Match fitness inaangaliwa baina ya wachezaji wanaocheza ligi linganifu.Mchezaji anaekaa bench Olympiacos (Greece league hii ni league kubwa nashangaa unaita ka league) ana fitness yakutosha kuliko mchezaji anaecheza mara kwa mara yanga au simba. Narudia tena hakuna kocha anaeweza kumuacha mkaa benchi everton, Brighton , CSk Moscow, Olympiacos au Getafe eti amchague anaecheza mara kwa mara simba au yanga, hayupo huyo kocha maana fitness anayopata akiwa kwenye training ni zaidi ya anaecheza mara kwa mara simba au yanga.
Ndio maana akina Elneny au Choup Moting wanaitwa timu zao za taifa Egypt na Cameroon pamoja na kukaa benchi kwenye vilabu vyao.
Pia ni sawa sawa na haiwezekani kupatikana timu bora ya taifa kwa wachezaji wanaocheza ligi isiyo bora hata kama wanajuana. Brazil au Argentina sio wajinga timu zao za taifa kuziunda kwa wachezaji asilimia kubwa kutoka ulaya.