Tuacheni ramli chonganishi: Tusihukumu tusije tukahukumiwa. Karma ndio pekee hutoa hukumu ya haki hapa duniani!

Tuacheni ramli chonganishi: Tusihukumu tusije tukahukumiwa. Karma ndio pekee hutoa hukumu ya haki hapa duniani!

It's true, bakora za karma ni kama ufalme wa Mungu, kwa maana hamjui siku wala saa, na bakora zikitembea hakuna taarifa kuwa ndio bakora, ni majanga ya kawaida ya ugonjwa au ajali etc, the bottom line ni lazima upigike, madaraka, mamlaka au pesa, can't do a thing.

P.
Dah
 
Karma inamtokea jamaa tatizo hasikii hashtuki na mpofu kwasababu ya shibe ya maugali ya bure at taxpayers expense anayoyabughia na kushindilia magogoni
 
Wanabodi,
karma.jpg

Hili ni bandiko la wito wa Tuacheni Ramli Chonganishi Kuhusu Mhusika wa Shambulizi la Risasi kwa Mhe. Tundu Lissu, kupotea kwa mwana jf maarufu Ben Saanane, kupotea kwa mwanahabari Azory Gwanda, kuibuliwa kwa miili yenye majeraha kwenye viroba, au vitendo vingine vyovyote vya ukatili na umwagikaji damu kunalofanywa na watu wasiojulikana, hivyo kupelekea watu fulani fulani kuhisiwa kuhusika!, wito wangu ni "Tusihukumu, Tusije Tukahukumiwa!. Tuiachie "Karma" Ndio Pekee Hutoa Hukumu ya Haki Hapa Duniani!".

Kwanza tuendelee kumuombea Lissu uponyaji wa haraka.
Nimenote katika baadhi ya mitandao ya kijamii, kumeibuka makundi ya watu kujenga nadharia mbalimbali kuhusu chanzo cha tukio hili, na hayo matukio mengine ya kupotea kwa Ben Saanane, Azori Gwanda na miili ya kwenye viroba, aliyepanga na aliyetekeleza, na wengine hadi kufikia kupiga ramli chonganishi kuwa aliyepanga mpango huo ni fulani, na kumtaji hadi majina!, mara ni fulani, mara ni fulani, alimradi kunyooshea watu vidole!, hili sio jambo jema hata kidogo!.

Kwa sisi wa imani ya Kikristu, dini yetu inatufundisha, "Tusihukumu, Tusije Tukahukumiwa!". Tena kwenye ile kesi ya mwanamke kahaba aliyeshikwa ready handed, Bwana wetu Yesu Kristo akawaambia, "Na asiye na dhambi, awe wa kwanza kutupia jiwe!", hakuna aliyethubutu!.

Vivyo hivyo kwenye hili tukio la Lissu kupigwa risasi, na hayo mengine, maadam aliyelipanga ni binadamu, na watekelezaji ni wanadamu, tangu dunia hii kuumbwa, haijawa kutokea hata mara moja, uovu ukashinda wema, au uongo kuushinda ukweli, damu ya mwanadamu asiye na hatia, aliyeumbwa na Mungu, haiwezi ikamwagika bure bila kufidiwa, kila anayefanya uovu katika dunia hii, lazima atalipwa kwa uovu na malipo ni hapa hapa duniani, na kila anayetenda mema atalipwa mema.

Japo alichofanyiwa Lisu ni uovu mkubwa, mbaya na ukatili wa ajabu, na kwa hao wengine waliopotea, hakuna anayejua hatma yao ilikuwaje, you can just imagine!, lakini hakuna haja, wala sababu ya kuanza kunyoosheana vidole, tuviache vyombo husika kufanya uchunguzi na kutupatia majibu ya kina, kuhusu hao watu wasiojulikana, waliofanya ukatili huo, na endapo hivyo vyombo husika ndio wahusika na tukio hilo, bado kuna chombo kikubwa kuliko vyote kinachoitwa karma, ambacho ndicho pekee hutoa hukumu ya haki kwa kila kinachofanyika hapa duniani!.

Tumuombee Lissu to Get Well Soon, arejee nyumbani salama akiwa bukheri wa afya, tuombe muujiza wa Ben Saanae na Azori Gwanda, waibuke wakiwa hai toka huko mafichoni walikofichwa!.
Mungu yupo, kama alivyokusimamia Lissu hadi sasa bado uko hai, yeye ndiye pekee kupitia karma, atawahukumu watesi wako wako na watesi wa wengine hao!.

"The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili Hapa ...

Angalizo kwa Wana JF: Tuwaepuke "Prophets Of The Doom", kauli zao ...

Paskali
Mkuu unaogopeshwa na nini katika hizo ramli unazoita chonganishi?
Katika ramli hizo huenda kukawa na ukweli maana "wataalamu wabobezi" ambao intelijensia yao huwa makini katika mikutano ya kisiasa wako "kazini" mpaka leo pasipo majibu yanayoondosha ramli hizo!!! Je kwanini ili ramli chonganishi zisiondolewe kwa kuitwa wachunguzi huru "wasiotakiwa" toka nje?
Ramli chonganishi zitaendelea kupigwa hata kama hazipendezi na hatuzipendi!!
Karma ilishafanya kazi yake kitambo mkuu ndio maana kuna watu wana miaka 100+ na hawajafa hadi sasa ili washuhudie jambo kuu litakalotokea...
 
Laana ya Mungu Baba na ikawe nao hadi kizazi chao cha 5. wadharauliwe hadi na mawe ambayo hayazungumzi, Jua liwe makazi yao, mvua iwanyeshee wakiwa wamepumzika usiku, ndoto zao ziwanyime usingizi wakiota mandoto mabaya na machafu tu. wawe kizazi cha ukahaba na kudhulumiwa MILELE!
 
"Karma" Ndio Pekee Hutoa Hukumu ya Haki Hapa Duniani!".
Asante kwa uzi huu... Nina swali kidogo kuhusu Karma. Tumeelezwa kuwa Karma inatabia kama ya tukio la ' what goes around comes round' ...pia tumeelezwa kuwa karma ni sawa na sheria za Newton za Every action there is equal and opposite reaction. Swali lenyewe sasa....Mkuu, Ni wakati gani tunatambua kuwa Sasa Karma 'is going around' ama 'is coming around'....Na pia ni wakati gani tunaweza kusema sasa Karma is an ACTION na siyo REACTION?
Kwa kifupi, ni wakati gani ama ni vigezo vipi tunatumia kutambua kuwa sasa Karma inaanzisha duara na ama sasa KArma inafunga duara?
===
Kwa haraka haraka ninajua kabisa umelielewa swali langu barabara. Nasubiri majibu Mkuu.
 
We jamaa matakonini? Mbona watanzania wenzio wanapopotezwa unakaa kimya?, watu wanaotekwa hamjawahi kupaza sauti, watu wanapigwa risasi mpo kimya uzalendo ni kwenye mambo yanayomhusu magufuli pekee?? Uzalendo sio kutetea madege hayo uzalendo ni kusimamia misingi ya utawala bora, haki n.k nyie kwenu uzalendo ni kumsifia magu hata kwenye ujinga... Acha upuuzi Paskali umenikera
Karibu
P
 
Wanabodi,
karma.jpg

Hili ni bandiko la wito wa Tuacheni Ramli Chonganishi Kuhusu Mhusika wa Shambulizi la Risasi kwa Mhe. Tundu Lissu, kupotea kwa mwana jf maarufu Ben Saanane, kupotea kwa mwanahabari Azory Gwanda, kuibuliwa kwa miili yenye majeraha kwenye viroba, au vitendo vingine vyovyote vya ukatili na umwagikaji damu kunalofanywa na watu wasiojulikana, hivyo kupelekea watu fulani fulani kuhisiwa kuhusika!, wito wangu ni "Tusihukumu, Tusije Tukahukumiwa!. Tuiachie "Karma" Ndio Pekee Hutoa Hukumu ya Haki Hapa Duniani!".

Kwanza tuendelee kumuombea Lissu uponyaji wa haraka.
Nimenote katika baadhi ya mitandao ya kijamii, kumeibuka makundi ya watu kujenga nadharia mbalimbali kuhusu chanzo cha tukio hili, na hayo matukio mengine ya kupotea kwa Ben Saanane, Azori Gwanda na miili ya kwenye viroba, aliyepanga na aliyetekeleza, na wengine hadi kufikia kupiga ramli chonganishi kuwa aliyepanga mpango huo ni fulani, na kumtaji hadi majina!, mara ni fulani, mara ni fulani, alimradi kunyooshea watu vidole!, hili sio jambo jema hata kidogo!.

Kwa sisi wa imani ya Kikristu, dini yetu inatufundisha, "Tusihukumu, Tusije Tukahukumiwa!". Tena kwenye ile kesi ya mwanamke kahaba aliyeshikwa ready handed, Bwana wetu Yesu Kristo akawaambia, "Na asiye na dhambi, awe wa kwanza kutupia jiwe!", hakuna aliyethubutu!.

Vivyo hivyo kwenye hili tukio la Lissu kupigwa risasi, na hayo mengine, maadam aliyelipanga ni binadamu, na watekelezaji ni wanadamu, tangu dunia hii kuumbwa, haijawa kutokea hata mara moja, uovu ukashinda wema, au uongo kuushinda ukweli, damu ya mwanadamu asiye na hatia, aliyeumbwa na Mungu, haiwezi ikamwagika bure bila kufidiwa, kila anayefanya uovu katika dunia hii, lazima atalipwa kwa uovu na malipo ni hapa hapa duniani, na kila anayetenda mema atalipwa mema.

Japo alichofanyiwa Lisu ni uovu mkubwa, mbaya na ukatili wa ajabu, na kwa hao wengine waliopotea, hakuna anayejua hatma yao ilikuwaje, you can just imagine!, lakini hakuna haja, wala sababu ya kuanza kunyoosheana vidole, tuviache vyombo husika kufanya uchunguzi na kutupatia majibu ya kina, kuhusu hao watu wasiojulikana, waliofanya ukatili huo, na endapo hivyo vyombo husika ndio wahusika na tukio hilo, bado kuna chombo kikubwa kuliko vyote kinachoitwa karma, ambacho ndicho pekee hutoa hukumu ya haki kwa kila kinachofanyika hapa duniani!.

Tumuombee Lissu to Get Well Soon, arejee nyumbani salama akiwa bukheri wa afya, tuombe muujiza wa Ben Saanae na Azori Gwanda, waibuke wakiwa hai toka huko mafichoni walikofichwa!.
Mungu yupo, kama alivyokusimamia Lissu hadi sasa bado uko hai, yeye ndiye pekee kupitia karma, atawahukumu watesi wako wako na watesi wa wengine hao!.

"The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili Hapa ...

Angalizo kwa Wana JF: Tuwaepuke "Prophets Of The Doom", kauli zao ...

Paskali
Si mafaili walisema yamefungwa ... Uchunguzi huo unafanywa na nani....!!?? Kuna jeshi jipya la polisi linalofanya uchunguzi tofauti na hili !!??
 
Leo siku ya tarehe 7/Sept. 2019 ni siku ya kumbukumbu ya miaka miwili toka Mh.Tundu Lisu aliposhambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana. Mpaka leo bado wasiojulikana hawa bado hawatajulikana na uchunguzi mkubwa, makini na mkali wa Jeshi letu adilifu la polisi, unaendelea kuwabaini wasiojulikana hawa, hivi sasa kuna mashuhuda wawili muhimu sana, wanasubiriwa wao tuu kuhojiwa ndipo taarifa rasmi ya polisi kuhusu maendeleo ya uchunguzi huu ndipo ilatolewa.

Naendelea kusisitiza tuvute subra, tuacheni ramli chonganishi, tusihukumu tusije tulahukumiwa.
Get well soon Mhe. Tundu Lissu and welcome back home.
P
 
Naam Paskali nimependa hii hoja ya kuachia Karma... Japo wapo baadhi husuasan ambao nafsi zao zinawasuta watakutukana.

Heshima kwako
Karma iliyowajaa nikuamua kumuua Lissu? Mtakufa tu na mafunza watawatafuna vizur.

Msijichukulie sheria mikononi mkiona mtu ametenda kosa mahakama zipo mpelekeni na akikutwa na hatia mhukumuni kwa sheria sio mabunduki na kuwapoteza watu bila ya sababu ya msingi. Hiyo ndio miongoni mwa karma unayoipigia debe lakini mnashindwa ni kuitekeleza. Shame on you.
 
Naam Paskali nimependa hii hoja ya kuachia Karma... Japo wapo baadhi husuasan ambao nafsi zao zinawasuta watakutukana.
Heshima kwako
Mkuu Kaka Mkubwa Wakudadavua, usemayo ni kweli, na nimeanza kuziona dalili za karma kufanya jambo.
P
 
Mkuu Kaka Mkubwa Wakudadavua, usemayo ni kweli, na nimeanza kuziona dalili za karma kufanya jambo.
P
Mkuu Pascal Mayalla nakumbuka ulijibu swali langu hili hapa chini. Lakini majibu yako siyaoni jamvini na kwenye uzi huu. Uliyafuta majibu yale!?
===

Asante kwa uzi huu... Nina swali kidogo kuhusu Karma. Tumeelezwa kuwa Karma inatabia kama ya tukio la ' what goes around comes round' ...pia tumeelezwa kuwa karma ni sawa na sheria za Newton za Every action there is equal and opposite reaction. Swali lenyewe sasa....Mkuu, Ni wakati gani tunatambua kuwa Sasa Karma 'is going around' ama 'is coming around'....Na pia ni wakati gani tunaweza kusema sasa Karma is an ACTION na siyo REACTION?
Kwa kifupi, ni wakati gani ama ni vigezo vipi tunatumia kutambua kuwa sasa Karma inaanzisha duara na ama sasa KArma inafunga duara?
===
Kwa haraka haraka ninajua kabisa umelielewa swali langu barabara. Nasubiri majibu Mkuu.
 
Tunaweza kwa uchungu kukaa kimya juu ya Azory gwanda kwasababu kidogo aligusa usalama wa nchi kule mkiru lakini Ben sanane alikosa Nini? Hivi mtu akiniambia Mimi ninaelimu ya la Saba wakati c kweli inampasa kupotezwa?
Mkuu Superbug, hii ni ramli chonganishi!.
Ben Saanane alipotea, hakuna ajuaye sababu, unless kama unaijua sababu, na ukiitwa kusaidia polisi utatoa ushirikiano
vinginevyo...

Hizi pen names humu jf zisitupe kiburi na jeuri ya kupitiliza kwa kusema lolote au kumtuhumu yoyote kwa kumtaja majina bila na ushahidi, tumuhurumie Mkuu Max, anateseka sana kwa ajili yetu, kwenye yale ya ukweli ni acha ateseke, na kusulubiwa, kwa sababu hata Yesu alisulubiwa kwa ajili ya dhambi zetu na ni kwa kupigwa kwake sisi tuliponywa, lakini tuhuma nyingine bila ushahidi ni kuponza tuu watu bure, kama kitu huna ushahidi usituhumu kwa kutaja majina!.

P
 
Tuzifunge mahakama pia, KARMA itafanya kazi, na uzuri haina mshahara hivyo bajeti itapungua. Na mapolisi pia hawana umuhimu wa kuwa na mahabusu au vitengo vya upelelezi, mtu akifanya kosa wao wampe kadi imeandikwa KARMA is a bitch wamwachie kazi KARMA.
 
Mkuu Superbug, hii ni ramli chonganishi!.
Ben Saanane alipotea, hakuna ajuaye sababu, unless kama unaijua sababu, na ukiitwa kusaidia polisi utatoa ushirikiano
vinginevyo...

Hizi pen names humu jf zisitupe kiburi na jeuri ya kupitiliza kwa kusema lolote au kumtuhumu yoyote kwa kumtaja majina bila na ushahidi, tumuhurumie Mkuu Max, anateseka sana kwa ajili yetu, kwenye yale ya ukweli ni acha ateseke, na kusulubiwa, kwa sababu hata Yesu alisulubiwa kwa ajili ya dhambi zetu na ni kwa kupigwa kwake sisi tuliponywa, lakini tuhuma nyingine bila ushahidi ni kuponza tuu watu bure, kama kitu huna ushahidi usituhumu kwa kutaja majina!.

P
Ila asubuhi asubuhi unataka kutibua watu nyongo. Mtu akipotea mwenye wajibu wa kwanza kumtafuta ni mke/mume, kisha familia maana yaweza kuwa sio kupotea ila kuchepuka. Baada ya hapo ndugu, marafiki na hata mwajiri na mwisho kabisa Polisi.
Hawa Polisi ndio wenyewe hasa maana wana manpower, teknolojia na wajibu katika kumtafuta.
Inapofika mahali mtafutwa hakuwa na mahusiano mazuri na utawala na polisi hawaonyeshi hatua zozote wanazochukua pamoja na kupewa hints mbalimbali katika kumtafuta utategemea nini zaidi ya ramli chonganishi? Hivi kuna hatua gani imeshafikiwa katika suala la Ben? Nani analo faili la uchunguzi? Hakuna bwana! Na yote hayo hayapunguzi machungu zaidi ya kuyaongeza na muhusika mkuu ni jeshi letu la Polisi
 
Karma ni kitu kisicho halisi. Kimsingi kinatumiwa kujifariji na watu waliokata tamaa. Ukiona unaonewa kwa jambo lolote chukua hatua ukisubiri Karma litakusaidia umeliwa kweupe maana its just a myth.
 
Narration yako makes a big sense! BUT look: Mr, Pascal, usizidi kunipa mashaka! Mauaji, upoteaji, uteswaji, kesi za 'kipuuzi" wanazokutana nazo watu... Rais fulani hajawahi kuzikemea. Yoooooooooooooooooooooooooooooooooote yaliyotokea kwa Lisu sanasana alichojibu ni kuwa yule jamaa amelitelekeza jimbo! Wadau woooooooooooooooooooooote walisema ruhusu uchunguzi huru toka nje watampata aliyempiga risasi Lisu.. he never commented anything! Watu wamekutuhumu, kujibu tuhuma unafanyaje? Unasema Njoo mchunguze then ukweli utapatikana.
Pascal nambie yaliyotokea kwa Lisu kama angalikuwa hana mkono wake asingeruhusu kuona watu wanapoteza CCTV, wanaondoa walinzi, angelisema nataka kujua leo leo nani aliwaondoa walinzi! He never did that..... Maswali ni mengi yanayomwelemea.. irresisitible inference kuwa anahusika...
Ngoja niachie hapa......
Hili ni vizuri kuachia hapa kwasababu whoever who was behind shooting ya Tundu Lissu ni shetani kabisa, the devil in human flesh, mimi siamini tunaye shetani wa aina hii, ila kwa vile sio kila kinachofanywa na serikali lazima kiripotiwe kwenye media hivyo mimi ninaamini 100% chini ya 100% serikali imechunguza, zile CCTV ni nyumba ya Kalemani ila sio CCTV za serikali, naamini hadi Mzee atakuwa ameulizia, na uchunguzi umekwama kutokana na kukosekana mashahidi wawili wakuu ambao ni muhimu sana. Endapo kugetokea fatality kazi ingekuwa well done, by now file lingeisha fungwa, lakini kwasababu mashahidi wapo, wanasubiriwa wahojiwe ndipo uchunguzi uendelee.
P
 
Pascal mimi natamani yafuatayo; kwakuwa sina uwezo na madaraka natamani lile jopo lililokaa na kuona suluhisho la kumdhibiti Tundu Antiphas Mughwai Lissu ni kumtwanga Risasi COVID-19 iwapitie, wale waliotafuta upenyo wa kibabe wa kukwepa kumlipia Lissu gharama za matibabu na akati anastahili hadi mimi na umasikini wangu nikakopa na kutuma Tsh1,000,000/= kama mchango wa dhati ya moyo wangu ili Lissu apatiwe matibabu ya kuokoa uhai wake nasema COVID-19 ikiwa na jina la Yesu ndani yeke pamoja na moto wa maserafi na makerubi ikawapige hao wauaji kama upepo wa kisulisuli.

Wale waliohusika kuua na kufunga miili ya watz kwenye sandarusi na kwenda kuitupa mto Ruvu na wengine kwenye fukwe za bahari nasema COVID-19 popote ulipo kawapitie hawa wasaidizi wa Lucifer watangulie kabisa kule kwenye ziwa la moto.
Haiwezekani ktk nchi hii kuwe na watu wenye mamlaka ya kutoa uhai wa watu halafu tusio na uwezo wa kuwafanya chochote tushindwe hata kumuomba Mungu au shetani kuwasulubisha.

Pamoja na kwamba kisulisuli kilishindwa kuwabeba wanaume wa kuwaoa wale mabinti wa kanisa la mlima wa moto pendine ni kwa sababu ya uzito wao lakini bado nakiamini kisulisuli hakiwezi kushindwa kuwabeba COVID-19 na kwenda kuwafanyia INOCULATION hao niliowataja hapo juu.
Haiwezekani watu watekeleze mauaji ya watz wenzetu halafu bado tuendelee kuwasifia kisa teuzi, wapitie huu uzi hapa ili wajue kuwa hatuwapendi kwa matendo yao.

Kuna hawa wadudu wengine wanaitwa wasiojulikana ikitokea COVID-19 ikawasafisha pamoja na vizazi vyao Pascal huoni kama hii itakuwa ni baraka kutoka kwa Mnyazi Mungu kwa kutupunguzia watu wenye roho mbaya za Black Mamba a.k.a Koboko (Dendroaspis polylepis) au Anaconda a.k.a Water boa or Bull killer kama wataalam wanavyomfaham kwa jina la Eunectes murinus.

Nikipata bahati ya kuipata AK47 ikiwa loaded halafu nikaonyeshwa kwamba huyu ndiye aliyemfyatulia risasi Lissu Pascal otea nini kitatokea? Kama niliyoyasema hapo juu ni uongo na kwamba hao hawahusiki na madhila husika basi namkaribisha ZRAIL nyumbani aje anisalimie na si vinginevyo.
Mkuu Konyola, nimekuleta huku kwasababu umewaombea Corona hawa wasiojulikana.
Kwa vile ni watu wasiojulikana, hata wakisombwa na Corona, hakuna atakayejua, ila tusiwaombee watu wafe kwa Corona kwa kuwahisi tuu bila ushahidi, karma inaweza kukugeuzia kibao.

Mfano ni kweli Tundu Lissu ameshambuliwa na watu wasiojulikana, kisha Mkuu Konyola akaombea shetani Corona awakusanye na kuwapeleka moja moja kwa mkuu wao Lucifer kule kwenye makao yao ya milele ya jahanum ya ziwa la moto wa milele, hii ni sawa ni ombi halali kwasababu Tundu Lissu ameshambuliwa kweli na waliopanga na waliotekeleza ushetani ule ni mashetani kabisa hivyo kuwaombea vifo ni halali kabisa na hili na mimi naliunga mkono.

Lakini ikitokea wewe Mkuu Konyola, kwavile mimi Paskali nimetofautiana na Tundu Lissu mahali, hivyo Tundu Lissu aliposhambuliwa, wewe Konyola bila ushahidi wowote ukahisi nitakuwa ni mimi kwasababu tulitofautiana na Tundu Lissu mahali, hivyo sasa unaniombea mimi Paskali ndio nife kwa Corona, ikitokea ni kweli mimi nilihusika, then naombi yako yatajibiwa na Corona itakula kichwa!, Lakini ikitokea sio mimi wala sihusiki na shambulio la Lissu, kitendo cha wewe Mkuu Konyola kuniombea nife kwa Corona, itakuwa ni ushetani, na kupitia kanuni ya karma, ombi lako hilo linaweza kujibiwa kwa kanuni ya 3 ya Newton's Laws of motion ile ya every action there is equal and opposite reaction, hivyo ombi hilo likakugeikia.

Mungu kupitia kwa Bwana wetu Yesu Kristo alitufunza tusihukumu, tusije kuhukumiwa, hivyo wasiojulikana waliomshambulia Lissu, maadam hawajulikani na Mungu anajua kila kitu, mwachie Mungu.

P
 
Back
Top Bottom