Tuache unafiki kipato cha tsh 7,000 kwa siku ni umasikini wa kutupa

Tuache unafiki kipato cha tsh 7,000 kwa siku ni umasikini wa kutupa

Mwendeshaji wa boda boda anapata kiasi gani kwa siku. Sio sio malipo ya ruti. Ruti sio pesa ya mwendesha bodaboda hizo kitaalamu wanaita gross sales🤔
Hujui hii kazi ya boda ilivyo

Iko hv mwendeshaji anapata hela kubwa kuliko mwenye pikpik,pia siku hz wengi pikpik ni za kwao

Kwa siku kama jiji la dar,boda boda anapiga zaidi ya 30,000 kwa siku

Uwe una uliza kwanza kabla ya kukurupuka
 
Hakuna bodaboda angeendelea kufanya hivyo kazi kwa kipato cha 7000 kwa siku.Hivi kipato cha wastani kwa watanzania wengi ni shillingi ngapi kwa siku?Hali ya uchumi ya watanzania na wengi wa majirani zetu inaeleweka.
Msijifanye kushangaa na kuwashauri watu wale keki kwa kwa sababu kuna ukosefu wa mikate.Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa mataifa na World Bank watanzania wengi wanaishi kwa kipato cha chini ya dola 2 kwa siku.
Huu ndio uhalisia. Mnaishi mijini na kuhukumu watu.Tembeleeni vijijini muone uhalisia wa maisha ya watanzania wengi.
 
Naona watu humu wanatoa tathmini ya mapato ya boda boda kwa kuhisia tu,eti anapata 15000 kwa siku,nyie mnasimuliwa hamjui uhalisia wa biashara hii kwa sasa.boda boda Sasa hivi zimejaa Kila Kona yaani ukifanikiwa kuingiza 10000 kwa siku kwenye boda boda siku hiyo katambike kwenye mizimu ya kwenu,hiyo kwa sasa siyo kazi ni LAANA yule jamaa hakukosea kusema hivyo.Tuache kuropoka vitu tusivyovijua
 
Bodaboda gani anapata elfu 7 tu kwa siku ?
Bodaboda analipa kwa boss elfu 10 bado anabaki na hela yake Kama elfu 10 au zaidi..Kama pikipiki Ni ya kwake anapata zaidi ya elfu 15 kwa siku..

..wabunge wangapi wa Ccm wanatamani kuacha ubunge ili wakaendeshe bodaboda?

..Mawaziri wangapi wa Ccm wanatamani kuachia V-8 ili watumie usafiri wa bodaboda?
 
Hakuna bodaboda angeendelea kufanya hivyo kazi kwa kipato cha 7000 kwa siku.Hivi kipato cha wastani kwa watanzania wengi ni shillingi ngapi kwa siku?Hali ya uchumi ya watanzania na wengi wa majirani zetu inaeleweka.
Msijifanye kushangaa na kuwashauri watu wale keki kwa kwa sababu kuna ukosefu wa mikate.Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa mataifa na World Bank watanzania wengi wanaishi kwa kipato cha chini ya dola 2 kwa siku.
Huu ndio uhalisia. Mnaishi mijini na kuhukumu watu.Tembeleeni vijijini muone uhalisia wa maisha ya watanzania wengi.
Vyema kabisa.
 
Mwendeshaji wa boda boda anapata kiasi gani kwa siku. Sio sio malipo ya ruti. Ruti sio pesa ya mwendesha bodaboda hizo kitaalamu wanaita gross sales[emoji848]
BadoBoda average kwa siku hupata 20-30 elfu Amini hilo baada ya matunizi yake
 
850000 × 365 = 310,250,000

Kwa hiyo wewe ulitaka kutuaminksha unaingiza 310,250,000/- kwa mwaka?

Hili sio tangazo kweli la kupata mademu. I wonder 🤔
Mbona kidogo hiyo, mtu anawastani wa mauzo ya 15mln pa day, hata kama anauza siment au nondo na kwa kila mfuko pengine anapata sh 3000 kokotoa hapo uone anaingiza sh? Kwa siku
 
ukianza kufuatilia hizi kazi na kuziita LAANA kwa kigezo cha kipato basi hata kazi za viwandani ni laana maana kule walio wengi wanalipwa elfu tano mpaka nane kwa siku, saidia fundi ni LAANA na ni hatari zaidi kiafya maana hawa wanalipwa elfu kumi mpaka kumi na tano kwa siku hapo umevuta na vumbi la cement la kutosha...kwangu mimi kazi yoyote halali huwezi iita LAANA kisa inaingiza kipato cha chini, muhimu ni kuangalia namna ya kuiboresha tu kwa kuanzia hapa panapoonekana hakufai
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Watanzania tutafute suluhisho na sio kuwa wanafiki. Kipato cha tsh 7,000 kwa siku hakitoshi na ni umasikini. Tunaweza kutofautiana kwenye siasa lakini sio ukweli hili. Badala ya kujidanganya tutafute mbinu bora. Vilevile boda boda hazija tengenezwa kwasababu ya usafiri wa abiria na inatakiwa kuwa na lesini maalumu za bodaboda ili kupunguza ajali ambazo zingeweza kuepukika.

Tusiweke utamaduni wa ubishi usio na msingi hata kwa mambo yaliyo wazi.

Lakini tuulize wataalamu wa afya kama ni vizuri kuendesha Pikipiki kwa masaa 12 kwa siku sita au saba tuone watasemaje. Bodaboda inatakiwa kuwa kama kazi za mpito na jamii zetu zinatakiwa kufikiria mbinu tofauti.

Lakini Mama Samia anajaribu sana kuanzia kwenye Veta na mashamba ya mikakati lakini hii haina maana Lema anachosema sio sawa.

Lakini tumeona umuhimu wa uhuru na mikutano kuruhusiwa sasa tuna mawazo tofauti ya kujadili ili tuwe na jamii bora. Kwanini huu mjadala hauja jadiliwa mpaka leo Lema ndiyo aseme ?

Niongezee tu hapa mimi naamini waendesha bodaboda wataweza kuwa viongozi wa baadae. Mimi mwaka 2000 nilikuwa naingiza kwa pesa za Tsh 95,000 kwa siku. Leo hii kipato changu kwa siku moja ni Tsh 850,000 kabla ya makato. Somo ni kwamba inawezekana lakini lazima ukubali hali halisi
Kama kipato chako ni laki nane na nusu kwa siku usinge kuwa na muda wa kutroll mitandaoni kuongea ujinga kwamba bodaboda anapata 7000 kwa siku bila taarifa yoyete labda huyo ni bodaboda wa kijijini uliko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona watu humu wanatoa tathmini ya mapato ya boda boda kwa kuhisia tu,eti anapata 15000 kwa siku,nyie mnasimuliwa hamjui uhalisia wa biashara hii kwa sasa.boda boda Sasa hivi zimejaa Kila Kona yaani ukifanikiwa kuingiza 10000 kwa siku kwenye boda boda siku hiyo katambike kwenye mizimu ya kwenu,hiyo kwa sasa siyo kazi ni LAANA yule jamaa hakukosea kusema hivyo.Tuache kuropoka vitu tusivyovijua
Sasa kama wewe unaendesha bodaboda Kijijini utapataje hata 5000 Kwa siku?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bodaboda gani anapata elfu 7 tu kwa siku ?
Bodaboda analipa kwa boss elfu 10 bado anabaki na hela yake Kama elfu 10 au zaidi..Kama pikipiki Ni ya kwake anapata zaidi ya elfu 15 kwa siku..
Asante mkuu. Umefafanua vema ila ngoja nikazie. Tukizungumzia bodaboda tuna makundi 3;
(1) Walioajiriwa na wanaopeleka hesabu ya siku kwa boss (kati ya 7k to 10k).

(2) Wanaoendesha bodaboda lakini ni mali zao binafsi (pesa yote inayopatikana kwa siku ni stahiki yao).

(3) Wanaoendesha boda boda kwa mkataba, yaani baada ya muda fulani wa kupeleka hesabu kwa boss ile bodaboda inakuwa mali yao.

Sasa huyu mtoa mada amekuja na 'findings' ambazo hazijatokana na uchambuzi makini kwa kuzingatia makundi hayo hapo juu. Kwa mfano tu, mtu wa kundi la pili anaweza kuingiza pesa nyingi tu tofauti na yule wa kundi la 1.

Huyu mtoa mada amefanya kitu kinaitwa 'fallacy of generalization'. Aende akajipange halafu arudi tena.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Nchi maskini sana acheni watu wajisaidie wanavyoweza, umachinga na bodaboda ndio kazi nyingi zinazopatikana kwa sasa acha watu wafanye ili waishi, siipendi CCM naamini imejaa wapumbavu watupu, Lema needs to chill asilete akili yake na mawazo yake ya Canada kwa nchi kama Tanzania ambayo watu wengi hawajui haki zao na wanawaona viongozi wa serikali kama class nyingine ya hali ya juu
 
Huko sahihi mkuu hata yeye akiingia ikulu bodaboda na wamachinga ni ngumu kuzuia watakuwepo tu, vilevile jamii yetu ya kiafrica haipendi kuambiwa ukweli ukisema ukweli wewe ni mbaya, wengi walimchukia jpm kwa sababu ya ukweli wake.
 
Mbona kidogo hiyo, mtu anawastani wa mauzo ya 15mln pa day, hata kama anauza siment au nondo na kwa kila mfuko pengine anapata sh 3000 kokotoa hapo uone anaingiza sh? Kwa siku
Ndio maana anadharau bodaboda si ndio?
Mtu anayeingiza laki nane na anajua maisha ni nini hawezi dharau elfu 7. .
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Ndio maana anadharau bodaboda si ndio?
Mtu anayeingiza laki nane na anajua maisha ni nini hawezi dharau elfu 7. .
kiafya na kiusalama sio sawa kuzunguka na boda boda masaa zaidi ya 12 na ndio mana tunaona ajali nyingi zinatokea vijana wanavunjika wengi wamepata ulemavu wa kudumu kuruhusu hii mikutano ya kisiasa kunasaidia kupata mawazo mbadala ni muda sasa tuangalie tutazitumiaje raslimali tulizonazo kama ardhi mito na maziwa tuwawezesha vijana kujikwamua kiuchumi pasipo na athari zote za kiafya na kiusalama
 
aliyekuambia anazunguka masaa 12 ni nani? uliambiwa na nani hivyo
 
Back
Top Bottom