Tuache siasa kwenye elimu ya Udaktari na Sheria. Jifunze kikwazo kilichopo Law School of Tanzania

100% nakuunga mkono hoja yako

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
SAUT nacho ni chuo kikuu?...katika vyuo vya hovyo tz hichi kinaongoza kwa kutoa wahitimu vilaza
 
Tunapaswa kupitia mfumo wetu wa elimu upya. Mfumo ujenge watu kua na uwezo wa kufikiri na kutafakari na kuchambua, na kuhoji sio kukariri tu na kutaka ufaulu mkubwa huku vitu basic tu vya common sense huwezi kuvidadavua.
Nimeipenda hii!, na hapa jf ni mfano halisi wa kinachotokea LST, waalimu wanatunga mitihani kuwapima wanafunzi uwezo wa kufikiri, kutafakari, kuchambua, na kuhoji sio kukariri!, vyuo vinatoa output ya ma copy cats hayana uwezo wa kufanya analysis, wakifeli ni kelele!.
P
 
Mkuu Paschal, wasomi wa sasa wamejaa ufaulu mzuri lakini hawana analytical skills, reasoning, logical thinking na vitu kama hivyo.

Unakutana na msomi ana vyeti vizuri sana ila sasa vitu basic kabisa vya kutumia common sense hawezi kuvielezea. Ni mfumo wa ajabu kabisa huu tulio nao.

Na kosa kubwa pia linaamza kwa wazazi, wazazi wengi wako obsessed na As za darasani lakini hawahoji uwezo wa watoto wao kwenye kutafakari na kudadavua mambo, wao wanachotaka mtoto apate A ama division one basi. Hii inaweka pressure ama msukumo usio wa kawaida kwa watoto na waalimu ili kukidhi mahitaji ya wazazi ya ufaulu mzuri ila sio uelewa.

Hili tatizo sio tu liko kwenye academic level, hata kwenye professional level kama LST, NBAA nk,. Kite huko wahitimu wanakariri tu ili kufaulu. Huko ndio tulitegemea kuwe tofauti lakini hali ni mbaya zaidi. Wanakuja wanasheria/mawakili na wahasibu wa NBAA uwezo wao mdogo sana ila wako certified na professional bodies.

Tunahitaji kufumua mfumo wetu wa elimu yote kuanzia vidudu hadi chuo kikuu na hadi kwenye professional bodies.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…