Tuacheni ujinga, unafiki na mihemko. Afande Sele aachwe asisumbuliwe kabisa

Sasa hapa umepinga hoja yangu au umeisapoti na kuzidishia nyama zaidi, kweli ukiwa mbali na Mungu hadi akili inapungua.

Kama watanzania wanadini 1000+ na kilamtu anaomba kwa imani yake jibu ni kadhihaki imani zote hizo 1000+...mzizi uliyopo hao ni watanzania na yeye kasema Mungu wa watanzania.
 
Ambaye ni yupi sasa?maana bwege wewe utamshtaki kuwa kamdhihaki mungu wako yupi? Mimi mtanzania nikisema alikuwa anamtukana mungu wangu na mungu wangu kaona haina shida yaishe wewe unamshtaki kwa kosa lipi?kwa nini udhani kamtukana mungu wako? je mungu wako ni kweli hafanyi lolote? Mimi najua wangu anafanya atakalo so hahusiki na matusi hayo...wako je?kaumizwa na matusi😂😂😂😂
 
Sio mimi sielewi.

Suala lenyewe ndilo halieleweki.

Ndiyo maana hata wewe nimekutaka uthibitishe Mungu yupo, umeshindwa.

Hata wewe huelewi jinsi ya kuthibitisha Mungu yupo.

Si mimi tu.
Hivi wewe jamaa ni lini utaamini Mungu ndo anaekupa hiyo pumzi unayoringia?
 
Kwanza wathibitishe huyo Mungu yupo.

Wasije kumuua Afande Sele kwa hadithi tu.
Ww huna tofauti na wanaosema yupo maana hujawahi thibitisha kwamba hayupo. Upo upo tu na critical thinking zisizo za kiimani

Sisapoti mambo ya kuombeana kifo kama njia ya kuthibitisha uwepo wa MUNGU.

Inaweza sababisha mauaji ili kuprove a point.
Afande aheshimiwe hisia zake na imani yake.

Afande aachwe ila na yeye aheshimu imani za wengine. Asitukane tukane bila mpangilio kama kuku aliyekatwa kichwa
 
Kwanza wathibitishe huyo Mungu yupo.

Wasije kumuua Afande Sele kwa hadithi tu.
Hapa ndipo nakuonaga mjinga!
Kitu ambacho huna imani nacho kwanini upoteze muda wako kujishughulisha nacho kwa namna yoyote ile?
Kwanini usiachane nacho na ukajikita ktk masuala mengine?
 
Kosa la afande sele ni lipi..kwani ni lazima kila mtu atambue na kutukuza uwepo wa mungu.muacheni
 
Hata kama wakristo wana Mungu wao na waislam wana Mungu wao ,,


Hao wote Mungu wao haoekani,,

Wote waamini Mungu lakini hawamuoni.

Afande Sele katukana Mungu asiyeonekana..

Huoni kama unatetea upuuzi?
 
Hivi wewe jamaa ni lini utaamini Mungu ndo anaekupa hiyo pumzi unayoringia?
Sitaki kuamini, nataka kujua.

Unaweza kuthibitisha Mungu yupo? Ukiweza kuthibitisha kimantiki mimi sina tatizo kukubali Mungu yupo.
 
Kwa mi maelezo hii. Nawe ni kinara wa waliokosa kaz ya kufanya
 
Nimethibitisha kwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo, kwa kutumia mantiki na problem of evil.

Hapo juu.

Ni wewe tu hunisomi.

Mimi pia sisapoti mambo ya kuombeana kifo kama njia ya kuthibitisha uwepo wa Mungu, kwa sababu Mungu hayupo.
 
Hapa ndipo nakuonaga mjinga!
Kitu ambacho huna imani nacho kwanini upoteze muda wako kujishughulisha nacho kwa namna yoyote ile?
Kwanini usiachane nacho na ukajikita ktk masuala mengine?
Hata mimi kuwa mjinga, kama kweli ni mjinga, ni ushahidi kwamba Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote hayupo.

Angekuwepo, asingeumba ulimwengu ambao una wajinga.

Kitu cha uongo ambacho kinasemwa kuwa cha ukweli, kukifunua uongo wake, ni kufunua ukweli.

Mathalani, mtu akisema ana dawa ya Covid-19, inatibu huo ugonjwa, halafu ukajua dawa hii ni ya uongo, watu wanaoiamini watakufa, ni wajibu wako kusema dawa hii ni ya uongo.

Mwenye kusikia asikie ajilinde asipate ugonjwa.

Sasa mimi nimeona watu wanasema kuna dawa ya Covid-19, najua dawa ya uongo, nawaasa watu hii dawa ya uongo.

Halafu wewe unaniuliza, kama dawa ya uongo, kwa nini najishughulisha nayo kwa namna yoyote ile?

Najishughulisha nayo ili kumulika uongo, watu wenye kusikia wasipotee kwa kutumaini uongo.

Hiyo si sababu nzuri na tosha?
 
Kwenye paragraph ya kwanza ya andiko lako, unasema Katiba inaruhusu uhuru wa kuabudu, bila shaka afande Sele anajikinga na mwamvuli huo, lakini usisahau watu wanaonekana kumjia juu ama wanaofanya jambo hili liwe," issue" kwa kumpinga nao wanatumia kivuli cha Katiba yaani uhuru wa maoni...

Nawe una uhuru wa kuchagua upande baina ya pande hizi mbili...
 
Mkuu,

Ni Mungu (Capital 'M') na siyo mungu (Small 'm').

Samahani lakini. Pole kwa msiba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…