Tuacheni Kujipa Moyo, Ndoa kwa Kizazi cha Sasa ni Gereza la Mateso

Mkuu hata ukioa ambaye hana kitu ila akishaanza anza vikoba na stories na majirani akishajua mambo ya kugawana nusu kwa nusu hilo ni bomu anajua ndoa ikivunjika yeye ndio anafaidika uwe hata unakijumba kimoja.
 
Ama kweli,siti ya mtu mmoja mnaweza kukaa wawili na safari ikaendelea duh!.

Maisha ni kusaidiana,ukimpata mwanamke mwelewa,mcha mungu,mwenye hofu na mungu.Basi mwanaume hata uyumbeje atakuwa ngao yako,hatopenda kuona unakosa furaha.Yuko radhi kukupatia heshima popote pale,
Ila ikiwa unampenda,unamjali,unandhamini pia.
Mwanamke nae ni binadamu anahitaji kupendwa na mda wote kufokewa na kuonekana kwamba hawezi jambo lolote paspo mwaume.Mpe nafasi mpe uhuru mwamini,maana kuna Leo na kesho.Wekeni misingi ya kuonekana mnategemeana ambapo hata Kama mwanaume utapata ajali basi familia isiteteleke.

Ila wanaume tunakosea pale unapotaka kujitangaza we mwamba badala mkeo ndo akutangaze we mwamba.

Kikubwa ni upendo pande zote mbili.
Kama ni heshima,mbona Nyani wanaheshimiana,kwani kuna wanavyomiliki zaidi ya kuishi juu ya miti.

Mwanamke ukimfanya rafiki yako Mambo mengi yanasonga.

Pia sio kila mwanaume ana akili chanya,wengine ni Viazi tu.

Kutafuta ni wajibu was kila mtu kutafuta,maana kuna kufa pia.
 
Naona watu wana chochea kizazi haramu kwa nguvu zote sasa.
si kweli watu wanapenda kuzaa nje ya ndoa lakini tafiti zisizo rasmi zinaonyesha matokeo yafuatayo katika kila hatua hasa kwa dada zetu ambao kwa mazingira yao kunauwezekano wa ukomo wa uzao kadri muda unavyokwenda.
  • anamaliza darasa la saba akiwa ni binti wa miaka 14-15 baada ya miaka minne atakuwa na miaka 18-19 ikiwa hakuweza kuendelea na shule akajishughulisha na shughuli ya kukuza kipato kidogo akifikisha 20-21 ataona bora atafute mtu azae kwa kuwa school mate wake anakaribia kumaliza chuo au amemaliza sasa yeye ananini cha kujivunia?
  • akifanikiwa kwenda mpaka kidato cha nne atamaliza akiwa na umri wa miaka 18-19 baada ya miaka minne kama hakukuwa kozi yoyote atakuwa na miaka 22-23 na yeye atafanya hivyo hivyo kwa kuzaa akiwa na miaka 25
ngazi zingine nisiendelee lakini iko hivi kila hatua ikizidi miaka minne toka umeikamilisha ni kazi kupata mume vinginevyo ukutane na mume ambaye kiukweli ameshatumika.
lakini ukifanikiwa kupata kazi nayo ikizidi minne hujaolewa unarudi palepale.
kwa kifupi si kwamba wanapenda mazingira ndio yanayolazimisha sidhani kama tunahitaji kuwaraumu na kuona wametoa watoto haramu
 
Dhambi iyo by the way ata Mimi nafikiria kufanya hivyo
 
Mwamba katika Ubora wako.Ahsante kwa Bandiko Nzuri
Kongore
 
Vijana wenyewe wengi wao ni Slayking. Hapo kuna ndoa hapo.

Ndoa inahitaji Mwanamke haswa na Mwanaume Haswa.
Waliokubali kufuata mifumo ya kizamani Kwa kuifanyia marekebisho kidogo kulinda nafasi ya kila mmoja ndani ya Ndoa
Sitaki kukuhukumu mapema. Nimesoma thread yako nimekuelewa ila naomba nisaidie kitu kimoja. Unasema tufate mifumo ya kizamani huku tukiweka usasa ili tufanikiwe kwenye ndoa.

Naomba nipe walau mifano miwili ya mifumo ya kizamani ipitie transtion ya kisasa.
 
Mkuu hivi ulichoandika uko serious kweli? Huyo mtoto unayetaka akusaidie uzeeni akikuuliza mama yuko wapi utamjibu nini? Kwa mantiki hiyo utamziaje huyo mtoto wako asije kuwa kama hao kwenye picha?

Ndugu Robert Heriel hii kampeni yako ya kataa ndoa kuna watu unaona mawazo yao yalipo? Ukikataa ndoa then solution yake nini? Si ndio mambo haya ya ushoga na yanakuja? Mimi nadhani tunapaswa kuelimishana namna ya kuishi kwenye hiyo mifumo ya kizamani na sio kukataa ndoa. Kuna watu wanawehuka na jamii inaenda kuharibika kama huyu mwenye hii comment.
 

Mkuu sijawahi kukataa Ndoa mahali popote.
Kuna sehemu unapishana na Mimi.
Soma Kwa utulivu
 


Aiseeh hii mashine hii imefunguka atakaye yapinga haya huyo NI chizii
 

Vizuri.

Mfano WA mfumo wa kizamani, Baba ndiye kila kitu, Mtoa mawazo na mawazo yake hayapingwi.
Maboresho; Baba Abaki kuwa Mtoa mawazo kama awali Ila yajadiliwe, yapimwe ikiwezekana yapingwe ikiwa yamekengeuka.
Na Hilo litafanyika kupitia uhuru, Haki, ukweli na upendo ikiwa vitakuwa ndio nguzo muhimu ya Familia.

Mwanamke asichukuliwe kama chombo kisichoweza kufanya lolote, Bali achukuliwe kama msaidizi na mshirika muhimu katika familia.

Hata hivyo mfumo wa kisasa uliolenga kumfanya Mwanamke naye awe kama sehemu kuu au kichwa cha familia, itaathiri pakubwa ndoa na familia nyingi.
Mfano, Vijana WA siku hizi wanawaachia Wanawake kuwa wazalishaji na wahudumiaji wakuu wa familia Jambo ambalo ni kinyume na misingi Mkuu wa Ndoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…