Mzalendo Uchwara
JF-Expert Member
- Jan 26, 2020
- 4,437
- 13,836
Kwa miaka nenda rudi genge la wazalishaji wa sukari wamekuwa wakilichezea soko letu ili kupiga super profit.
Wanatengeneza uhaba wa sukari, wanaacha ipande bei, kisha wanapata vibali vya kuagiza nje na kuuza kwa bei ya juu. Tena wakati mwingine wanabadili vifungashio ili ionekane imezalishwa nchini.
Sukari ya nchi za nje kama vile Brazil na Maritius ni bei poa mno, kwahiyo hawa mabwana walikuwa na kila motisha ya kutafuta namna ya kutengeneza uhaba wa sukari ili wapewe vibali vya kuagiza..
Alichokifanya waziri Bashe sio tu ni uamizi sahihi bali ni uamizi wa kizalendo, nchi haiwezi kuwa inashikwa mateka na genge la watu wachache.
Alichokisema Luhaga juu watu wachache kuhodhi sukari: Luhaga Mpina: Usambazaji wa sukari haukuwa ukifanywa na mfanyabiashara mmoja wa Mwanza pekee, Waziri Bashe alidanganya
Going foward hii ndio iwe dawa, tuendelee kulilinda soko la wazalishaji wa ndani lakini pale kunapotokea uhaba basi yeyote mwenye uwezo apewe kibali cha kuagiza sukari haraka iwezekanavyo.
Hongera Mh. Bashe kwa kufikiri nje ya box na kuthubutu. Kwenye hili Mpina amechemka, yaani nchi ikose bidhaa muhimu kwasababu tu kuna wapuuzi wanajivutavuta kuagiza sukari? Thubutu!
=====
Kupata ushahidi na ufafanuzi wa Luhaga juu ya Mpina juu ya sakata la uhaba wa sukari soma:
- Luhaga Mpina: Waziri Bashe na Mwigulu walitengeneza uhaba wa sukari nchini, zilikuwa njama za kuiba mapato ya nchi
- Luhaga Mpina amshukia Waziri Bashe, adai amelidanganya Bunge, awataja Magufuli, Rais Samia
- FULL TEXT: Maelezo ya Ushahidi wa Luhaga Mpina kwa Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson juu ya Waziri Hussein Bashe kusema Uongo Bungeni kuhusu Sukari