Tuache siasa kwenye elimu ya Udaktari na Sheria. Jifunze kikwazo kilichopo Law School of Tanzania

Tuache siasa kwenye elimu ya Udaktari na Sheria. Jifunze kikwazo kilichopo Law School of Tanzania

Waliosoma Law school na kufaulu watanielewa vizuri kwenye uzi huu.

Tusirudie makosa ya kulazimisha watoto wote wa shule ya msingi hata wasiojua kusoma na kuandika wafaulu kilazima na kujiunga na sekondari.

Matokeo yake tumeshaanza kuyaona, Hawa watoto hawawezi kushindana na watoto wa wakubwa waliosoma shule bora, Watoto wa kufaulu bila kujua kusoma na kuandika wataishia kutawaliwa daima.

Kuna kazi kila mtu anaweza kufanya, Lakini kuna kazi zinahitaji specialization.

Taasisi zinazosimamia udaktari na sheria hazipaswi kwenda na mfumo wa kuwaridhisha wanasiasa eti kuongeza idadi ya madaktari na mawakili bila kuangalia uwezo na ubora wa taaluma.

Shule ya sheria Tanzania haina tatizo, Tatizo lililo mbele ni mfumo wa elimu ya sheria vyuo vikuu.

1. Wanafunzi vyuo vikuu Tanzania wanasoma nadharia tu na kukariri mambo, Wanapojiunga law school kuna mambo wanahitajika kuyaweka kwenye mfumo kazi, yaani Practical.

Batch ya pili Law School mwaka 2009± pale Law school nilishuhudia kwa baadhi ya wanafunzi waliofeli na kutaka kuanza kuwaaminisha watu kuwa law school ni ngumu.

Mfano: Vyuoni wanafunzi wanajifunza mambo ya charge sheet kwa kuelezea what is charge sheet? Hii ni hati ya mashtaka na swali hili liliulizwa kwenye ile batch ya 2009±

Law school, Mwanafunzi anaambiwa aandae charge sheet /Hati ya mashtaka kitu ambacho hajawahi kukifanya, Tena anaambiwa with practical example and evidence, ule mwaka wengi waliofeli walishindwa kuaandaa charge sheet lakini wanajua kudefine charge sheet.

2. Exposure ya wanafunzi na vitu vinavyoendelea mahakamani ni mdogo sana, Mambo ya Mahakama yamefanywa siri Tanzania. Kesi hazioneshwi kwenye Television hasa zile zinazovuta umma, Wanafunzi wengi inakuwa ngumu kuelewa uhalisia wa mambo yanavyokwenda kwa mfumo wa kazi, yaani Practical.

Suluhisho
Mfumo wa elimu ni mbovu na ufumuliwe hasa elimu ya nadharia inayowekewa mkazo kwa asilimia 100% vyuo vikuu inabidi igawanywe kwa mfumo wa prolata base yaani 50% iwe practical na watu waende maeneo ambayo kuna kesi nyingi mfano Mahakama ya Kisutu.

Mwanafunzi akitoka chuo practical vizuri ni ngumu kushindwa law school.

2. Muda ni mfupi sana pale law school na sio law school hata mfumo wetu kwenye Board za uhasibu ni vichekesho Sana. Baadhi ya nchi Mwanafunzi anaruhusiwa kusoma chuo kikuu huku akisoma kwenye hizi regulatory schools kama lawa schools na Bodi za uhasibu.

Mwanafunzi anapoanza chuo kikuu anajisajili pia law schools kwenye baadhi ya nchi ili kupata muda mrefu wa kuyafahamu mambo.

Hapa Tanzania Law school imekuwa kwa watu mpaka wanapohitimu sheria, Mfumo huu haufai kwani unampa mwanafunzi muda kidogo wa kujifunza.
100% nakuunga mkono hoja yako

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Nawapongeza sana Law School kwa ku set standards, ukiona una kichwa cha kubebea mizigo , achana na mambo magumu kabebe mizigo kwa m'bichwa wako, mbona utapata tu pesa? Kuna msichana namfahamu ni graduate wa sheria Saut Mwanza, duh..... eti ana upper second kwenye cheti, kichwani hamna kitu kabisa. Nimefurahi sana Law School walivyosema arudie upya darasa la nne B
SAUT nacho ni chuo kikuu?...katika vyuo vya hovyo tz hichi kinaongoza kwa kutoa wahitimu vilaza
 
Tunapaswa kupitia mfumo wetu wa elimu upya. Mfumo ujenge watu kua na uwezo wa kufikiri na kutafakari na kuchambua, na kuhoji sio kukariri tu na kutaka ufaulu mkubwa huku vitu basic tu vya common sense huwezi kuvidadavua.
Nimeipenda hii!, na hapa jf ni mfano halisi wa kinachotokea LST, waalimu wanatunga mitihani kuwapima wanafunzi uwezo wa kufikiri, kutafakari, kuchambua, na kuhoji sio kukariri!, vyuo vinatoa output ya ma copy cats hayana uwezo wa kufanya analysis, wakifeli ni kelele!.
P
 
Nimeipenda hii!, na hapa jf ni mfano halisi wa kinachotokea LST, waalimu wanatunga mitihani kuwapima wanafunzi uwezo wa kufikiri, kutafakari, kuchambua, na kuhoji sio kukariri!, vyuo vinatoa output ya ma copy cats hayana uwezo wa kufanya analysis, wakifeli ni kelele!.
P
Mkuu Paschal, wasomi wa sasa wamejaa ufaulu mzuri lakini hawana analytical skills, reasoning, logical thinking na vitu kama hivyo.

Unakutana na msomi ana vyeti vizuri sana ila sasa vitu basic kabisa vya kutumia common sense hawezi kuvielezea. Ni mfumo wa ajabu kabisa huu tulio nao.

Na kosa kubwa pia linaamza kwa wazazi, wazazi wengi wako obsessed na As za darasani lakini hawahoji uwezo wa watoto wao kwenye kutafakari na kudadavua mambo, wao wanachotaka mtoto apate A ama division one basi. Hii inaweka pressure ama msukumo usio wa kawaida kwa watoto na waalimu ili kukidhi mahitaji ya wazazi ya ufaulu mzuri ila sio uelewa.

Hili tatizo sio tu liko kwenye academic level, hata kwenye professional level kama LST, NBAA nk,. Kite huko wahitimu wanakariri tu ili kufaulu. Huko ndio tulitegemea kuwe tofauti lakini hali ni mbaya zaidi. Wanakuja wanasheria/mawakili na wahasibu wa NBAA uwezo wao mdogo sana ila wako certified na professional bodies.

Tunahitaji kufumua mfumo wetu wa elimu yote kuanzia vidudu hadi chuo kikuu na hadi kwenye professional bodies.
 
Back
Top Bottom