Tuacheni ujinga, unafiki na mihemko. Afande Sele aachwe asisumbuliwe kabisa

Watanzania ni nyie tu mliokusanyika huko Karimjee? Wewe unapoongea utumie akili Watanzania ni wangapi na wanapatikana wapi?

Unatakiwa uwe na akili kuelewa. Watanzania ni wengi Tanzania ina watu zaidi ya milion 50 kule mwanza wana mungu wao wanamwabudu mwanamke.

Na wengine wengi wana miungu yao ya jadi,mizimu ,majini n.k haijawaondolea utanzania. Wewe uliambiwa watanzania wana Dini tatu tu? We una akili kweli? Kuna dini zaidi ya 200 nchini
Sasa hapa umepinga hoja yangu au umeisapoti na kuzidishia nyama zaidi, kweli ukiwa mbali na Mungu hadi akili inapungua.

Kama watanzania wanadini 1000+ na kilamtu anaomba kwa imani yake jibu ni kadhihaki imani zote hizo 1000+...mzizi uliyopo hao ni watanzania na yeye kasema Mungu wa watanzania.
 
Ambaye ni yupi sasa?maana bwege wewe utamshtaki kuwa kamdhihaki mungu wako yupi? Mimi mtanzania nikisema alikuwa anamtukana mungu wangu na mungu wangu kaona haina shida yaishe wewe unamshtaki kwa kosa lipi?kwa nini udhani kamtukana mungu wako? je mungu wako ni kweli hafanyi lolote? Mimi najua wangu anafanya atakalo so hahusiki na matusi hayo...wako je?kaumizwa na matusi😂😂😂😂
 
Sio mimi sielewi.

Suala lenyewe ndilo halieleweki.

Ndiyo maana hata wewe nimekutaka uthibitishe Mungu yupo, umeshindwa.

Hata wewe huelewi jinsi ya kuthibitisha Mungu yupo.

Si mimi tu.
Hivi wewe jamaa ni lini utaamini Mungu ndo anaekupa hiyo pumzi unayoringia?
 
Kwanza wathibitishe huyo Mungu yupo.

Wasije kumuua Afande Sele kwa hadithi tu.
Ww huna tofauti na wanaosema yupo maana hujawahi thibitisha kwamba hayupo. Upo upo tu na critical thinking zisizo za kiimani

Sisapoti mambo ya kuombeana kifo kama njia ya kuthibitisha uwepo wa MUNGU.

Inaweza sababisha mauaji ili kuprove a point.
Afande aheshimiwe hisia zake na imani yake.

Afande aachwe ila na yeye aheshimu imani za wengine. Asitukane tukane bila mpangilio kama kuku aliyekatwa kichwa
 
Hapa ndipo nakuonaga mjinga!
Kitu ambacho huna imani nacho kwanini upoteze muda wako kujishughulisha nacho kwa namna yoyote ile?
Kwanini usiachane nacho na ukajikita ktk masuala mengine?
 
Kosa la afande sele ni lipi..kwani ni lazima kila mtu atambue na kutukuza uwepo wa mungu.muacheni
 
Wewe utakuwa mchawi au mpiga ramli. Maana sijasema namwabudu Mungu gani. Ila unajaribu kupiga ramli. Au umeoneshwa na majini?[emoji23] Yamekudanganya. Wakristo wana Mungu wao hali kadhalika Waislamu. Tanzania ina wananchi zaidi ya Milion 50 na wapo wengine wana miungu yao.

Sasa wewe ambaye huna Elimu umekariri tu wakristo na waislamu. Kuna mabaniani,kuna wanaoabudu mizimu,kuna wanaoabudu majini,kuna wanaoabudu miti,kuna wanaoabudu jua,kuna wanaoabudu mwezi, kuna wanaoabudu nyota, kuna wanaoabudu vitu vya kufikirika.

Sasa wewe unajuaje afande sele alimtaja mungu wako na sasa unataka kuvaa silaha ukampiganie.maana ni wazi hajiwezi otherwise wala hukuwa na sababu ya kupaniki.
Hata kama wakristo wana Mungu wao na waislam wana Mungu wao ,,

Hao wote Mungu wao haoekani,,

Wote waamini Mungu lakini hawamuoni.

Afande Sele katukana Mungu asiyeonekana..

Huoni kama unatetea upuuzi?
 
Hivi wewe jamaa ni lini utaamini Mungu ndo anaekupa hiyo pumzi unayoringia?
Sitaki kuamini, nataka kujua.

Unaweza kuthibitisha Mungu yupo? Ukiweza kuthibitisha kimantiki mimi sina tatizo kukubali Mungu yupo.
 
Katiba inasema kuna uhuru wa kuabudu. Afande Sele alitoa audio moja ambayo haikuwa na maadili au maneno mazuri. Alimtukana mungu.

Kuna watu wanataka ifanya issue.mimi naamini kwa uwezo wake mungu huyo anaweza jipigania. Mungu mkuu hahitaji jeshi la wanadamu kumpa support.

But zaidi sikusikia akimtaja mungu wa mtu yeyote. Why sasa muanze ifanya kuwa ni issue? Ni kukosa kazi,kutokuwa na elimu,kutokuwa na ufahamu na uwezo wa kufikiri.

Yeye anaamini mungu si kitu na ametoa lugha ya kuudhi kwa mungu.wewe unapata wapi ujasiri wa kusema kamtukana mungu wako? Na je mungu akiitwa aje atoe ushahidi ameumizwa kiasi gani na maneno ya afande sele atakuja?

Lakini ikiwa zikapita siku hizo zilizotamkwa na asipokufa je itamanisha huyo mungu hana lolote? Na je akifa ndani ya siku hizo itaaminisha wengine kuwa mungu alichukia?kuna tofauti gani ukagombana na jirani mchawi akasema kesho hufiki na usiku ukafa?je naye ni mungu?

Na sisi tumemkufuru mara ngapi kwa kutenda dhambi ? Afande Sele hajawah kuwa na akili timamu toka miaka mingi imepita wenye akili wala hatuhitaji kuhangaika naye. Zaidi mna m promote tu.

But simuungi mkono kwa lugha chafu aliyotumia. Mimi naamini Mungu wangu ana uwezo mkubwa na atajionesha uwezo wake. Si lazima mpaka afande sele amtambue. Hana haja. Na walio karibu naye wamuase kuacha tumia vitu vinavyomchanganya akili.
Kwa mi maelezo hii. Nawe ni kinara wa waliokosa kaz ya kufanya
 
Ww huna tofauti na wanaosema yupo maana hujawahi thibitisha kwamba hayupo. Upo upo tu na critical thinking zisizo za kiimani

Sisapoti mambo ya kuombeana kifo kama njia ya kuthibitisha uwepo wa MUNGU.

Inaweza sababisha mauaji ili kuprove a point.
Afande aheshimiwe hisia zake na imani yake.

Afande aachwe ila na yeye aheshimu imani za wengine. Asitukane tukane bila mpangilio kama kuku aliyekatwa kichwa
Nimethibitisha kwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo, kwa kutumia mantiki na problem of evil.

Hapo juu.

Ni wewe tu hunisomi.

Mimi pia sisapoti mambo ya kuombeana kifo kama njia ya kuthibitisha uwepo wa Mungu, kwa sababu Mungu hayupo.
 
Hapa ndipo nakuonaga mjinga!
Kitu ambacho huna imani nacho kwanini upoteze muda wako kujishughulisha nacho kwa namna yoyote ile?
Kwanini usiachane nacho na ukajikita ktk masuala mengine?
Hata mimi kuwa mjinga, kama kweli ni mjinga, ni ushahidi kwamba Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote hayupo.

Angekuwepo, asingeumba ulimwengu ambao una wajinga.

Kitu cha uongo ambacho kinasemwa kuwa cha ukweli, kukifunua uongo wake, ni kufunua ukweli.

Mathalani, mtu akisema ana dawa ya Covid-19, inatibu huo ugonjwa, halafu ukajua dawa hii ni ya uongo, watu wanaoiamini watakufa, ni wajibu wako kusema dawa hii ni ya uongo.

Mwenye kusikia asikie ajilinde asipate ugonjwa.

Sasa mimi nimeona watu wanasema kuna dawa ya Covid-19, najua dawa ya uongo, nawaasa watu hii dawa ya uongo.

Halafu wewe unaniuliza, kama dawa ya uongo, kwa nini najishughulisha nayo kwa namna yoyote ile?

Najishughulisha nayo ili kumulika uongo, watu wenye kusikia wasipotee kwa kutumaini uongo.

Hiyo si sababu nzuri na tosha?
 
Katiba inasema kuna uhuru wa kuabudu. Afande Sele alitoa audio moja ambayo haikuwa na maadili au maneno mazuri. Alimtukana mungu.

Kuna watu wanataka ifanya issue.mimi naamini kwa uwezo wake mungu huyo anaweza jipigania. Mungu mkuu hahitaji jeshi la wanadamu kumpa support.

But zaidi sikusikia akimtaja mungu wa mtu yeyote. Why sasa muanze ifanya kuwa ni issue? Ni kukosa kazi,kutokuwa na elimu,kutokuwa na ufahamu na uwezo wa kufikiri.

Yeye anaamini mungu si kitu na ametoa lugha ya kuudhi kwa mungu.wewe unapata wapi ujasiri wa kusema kamtukana mungu wako? Na je mungu akiitwa aje atoe ushahidi ameumizwa kiasi gani na maneno ya afande sele atakuja?

Lakini ikiwa zikapita siku hizo zilizotamkwa na asipokufa je itamanisha huyo mungu hana lolote? Na je akifa ndani ya siku hizo itaaminisha wengine kuwa mungu alichukia?kuna tofauti gani ukagombana na jirani mchawi akasema kesho hufiki na usiku ukafa?je naye ni mungu?

Na sisi tumemkufuru mara ngapi kwa kutenda dhambi ? Afande Sele hajawah kuwa na akili timamu toka miaka mingi imepita wenye akili wala hatuhitaji kuhangaika naye. Zaidi mna m promote tu.

But simuungi mkono kwa lugha chafu aliyotumia. Mimi naamini Mungu wangu ana uwezo mkubwa na atajionesha uwezo wake. Si lazima mpaka afande sele amtambue. Hana haja. Na walio karibu naye wamuase kuacha tumia vitu vinavyomchanganya akili.
Kwenye paragraph ya kwanza ya andiko lako, unasema Katiba inaruhusu uhuru wa kuabudu, bila shaka afande Sele anajikinga na mwamvuli huo, lakini usisahau watu wanaonekana kumjia juu ama wanaofanya jambo hili liwe," issue" kwa kumpinga nao wanatumia kivuli cha Katiba yaani uhuru wa maoni...

Nawe una uhuru wa kuchagua upande baina ya pande hizi mbili...
 
Katiba inasema kuna uhuru wa kuabudu. Afande Sele alitoa audio moja ambayo haikuwa na maadili au maneno mazuri. Alimtukana mungu.

Kuna watu wanataka ifanya issue.mimi naamini kwa uwezo wake mungu huyo anaweza jipigania. Mungu mkuu hahitaji jeshi la wanadamu kumpa support.

But zaidi sikusikia akimtaja mungu wa mtu yeyote. Why sasa muanze ifanya kuwa ni issue? Ni kukosa kazi,kutokuwa na elimu,kutokuwa na ufahamu na uwezo wa kufikiri.

Yeye anaamini mungu si kitu na ametoa lugha ya kuudhi kwa mungu.wewe unapata wapi ujasiri wa kusema kamtukana mungu wako? Na je mungu akiitwa aje atoe ushahidi ameumizwa kiasi gani na maneno ya afande sele atakuja?

Lakini ikiwa zikapita siku hizo zilizotamkwa na asipokufa je itamanisha huyo mungu hana lolote? Na je akifa ndani ya siku hizo itaaminisha wengine kuwa mungu alichukia?kuna tofauti gani ukagombana na jirani mchawi akasema kesho hufiki na usiku ukafa?je naye ni mungu?

Na sisi tumemkufuru mara ngapi kwa kutenda dhambi ? Afande Sele hajawah kuwa na akili timamu toka miaka mingi imepita wenye akili wala hatuhitaji kuhangaika naye. Zaidi mna m promote tu.

But simuungi mkono kwa lugha chafu aliyotumia. Mimi naamini Mungu wangu ana uwezo mkubwa na atajionesha uwezo wake. Si lazima mpaka afande sele amtambue. Hana haja. Na walio karibu naye wamuase kuacha tumia vitu vinavyomchanganya akili.
Mkuu,

Ni Mungu (Capital 'M') na siyo mungu (Small 'm').

Samahani lakini. Pole kwa msiba.
 
Back
Top Bottom