinyesi vya wanyama ukazalisha Bayogesi maabara. Kampaundi inayounda Bayogesi ndio ile iliyopo kwenye gesi asilia.

Lakini pia unaweza kutumia makaa ya mawe kuzalisha hiyo gesi maabara. Japo utahitaji kutumia gharama kidogo.
 
Hiyo gesi inayotumika kufua umeme Kinyerezi Dar es Salaam ni gesi asilia pia inayozalishwa katika vitalu vya Songo Songo na Mnazi Bay.

Kitalu cha Mnazi Bay kinasimamiwa na kampuni inaitwa PanAfrican Energy Tanzania Ltd lakini pana ubia makampuni mengine.

Na kitalu cha Mnazi Bay kinamilikiwa na Maurel & Prom (hisa 48.06%), TPDC (hisa 20%) na Wentworth Resources PLC (hisa 31.94%). Hivi vitalu viwili viligunduliwa zamani kidogo na gesi yake inapatikana kwenye maji ya kina kifupi na nyingine nchi kavu kabisa.

Lakini gesi inayozungumziwa kuwa itabadilisha uchumi wa Tanzania ni ile iliyogunduliwa kwenye maji ya kina kirefu katika kitalu cha Block 2 Offshore Field. Hiyo ndio gesi nyingi ambayo haiwezi kuzalishwa bila uwepo wa kiwanda cha kuibadilisha hiyo gesi nyingi kuwa kimiminika (LNG) ili isafirishwe kuuzwa nje ya nchi.
Shukrani kwa ufafanuzi.
 
Inaitwa gesi asilia (Natural Gas).

Mtwara tuna aina moja ya gesi asilia yenye kiwango kikubwa cha kampaundi ya methane. LNG sio aina ya gesi. Kwanza tambua kwamba LNG kirefu chake ni Liquefied Natural Gas (Gesi asilia iliyo badilishwa kuwa kimiminika).

Tambua kwamba ni gesi iliyobadilishwa kuwa kimiminika ili iwe rahisi kuifadhi na kuisafirisha kwa wingi katika umbali mrefu sana sana nje ya nchi. Ukiibadilisha gesi kuwa kimiminika ndipo unaweza kuisafirisha kwa wingi zaidi. Kipimo kimoja cha gesi asilia kinakua mara 600 ikiwa katika hali ya kimiminika.

Bado LNG haijaanza kuzalishwa Mtwara. Ili kuizalisha LNG kinatakiwa kijengwe kiwanda kinacho gharimu Trillion 70 Tsh.

Hivyo kazi kubwa ya kiwanda hicho itakua ni kuibadilisha gesi asilia kuwa LNG.

CNG kirefu chake ni compressed natural gas yaani gesi asilia iliyo kandamizwa au shindiliwa. Nayo bado ni gesi asilia ila yenyewe imeshindiliwa kwa kutumia mashine ili itumike kwenye magari.

LNG na CNG zote ni gesi asilia na zote zina kampaundi ya methane. Isipokua LNG ipo katika katika mfumo wa kimiminika na CNG katika muundo wa kukandamizwa. Lengo kuu ni kuweza kuifadhi na kusafirisha.
Una ufahamu mdogo sana wa masuala ya gesi ila ni kwa vile unaowaelekeza hawana kabisa , jifunze kwanza uongeze maarifa Google haitoshi pekee mtafute expert wake
 
Una ufahamu mdogo sana wa masuala ya gesi ila ni kwa vile unaowaelekeza hawana kabisa , jifunze kwanza uongeze maarifa Google haitoshi pekee mtafute expert wake
Boss kama unaufahamu mzuri zaidi kwenye masuala ya gesi tunakuomba uandike chochote hapahapa kweni uzi ili tupate knowledge zaidi. Karibu boss.
 
Una ufahamu mdogo sana wa masuala ya gesi ila ni kwa vile unaowaelekeza hawana kabisa , jifunze kwanza uongeze maarifa Google haitoshi pekee mtafute expert wake
Hatutaki wahuni kama wewe kwenye mada hii. Ungekuwa wa maana ungeongezea kinachopungua. Duniani ufahamu kuhusu kitu haujawahi kwisha, bali watu huendelea kushirikishana ili kupata ufahamu ulio mpana zaidi. Kudos kwa mleta mada.
 
Una ufahamu mdogo sana wa masuala ya gesi ila ni kwa vile unaowaelekeza hawana kabisa , jifunze kwanza uongeze maarifa Google haitoshi pekee mtafute expert wake
Bora Meneja wa Makampuni anayetushirikisha huo unaouita "ufahamu mdogo", kuliko wewe mwenye ufahamu mkubwa unaobaki nao peke yako.
 
Ahsante sana kwa shule ya gesi Meneja Wa Makampuni meneja wa makampuni,

Kuna hawa wachina wa Anric gas company CNG hapo awali waliingia mkataba na DIT( Dar Institute of Technology) kutengeneza na kufanya installation ya mifumo ya gesi ya CNG kweny magari, je, serikali haiwezi kutumia makampuni yake kufanya hizo installation na kusaidia kupunguza gharama za maisha kwa wananchi hata kwa magari ya serikali na umma?

Je, ile kampuni ya pan Africa energy pale ubungo maziwa ni ya nani inahusika na kujaza CNG?

Nimeona magari ya Dangote yamefungwa mifumo ya gesi CNG je anapata wapi gesi asilia? Anamiliki mitambo yake mwenyewe?

Kwanini vituo vya gesi ni kimoja tu kipo ubungo tu? Kwanini visiwepo sehemu nyingine mikoani n.k?

Je, miradi mikubwa kama hiyo kwa nini wasipewe taasisi Kama JWTZ kwa mikakati kutokana na credibility ya taasisi zetu?

Ukiacha EWURA na mamlaka zingine, idara yetu ya usalama wa Taifa ( TISS) ina nguvu gani au uelewa gani na mamlaka na uwezo wa kushauri mambo muhimu ya rasilimali Kama gesi? Je, kuna au tuna vijana wangapi mpaka sasa katika Taifa letu waliosoma ndani na nje ya nchi na kubobea kwenye taaluma ya gesi?

Serikali inakwama wapi kubadilisha mifumo yote ya mafuta na kuweka iwe ya gesi mpaka pikipiki Kama gharama za mafuta ni kubwa?

Kwanini gesi isitumike kuzalisha umeme kurahisisha kukua kwa uchumi wa viwanda?

Ahsante sana nitaendelea kuuliza na kijifunza hapa.
 
Una ufahamu mdogo sana, na pia kwenye Uzi huu unadhihirisha watu wengi walivyo na ufahamu mdogo sana pia.

Na hawa ndio watu kutwa kutukana serikali na viongozi ikjwa mambo madogo Kama haya hawalewi kabisa.

Nchi hii aisee
 
Una ufahamu mdogo sana, na pia kwenye Uzi huu unadhihirisha watu wengi walivyo na ufahamu mdogo sana pia.

Na hawa ndio watu kutwa kutukana serikali na viongozi ikjwa mambo madogo Kama haya hawalewi kabisa.

Nchi hii aisee
Boss najua unaufahamu mzuri zaidi kwenye masuala ya gesi asilia tunakuomba uandike chochote hapahapa kweni uzi ili tupate knowledge zaidi. Karibu boss.
 
Kwa hiyo Kikwete ameshauza maeneo au visima vyenye gesi na inasemekana pia Katoa mengine kwa wachina ili amuokoe kijana wake alipokamatwa na madawa ya kulevya.
Hii nayo ni Hadithi yakuaminiwa nawagonjwa hakiri.

Mtoto wa Rais hatama akihusisha na madawa hawezi kua punda.
Kwenye haramu zote matajiri wanakua wamwishi kuhusika.
 
Boss najua unaufahamu mzuri zaidi kwenye masuala ya gesi asilia tunakuomba uandike chochote hapahapa kweni uzi ili tupate knowledge zaidi. Karibu boss.
Sijui hata nianzie wapi kwa aina hii ya ufahamu ulionao na hao wengine pia.

Kuna sehemu hadi nimeona aibu uliposema mradi wa Kinyerezi ni gesi kutoka songosongo na mnazi bay. Hivi hata songosongo unaoajua kweli?
 
Back
Top Bottom