Tuache Unafiki: Bashe alichukua hatua sahihi kumaliza tatizo la sukari. Hongera Dr. Tulia kwa kumlinda na kulinda maslahi ya nchi

Typical JPM follower huna akili kabisa. Sasa nchi ina uhaba wa sukari, kilo ikauzwa mpaka elfu 8 eti mtu analeta Sukari hadi bei imeshuka watu bado mnalalamika.

Ingekua kosa kama angempa tender mtu mmoja pekee tungesema ni monopoly. Cha ajabu wameleta watu wengi na bei imeshuka sasa lawama za nini?

Je tulitaka sukari iuzwe kilo elfu 6 kisa wenye vibali hawaagizi? Hii nchi ina ujinga mwingi hatuwezi kuwa held hostage na watu wachache.

Kwa hili namuunga mkono Bashe,
 
Kwahiyo mfano siku DP world ikigoma kupakua mizigo basi nchi ikae bila huduma ya bandari kisa "taratibu" na "kanuni" za kumpata mwekezaji mpya "zinashughulikiwa"??

Hivi itakua nchi au kampuni binafsi?
 
Naunga mkono hoja yako asilimia 100
 
Kwahiyo mfano siku DP world ikigoma kupakua mizigo basi nchi ikae bila huduma ya bandari kisa "taratibu" na "kanuni" za kumpata mwekezaji mpya "zinashughulikiwa"??

Hivi itakua nchi au kampuni binafsi?
Kosa moja halihalalishi kosa jingine.
Sheria na taratibu zipo zifuatwe sasa zinatungwa kwa nini?
Embu acha kujitoa ufahamu kutetea wizi
 
Serikali yetu inajitabanaisha kama serikali inayofuata sheria.
Serikali inatumia fedha nyingi sana kugharamia utungaji wa sheria hizo sasa haikubaliki mtu avunje sheria tena waziri na alidanganye na bunge kwa sababu yeyote ile acheni wizi
 
Mpina kaongwa hela na wenye viwanda
 
Hivi mnatumiaga makalio kufikiria??.

Uhaba?? Nini ilikua kiini Cha uhaba huo wa Sukari?.

Je wazawa wetu wa Ndani wanaozalisha Sukari, waloshindwa ku anticipate mapema kua kutakua na uhaba??.

Na kama walijua Hilo, walitoa taarifa Kwa Bodi ya Sukari?.

Na kama Walitoa, walitoa muda gan?.


Je kama wazawa ambao Sheria inawapa Hali ya kuagiza Sukari, je BASHE aliwapa Kibali Baada ya muda gan Toka waandike Barua Yao??.


Kwa akili yako ndogo tu, unadhan Wazawa wetu Wamiliki wa Viwanda, wangeshindwa kuingia Sukari Ndani ya Nchi mapema kabisa, ikiwa Vibali wangewepa mapema??.


Kwamba Mtu ambaye shughuli zake zote ni Sukari, ashindwe kuingiza Sukari, badala yake mtu wa STATIONARY mwenye mtaji wa million Moja, Aweze kuleta Sukari Tani na matani??.


Kwamba kosa kama angempa mtu Mmoja?? Are you serious ?? Sheria zinataka Kibali Akina nani??

Je BASHE baada ya yeye kuona Wazawa wameshindwa , je alitangaza tenda hiyo kama Sheria zinavyotaka??.


Tukisema nyuma ya hizo kampuni uchwara, Kuna Fedha HARAMU za watu wachache , tutakua tumekosea?.


Yaan Bashe Atengeneze tatizo, aje na solution yake, alafu tumxhekee??.



Nia yake ni ipi?? Kuua Viwanda vya wazawa??? Kuua Ajira za watanzania? Kupunguza Kodi ?? Kuua Kilimo na kuua Wakulima??.


Hivi mna ukichaa????? .

Mnadhani Late JPM, alipoamua kufufua vya kwetu Hakua na akili??.

Yaan Leo hii, turuhusu Viwanda kufa, Kilimo Cha miwa kufa, Ajira kufa, Umasikini kuongezeka kisa TUMEMILIKISHA BIASHARA YA SUKARI KWA MAJAMBAZI YASOPUNGUA 10 ??.


NI AKILI AU MATOPE??.
 
Kumbe ni Mzalendo Uchwara????? 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Nayajua majibu ya hayo maswali yote. Narudia tena, nimefanya kazi Kilombero sugar, Mtibwa sugar na Kagera Sugar. Wewe unasimuliwa hayo mambo, mimi nayajua kwa undani.

Uhaba wa sukari ulitengenezwa na wazalishaji wa sukari wenyewe wakitegemea ku exploit fursa ya wao kuwa waagizaji pekee wa sukari toka nje kwa ajili ya kufidia pengo lililopo kwenye uzalishaji.

Kwahiyo watu hao hawawezi kuwa part ya solution. Kuhusu nini kitatokea baada ya kujaza sukari ya bei nafuu kwenye soko ni hao wazalishaji kujifunza na kutorudia ujinga huo.

Some people can only learn the hard way. Walitegemea super profit sasa wanakwenda kula hasara. Hawatarudia ujinga huo next time. Na waziri kawaambia waziwazi, warudie waone.

Huyo Mpina hawezi kuwasidia. Waache konakona wafanye wajibu wao, kama umewashinda basi waachie hivyo viwanda wapewe wengine wenye uwezo wa kuendesha.
 
Bashe yupo sahihi sukari imeagizwa na kuletwa, imesambazwa wananchi wamepata unafuu. Swala la kiwango kuwa kikubwa ametolea ufafanuzi kuwa ni kutokana na hali ya hewa, mvua kuwa nyingi mwaka huu miundo mbinu ya uingiaji mashambani kuwa mgumu na hali hiyo itapelekea viwanda vyetu kuchelewa kuanza uzalishaji kwa muda mrefu, hivyo ili kuondokana na tatizo la upungufu wa sukali Wizara ikaagiza kiwango kikubwa. Kuhusu nani amepewa kibali wakati sukari imeletwa sioni kasoro, wangeshindwa au kuleta kwa bei kubwa hapo tatizo lingekuwepo. Mpina Msukuma na anasukumwa na wajanja waliobanwa maslahi yao
 
Ukiondoa kodi na ushuru mwingine kwenye sukari, kilo moja ya sukari itauzwa chini ya shilingi 1,000. Sasa hapo ndio utajua anaemuumiza mwananchi ni nani.

Kwa hoja hii tuache kupambana na waagiza sukari, tupambane na serikali iondoe kodi kandamizi kwa wazalishaji ili bei iwe nafuu kwa mlaji.

Na siyo kupambana na anayeingiza sukari nchini then tunaacha kile kinachosababisha maisha yetu kuwa duni.

Wenzetu Kenya wanaelewa umuhimu wa sheria zinazopitishwa namna zitakavyokandamiza wananchi.

Hata leo hii Bashe angefuata sheria bado hizi cartels za wazalishaji wa sukari wangefanya kila namna sukari iadimike ili wapige faida ndefu zaidi.
 
Serikali yetu inajitabanaisha kama serikali inayofuata sheria.
Serikali inatumia fedha nyingi sana kugharamia utungaji wa sheria hizo sasa haikubaliki mtu avunje sheria tena waziri na alidanganye na bunge kwa sababu yeyote ile acheni wizi

Kwa hiyo sheria ifuatwe tu hata kama inaonyesha kuwa na mapungufu!! Hili nakataaa kuwatetea hawa wenye viwanda.

Hoja ya Mpina ukiingalia kwa jicho la tatu imejikita kutengeneza monopoly ya viwanda vya ndani kuumiza wananchi!! Kuwatengenezea nafasi ya kutoshindana ili kuumiza wananchi!! Wakubaliane na hali washindane na wazalishaji wa viwanda vya nje.

Sisi tunachotaka walaji ni sukari ishuke bei, hizi nyingine ni bla, bla bla tu,
 
Je wazawa wetu wa Ndani wanaozalisha Sukari, waloshindwa ku anticipate mapema kua kutakua na uhaba??.
Walijua uhaba unakuja ila ni faida kwao maana supply ikiwa ndogo demand inapanda na ndio maana bei ikafika elfu 8 kwa kilo na kuna maeneo ilikua haipatikani kabisa.

Wazalishaji wa ndani hawawezi anticipate maana scarcity ndio huwanufaisha.
 
Kinachohitajika ni sukari ipatikane kwa bei nafuu.hayo ya nani mzalishaji au muingizaji wala hayana umuhimu kwa mwanachi wa kawaida kwasababu hayo yanakuja kutokana na usimamizi na uwajibikaji mbovu.
 
Kwamba Mtu ambaye shughuli zake zote ni Sukari, ashindwe kuingiza Sukari, badala yake mtu wa STATIONARY mwenye mtaji wa million Moja, Aweze kuleta Sukari Tani na matani??.
Acha kukariri tokea enzi za JPM hata Bakwata wana kibali cha kuagiza sukari kwani Bakwata wana kiwanda cha sukari? Kuna mambo kama hujui uliza.

Kampuni huwa zinafanya multiple business, ndio maana hata NMB licha ya kwamba ni benki ila imeshinda tender ya kutengeneza vitambulisho vya JAMII NUMBER!! Let alone inafanya biashara ya data hosting.

Jitahidi kutafuta exposure sio kuleta ujuaji kwenye mambo yaliyokuzidi uwezo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…