Tuache Unafiki: Bashe alichukua hatua sahihi kumaliza tatizo la sukari. Hongera Dr. Tulia kwa kumlinda na kulinda maslahi ya nchi

Jitathimini ndugu.
Kama vipi wai kliniki ya afya ya ufahamu
 
Watanzania sijui huwa hawajielewi. Wamiliki wa viwanda huwa wanatengeneza mfumo wa kuadimika kwa sukari na kupandisha sana bei za sukari. Kama mimi ndo mzalishaji na ndo mwenye liseni ya kuagiza sukari kwa nn nisitengeneze mpango wa sukari kuadimika nipige hela?

Kama wafanyabiashara wamepewa vibali vya kuagiza sukari nje, na sukari ikaagizwa, ikaja kwa viwango vizuri vya kuweza kutumika na binadamu, na bei ya sukari ikawa chini, mwananchi wa kule kijijini akanunua sukari kwa bei ya chini na akapata ahueni ya maisha, sioni tatizo!!

Kama hiyo sukari iliyochukuliwa imefanya bei ya sukari kuwa juu zaidi hapo ndo penye shida.

Ila kama kelele zote ni kulindiana sijui maslahi viwanda vya ndani itakuwaje huu ni upumbavu!! Watengeneze mazingira ambayo yatakuwa competitive kwao kushindana na viwanda vya nje hata sukari ikiingizwa nchini ya kwao ndo iwe bei nafuu kuliko hiyo iliyokuwa imported!! Wananchi watakimbilia product yao, lakini siyo kumuumiza mtanzania kwa kigezo cha kipumbavu eti kulinda viwanda!! Washindane washinde!
 
Katumia m@tak0 huyo
 
Sio tu akili timamu, bali nazijui hizo mishe nje ndani, nilishakuwa mdau kwenye uzalishaji wa sukari zaidi ya miaka 10. Niulize chochote kuhusu Kilombero sugar, Mtibwa sugar au Kagera Sugar.
Ok, wewe unayeijua sekta hii vizuri tusaidie ufafanuzi wa hoja hii,

Wazalishaji wa sukari walimtaarifu waziri kwa barua juu ya uhaba wa sukari tangu mwezi novemba kutokana na uwepo wa elnino. Wakamkumbusha tena Desemba, akatoa vibali Februali akitaka sukari iwe imeingizwa ndani ya siku 14 jambo ambalo anajua haiwezekani. Hoja,

1.Je kati ya waziri na wazalishaji nani alisababisha uhaba wa sukari?

2. Kwa nini alichelewa kutoa vibali na baadae akavitoa akijua kwa muda huo wazalishaji hawataweza kuingiza sukari na badala yake akatengeneza kampuni zake za mfukoni zisizo na sifa kinyume na Sheria na kuzipa tenda ya kufanya biashara ambayo hawaijui na hawajawahi kuifanya?

3. Kwa nini hata kiwango cha sukari iliyopendekezwa na bodi kuingizwa tani laki 3 waziri alizidisha na kuingiza tani laki 4.1

4. Kwa nini Waziri mwenye vyombo vya dola alishindwa hata kutangaza rasmi na kusimamia bei elekezi hadi sukari hiyo hiyo iliyoagizwa kwa vibali vyake ikauzwa sh 10,000 kwa kg huku akiwa ametoa msamaha wa kodi kwa makampini hayo ya mfukoni hayo? Ni hasara kiasi gani taifa limepata au fedha kiasi gani hayo makampuni ya mfukoni (utakatishaji) wameifisidi serikali?

5. Je wewe unaonaje hali ya usalama kwa taifa kwa mtu asiyejua UBORA wa kitu chenyewe kupewa kazi hiyo hata bila kuthibitishwa na vyombo husika, kampuni za simu, stationary, store, nk zenye usajili tata na mtaji usiozidi 1,000,000. Huu ni utakatishaji wa fedha ulio dhahiri.
 
Sukari huko kwenu kilo shillingi ngapi?
 
Hii ndio mifano ya Gen - Z ya Tanganyika, machawa yasiyo na akili.
Achana na mambo ya kimarekani hayo ya gen z sijui. Kesho watataka muwe mashoga na mtakubali, kwanini vijana wa ki Afrika mnapenda kuigaiga mambo ya wazungu nyie??
 
Sawa mmiliki wa stationery
 
Mambo ni mengi kuelekea 2030
 
Unamwamini Mpina?? Hayo ni maelezo ya Mpina copy and paste. Mengi ni ya uongo. Na ndio maana anakwenda kula rungu zito kule bungeni.
 
Sawa Bashe tumekusikia. Wewe ni fisadi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…