FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 38,920
- 44,970
Pia ikumbukwe hatupingi kuoa, bali tuna kataa ndoa!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Elewa, hakuna anaepinga kuoa, bali tunakataa ndoa!Watoto wa nje shetani ameamua kuwatumia kupinga ndoa ambao ndio mpango wa Mungu.
Ukipinga ndoa unaunga mkono ushoga, usagaji, uzinzi, punyeto nk
Ndoa ni mpango wa Mungu. Kinyume cha ndoa ni doa, na ukitaka kuliepuka doa, OA.Elewa, hakuna anaepinga kuoa, bali tunakataa ndoa!
Kitu sahihi ni ndoa,Ndoa ni mpango wa Mungu. Kinyume cha ndoa ni doa, na ukitaka kuliepuka doa, OA.
NDOA
DOA
OA
Mi nimeoa zamani tu, na watoto ninao wa kutosha, ila ndoa sifungi, ujue kutofautisha dogo..; Kataa ndoa. Tambua watu ‘wanafunga ndoa’, kwani iwe ‘kufunga’ na sio ‘kufungua’, kwamba ni kifungo au sio? 😂😂Ndoa ni mpango wa Mungu. Kinyume cha ndoa ni doa, na ukitaka kuliepuka doa, OA.
NDOA
DOA
OA
Mwalimu wako alipata tabu kukufundisha, mzazi wako alipoteza pesa kukusomesha bora hiyo pesa angenunua mashamba awekeze angepata faida.Wabongo mnaotangaza hii kauli mbiu mna tofauti gani na wanaoueneza ushoga na imani ya LGBTQ?
The world order imetengeneza mfumo mzuri wa ndoa, watoto wazaliwe ndani ya ndoa ili wawe na misingi mizuri pamoja na malezi mazuri kutoka pande zote.
Sasa wewe kama hutaki ndoa baki hivyo na imani yako, kwanini ui project hiyo imani yako kwa watu wengine? Leo mnasema kwanini wazungu wanasambaza ushoga ila nyie pia mnafanya the same thing kusambaza hiyo kataa ndoa inamaana watu wawe mashoga, wawe wazinzi, wazidi kuzaliana single mothers na watoto wanalelewa bila baba.
Jitafakarini
Acha upumbavu, hakuna sehemu umeambiwa ukatae ndoa na mtoa mada, ila umeambiwa utumie sheria za asili(zamani)ili uweze kuyamudu mapenzi, Watanzania wengi kweli akili bado ni takataka, kusoma unaweza lakini kuelewa huwezi? Umuhimu wa shule ukowapi hapo? Sasa watoto wako utawafundisha nini kama huwezi kuelewa mada nyepesi kama hii? Ninyi ndio mnaofanya wanawake wadharaulike na kuongeza idadi ya machokoraa mitaani sababu ya kuikataa elimu asilia ya mahusiano.Mkuu hivi ulichoandika uko serious kweli? Huyo mtoto unayetaka akusaidie uzeeni akikuuliza mama yuko wapi utamjibu nini? Kwa mantiki hiyo utamziaje huyo mtoto wako asije kuwa kama hao kwenye picha?
Ndugu Robert Heriel hii kampeni yako ya kataa ndoa kuna watu unaona mawazo yao yalipo? Ukikataa ndoa then solution yake nini? Si ndio mambo haya ya ushoga na yanakuja? Mimi nadhani tunapaswa kuelimishana namna ya kuishi kwenye hiyo mifumo ya kizamani na sio kukataa ndoa. Kuna watu wanawehuka na jamii inaenda kuharibika kama huyu mwenye hii comment.
Kinaweza kikawa kibovu kwako kwa mwenzio ni kipya.Kuna vibovu sokon kwasababu bado kuna wajinga wanaenda kununua
Wewe ndo umewashwa na umejikuna pasipo husika. Mtoa mada ni mwandishi mzuri tu na huwa namuelewa. Nawajibu wanao kuja kucomment kwasababu huwa nakutana nao kwenye hizi mada mara nyingi. Na nnachokiongea ntakisimamia hadi siku ya mwisho. Acheni watu waoane wakishindwana watawanyike mbona simple. Msituletee kizazi haramu hapa. Na kwanza nyie ndo mnaongoza kutukana single mothers humu ila sijawahi skia mtu akitukana single father. HamjielewiMwalimu wako alipata tabu kukufundisha, mzazi wako alipoteza pesa kukusomesha bora hiyo pesa angenunua mashamba awekeze angepata faida.
Mtoa mada hakuna sehemu aliyosema ama kakataza watu wasioe bali kakazia mwanaume kuurudia uanaume wake na sheria zake za kizaman ili aweze kuishi vzr na mwanamke, pia mwanamke kutii sheria za asili ambazo zilitumiwa na watu wa zamani ktk ndoa,
Na kakazia kuwa kama mwanaume hana uwezo wa kumuhandle mwanamke kwann aoe? kama sio kutafta matatizo, na mwanamke kama hana uwezo wa kutii sheria za asili za ndoa aolewe? Hapa ndipo linapoibuka Suala la KATAA NDOA ZA MICHONGO michongo yenyewe ndio hizo ndoa za kuoa watu wasiojielewa wala kujua maana ya ndoa.
Mnapocomment muwe mnasoma vizuri maana kabla ya kupayuka humu
Attention seeker. Am sorry man you hit a wrong door. Unazidi kuprove kati yangu na wewe nani MPUMBAVU na nyie ndio mashoga wenyewe tunaowapinga kenge mpeku wewe.Acha upumbavu, hakuna sehemu umeambiwa ukatae ndoa na mtoa mada, ila umeambiwa utumie sheria za asili(zamani)ili uweze kuyamudu mapenzi, Watanzania wengi kweli akili bado ni takataka, kusoma unaweza lakini kuelewa huwezi? Umuhimu wa shule ukowapi hapo? Sasa watoto wako utawafundisha nini kama huwezi kuelewa mada nyepesi kama hii? Ninyi ndio mnaofanya wanawake wadharaulike na kuongeza idadi ya machokoraa mitaani sababu ya kuikataa elimu asilia ya mahusiano.
Mimi kazi yangu ni kudeal na vichwa panzi kama ninyi katika mada Ngumu mnazoforce kuchangia upupu wenu.
Mkuu heshima kwako,TUACHE KUJIPA MOYO, NDOA KWA KIZAZI CHA SASA NI GEREZA LA MATESO.
Anaandika, Robert Heriel
Kuhani!
Soma Kwa Utulivu;
Linatesa Wanawake
Linatesa wanaume;
Lakini Kwa nini?
Ili ndoa iwe ndoa kweli sharti ifuate mfumo wa kizamani, hilo nimeshalieleza kila mara. Kwa sababu ndoa misingi yake imejengwa kizamani. Misingi hiyo ndio inaifanya ndoa iwe ya muhimu na lazima.
Kam utakuwa ukinifuatilia Kwa umakini Kwa Akili bila kuonyesha mihemko utagundua kuwa Taikon ninamawazo ya kizamani, na ninatumia mifumo mingi ya kizamani.
Wengi wa wanausasa huniona kama kijana mwenye mitazamo ya mfumo dume, mchukia Wanawake, mkatili na mwenye mambo ya kikoloni.
MTU yeyote anayetumia mifumo ya kizamani Ndoa haiwezi kumsumbua, matatizo sijui ya nguvu za kiume hayawezi kumpata, Kwa sababu mifumo ya kizamani inasuluhu ya mambo ya sasa.
Ndoa Kwa vile ni mfumo wa kizamani umejengwa katika misingi Mikuu ifuatayo;
1. Ndoa lazima ifuate muundo huu wa Familia (Family Structure)
a)Baba ndiye Mtawala.
Kiongozi, msemaji wa mwisho, mtafutaji, mtunzaji na mlindaji wa Familia.
Baba anauwezo wa kuamua jambo lolote pasipo kuingiliwa.
b). Mama ndiye Msaidizi
Mlezi wa familia Kwa kupika, kuhakikisha usafi WA nyumba, kuwafundisha Watoto heshima na adabu, kufanya shughuli ndogondogo za uzalishaji ambazo hazitampunguzia wajibu wake Mkuu wa nyumbani kama Mama.
C) Watoto Kama matunda ya familia.
Watoto ni Mali ya Familia, hasahasa Mali ya Baba kwani Baba ndiye Mtawala, Mfalme na Kiongozi.
Watoto watafuata sheria zote za familia na ukoo bila kujali umri wao, hata wakiwa Watu wazima, watabaki kuwa Chini ya maamuzi ya Baba Yao.
Kama itatokea utengano baina ya Baba na Mama, Watoto watakuwa Mali ya Baba, na ukoo wa Baba. Hivyo ndivyo ilivyokuwa na ndio msingi wa Ndoa ulipo.
Ukiangalia msingi huu Kwa kizazi cha sasa umevunjwa, n automatically ndoa inapoteza nguvu kumaanisha inakosa umuhimu. Siku hizi Mtoto sio Mali ya Baba tena ni Mali ya Mama. Wanawake wanang'ang'aniza umiliki WA watoto, hata Baada ya kuachana.
Ieleweke kuwa Kiasili mtoto ni wababa lakini anayekulia katika tumbo la Mama.ndio maana Mama anaweza kuzaa Watoto wa asili nyingi tofauti tofauti kama vile Wahindi, wasukuma, Wachina kulingana na Baba zao lakini mwanaume Han uwezo wa kuzalisha mtoto Aina tofauti na asili yake, yaani kama Mwanaume ni Mpare basi Watoto atakaowazaa automatically watakuwa Wapare. Hata angezaa na Wanawake WA mataifa yote Duniani.
2. Wajibu na Majukumu
Huu ni msingi WA pili Baada ya muundo wa Familia. Mgawanyo wa majukumu katika familia haukuwekwa Kwa bahati Mbaya. Uliwekwa na watu wazima wenye Akili zao. Mgawanyo huo ulizingatia mambo Makuu yafuatayo;
i. Hulka, Akili na Maumbile ya Binadamu.
Mwanamke anahulka,Akili na maumbile yake na Mwanaume anahulka, akili na maumbile yake.
Majukumu ya Mwanamke na Mwanaume hayawezi kuwa Sawa Kwa sababu wanatofautiana katika tabia, Akili na maumbile Yao.
Sisi wanaume kimaumbile tuna misuli yenye nguvu ndio maana kazi za nguvu zinatuhitaji lakini Wanawake maumbile Yao ni nyoronyoro na nyororo hivyo kazi za nguvu sio Haki kwao kuzifanya, ingawaje wapo wanaojilazimisha lakini matokeo yake tunayaona wanapoteza Ile asili Y utukufu wao wa kike.
Mwanaume akifanya kazi za nguvu atazidi kuvutia na utukufu wa uanaume wake utazidi kushamiri.
Lakini Kwa Mwanamke atadhoofika na itakuwa kumuonea tuu.
Akili ya mwanaume Imeumbwa kufikiri na kukabiliana na mambo makubwa na mazito. Huku Akili ya Mwanamke Imeumbwa kufikiri na kukabiliana na mambo madogomadogo na Mwepesi.
Wanawake wako Very Sharp kuwaza na kukimbizana na mambo madogo madogo hata yawe Kumi na moja Kwa wakati mmoja. Lakini Jambo zito moja kubwa Kwa kweli wasingependa kulikabili.
Hata hivyo Kwa Sisi wanaume Akili zetu hazipo sharp kukimbizana na mambo madogo madogo Kwa wakati mmoja Ila tupo vizuri katika Jambo zito moja kubwa kulikabili.
Hii ni kusema, Chemistry hiii ndani ya familia ikitumiwa vizuri ndio huzalisha Maendeleo. Ukiwa na Mkeo ndio mnaanza Maisha ni rahisi kufanikiwa hasa ukimfuatisha katika mambo madogo madogo alafu naye akikufuatisha Kwa mambo makubwa makubwa. Ni ngumu Sana kuingia hasara ikiwa mtakubaliana katika tofauti zenu za Kiakili.
Bado hujamuelewa Taikon? Subiri utanielewa. Wakati Mwanamke anawaza kununua Jiko la Gesi, sahani za udongo, mapazia mazuri, n.k. Kwa mwanaume mambo hayo anaweza kuyapuuza asinunue Kwa sababu yeye anafikiri mambo makubwa kubwa kama kununua Gari, kiwanja, au kujenga nyumba.
Msipokuwa Makini katika utofauti wenu wa Kiakili mnaweza kujikuta mkipiga mark-time pasipokufanya Jambo zuri lolotendani ya Nyumbani.
Taikon ninashauri, Kwanza jueni ninyi ni mwili mmoja lakini mna hulka, Akili na maumbile tofauti, hivyo timizeni mambo ya familia Kwa utofauti wenu bila kuathiriana. Wekeni vikao na mijadala kisha muweke mipango na malengo yenu.
Mfano, Ndio mmeanza Maisha. Hamna kitu chochote. Mwanaume elewa kuwa Mkeo Akili yake na tamaa yake zinapishana, ni kweli anatamaa na vitu vikubwa kama umiliki WA nyumba na magari lakini Akili yake Kwa muda huo itawaza vitu vidogo vidogo.
Elewa kuwa Mwanamke ofisi yake ya Kwanza ni hapo nyumbani Wakati kwako mwanaume nyumbani ni sehemu ya mapumziko tuu. Hiyo pekee inatosha kukuambia upo utofauti.
Ikiwa Kwa Mkeo nyumbani ni Ofisini, basi hakikisha zana na vyombo vyote vya kazi zake vipo, na hapa nazungumzia vyombo vya Kisasa vitakavyomrahisishia kazi na majukumu yake.
Ni mateso makubwa kuoa Mwanamke na kumuweka nyumbani pasipo kuyatengeneza mazingira ya ofisi yake kuwa mazuri.
Unajua Mwanamke anapenda kupika kwaajili yako, mnunulie Majiko mazuri, vifaa ya Upishi kama Brenda, Mashine ya kufulia, pasi, Fridge, N.k.
Unajua kabisa Mkeo kuna muda atahitaji kupumzika hivyo lazima umuwekee Luninga, Sabufa, Feni au AC, muwekee vitabu vya simulizi ajisomee, Unga bando la ving'amuzi Mkeo ajisikie Raha, Nunua makochi au masofa mazuri na kitanda, Zulia na mito. Ili akichoka apumzike akikusubiri.
Kwa sababu ili mwanaume apumzike vizuri akirudi nyumbani sharti Mwanamke awe amepumzika vyema.
Sio mwanaume mzima unafungia TV na Deki ndani ATI ili Mkeo asiangalie, Huo ni uchizi, na wewe ni Mwendawazimu, na nitashangaa Mwanamke akikubali kuishi na kichwamaji.
Tabia ya Mwanamke na Mwanaume zinapishana Kwa kiwango kikubwa. Kupishana Huko ndiko kunafanya majukumu na wajibu kutofautiana.
Hakunaga usawa WA kiwajibu na kimajukumu baina ya MKE na Mume. Hiyo haipo. Ukitaka kuharibu familia yako basi weka huo usawa.
Nakupa Mfano, ni Hulk ya Mwanamke kutaka kupendwa, Wakati ni hulka ya mwanaume kutaka kuheshimiwa.
Ni hulka ya Mwanamke kutaka kusifiwa, Wakati Kwa mwanaume ni hulka yake kutaka kutukuzwa.
Mfano, umerudi nyumbani umemkuta Mkeo kajiliza, Mchana kutwa alikuwa akijishughulisha na kazi ya usafi na Kupanga nyumba.
Hata kama umechoka vipi ni jukumu lako kumsifia Kwa kazi nzito na nzuri aliyoifanya Mkeo. Utaangaza macho Kwa kustaajabu, ukiangalia huku na huku katika nyumba kisha utamtazama Mkeo na kumwambia;
Hakika hapa nimeoa Mwanamke, pamependeza mno, yaani pakitoka Mbinguni Kwa uzuri basi panafuata hapa nyumbani kwetu. Kisha unamfuata unamsiriba mabusu yakutosha.
Usijesema Taikon ni mchawi jinsi mambo yenu yatakavyowaendea vizuri. Ni vitu rahisi vinavyojulikana Sana Ila vilivyopuuzwa na Wengi.
Lakini wewe umerudi, ni kweli umetoka kazini, ni kweli umechoka, sasa unataka uonewe huruma za kijinga kama litoto lijinga, au uambiwe Pole, pole ya nini.
Mwanaume hautakiwi kutafuta pole za ajabuajabu. Usilazimishe mapenzi, pole ni sehemu ya kujali, kujali ni sehemu ya mapenzi, mapenzi yapo kwaajili ya Wanawake.
Mwanaume unatakiwa utoe Kwanza mapenzi ili urudishiwe kibaba cha heshima na mahaba.
Msingi huu umevunjwa katika Zama za Leo. Wanawake wanatafuta heshima badala ya kupendwa. Huku wanaume wanatafuta kupendwa badala ya kuheshimiwa.
Hapo automatically ndoa haina umuhimu wowote Kwa minajili hiyo. Kwani itageuka uwanja WA mateso makubwa.
Unataka ule hela za Mkeo alafu unategemea Mkeo akuheshimu? Unataka Mkeo atunze familia alafu unategemea heshima hapo? Taikon nazungumzia Uhalisia hapa.
Njia nzuri ya Kula hela za Mkeo au Wanawake ni kuwapenda, Full-stop. Na kuwapenda ni gharama zaidi ya Pesa watakazokupa[emoji23][emoji23] ingawaje Kwa MTU mwenye True love hatoona kazi.
Elewa kuwa Mwanamke anachotafuta Kwa mwanaume ni upendo tuu. Hivyo ni jukumu la mwanaume kuhakikisha anaiteka Imani na Akili ya Mwanamke Ione upendo wake(mwanaume).
Hata hivyo weka Akili kuwa Mwanamke kama hakupendi ni hakupendi tuu! Pia elewa kuwa Wanawake pia wanatamaa za miili Kam walivyowanaume hivyo anaweza kukukubalia Kwa sababu ya tamaa yake lakini hiyo tamaa ikiisha utaonja joto la jiwe.
Ili Mkeo au Mwanamke yoyote akuheshimu na kukurejeshea mahaba lazima uwe Mwanaume kweli. Usimamie misingi ya kiume.
ii) Mwenye Umiliki.
Mwenye Umiliki ndiye anatakiwa kuwajibika zaidi kuliko asiyemiliki. Hiyo ni kanuni ya Asili. Kwenye Ndoa au familia, mwanaume ndiye mmiliki wa Mke, Watoto na mali.
Hivyo yeye majukumu yake lazima yawe makubwa kuliko Mwanamke. Wanawake wote Duniani wanajua kuwa wakiolewa wanaenda kumilikiwa au kuwa Chini ya umiliki WA mwanaume. Kwao huo ni ufahari hasa wakimilikiwa na wanaume wanaowapenda.
Wajibu wa Mwanamke Kwa mwanaume ni mdogo Sana ukilinganisha na wajibu wa mwanaume Kwa Mwanamke.
Ni sharti mwanaume umvalishe Mkeo, umlishe, akiumwa umpeleke hospitali, Watoto halikadhalika.
Ila sio wajibu wa mwanamke kukufanyia hayo. Umiliki ndio Sababu kuu ya Jambo Hilo.
Ndoa kama mfumo wa zamani umejengwa katika mfumo huo wa umiliki. Kizazi cha sasa kimevunja msingi huo ndio maana ndoa imegeuka mateso makubwa Kwa Zama za leo.
Wewe unataka kuoa au umeoa, alafu umvalishi Mkeo, humlishi chakula kizuri, Watoto wanahangaika, alafu bado unataka heshima Kwa Mkeo huoni hapo kuna tatizo Pande zote mbili.
Unamtesa Mkeo kimwili, Kiakili na kihisia Kwa kushindwa kummiliki Kwa sababu ni Haki ya Mwanamke kumilikiwa ili ajihisi kupendwa.
Na pia ni mateso kwako mwenyewe(mwanaume) Kwa kutokuheshimiwa kwani utaishi Maisha ya TAABU ukidhani unadharauliwa na Wanawake(including Mkeo)
Hauwahudumii Watoto, Watoto wanatunzwa na Mama Yao alafu unataka Haki ya umiliki Kwa hao Watoto, come on! Huko ni kutesana tuu.
Ni vizuri, kama kweli mmeamua kuoa na kuolewa mfuate mifumo ya kizamani ili kulinda furaha, Amani na Mustakabali wa familia na kizazi chenu.
3. Kuvurugika Kwa utamaduni
Sisi ni waafrika, kuanzia asili yetu, ngozi zetu, Akili zetu na hata bara tunaliishi ni Afrika. Tuna tamaduni zetu ambazo ndoa na familia zilikuwa na nguvu.
Ujio wa tamaduni za kigeni kupitia dini ya kiarabu(Uislam) na Dini za Wazungu( Ukristo) umezifanya ndoa zetu kuwa magereza ya mateso.
Hatuwezi kuendesha ndoa zetu Kwa mifumo ya kigeni na kuacha mifumo yetu ya Asili. Kadiri tunavyojiingiza kwenye mambo ya kigeni ndivyo kunavyoiangusha Taasisi ya Ndoa zetu za kiafrika.
Mfumo wetu wa kiafrika hatuambui kitu kiitwacho Single mother, wala pasingekuwa na single mother, lakini mfumo wa Kiafrika unatambua Mwanamke Mjane basi,
Sheria, miiko, Mila na desturi zilijengwa katika mifumo ya kuhakikisha kuwa mwanamke anaolewa Kwa namna yoyote Ile tena Kwa asilimia kubwa akiwa Bikra.
Mfumo wa Kiafrika hajitambui kitu kinachoitwa ushoga, na hakukuwepo na ushoga na kama ingetokea dalili yoyote ya ushoga basi kijana huyo angekula Chuma akafie Mbele.
Mfumo wa kizamani ni ngumu Sana mambo ya ushoga kutokea Kwa sababu majukumu ya mwanaume ni makubwa, kazi zake na Chakula chake anachokula hazimfanyi afikirie upuuzi upuuzi, lakini mfumo wa Kisasa WA kijana muda wote amekaa kaa tuu, anajiangalia kwenye Kioo siku nzima, anajipodoa kama Mwanamke unategemea nini kama sio kutaka Kufirwa Huko.
Lakini kuvurugika Kwa utamaduni imekuwa chanzo kikuu cha kuifanya ndoa kuwa uwanja wa mateso.
Ndio maana nikasema sehemu Fulani kuwa wenye Kampeni ya kukataa Ndoa wanazohoja za msingi tena kubwakubwa.
Kijana au Binti, Oa au Olewa na kijana au Binti anayefuata mifumo ya kizamani lakini mwenye Akili za kisasa alafu utakuja kunishukuru.
Taikon ngoja nipumzike, watakanielewa wanielewe. Watakaonipinga wanipinge. Tumalize zamu yetu, tuwaache wanaokuja.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
ki uhalisia kwa maisha ya mjini watu wote tumetumika kabla ya ndoa wachache sana hawajatumika japo wanawake wanatumika zaidi kwa kuwa wao wanaenda mbali sana kwa kufiwa na watoto waliotarajiwa!Kumbe siku hizi kuna mume aliyekwisha tumika.
Kwako binafsi, I married kwa 15yrs now sijawahi kuona jipya la kuwafanya vijana mkatae ndoa