Tuambie Mechi yako Bora zaidi ya soka ambayo umewahi kuishuhudia

Liverpool vs Ac Milan - Istanbul 2005. (Miracle of Istanbul)

Wenyewe wanakuambia hawezi sahau, password za wengii kwenye Account(Gmail/yahoo etc) zilikuwa na neno hilo. (Istanbul)
 
Italy vs Germany 2006 world cup semi final Del piero alifanya unyama Sana pale pale ardhi ya wajerumani alipiga bonge la curve hatari
Also Liverpool vs Barcelona Origi anawaua chuma ya nne one of the best comeback in Ucl

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mechi ya Champions league mwaka 2000 Realmadrid vs Valencia ilikuwa binge la mechi
 
Kuna hiyo ya Simba na Stella Abidjan mwaka 1993. Ilikuwa fainali ya ambayo sasa inajulikana kama CAF Confederation Championship. Ndio mechi ilifanya niwe shabiki wa Simba mpaka leo.
Aisee kumbe huwa tunabishana na wazazi wetu
 
Kwangu mimi mechi bora inabaki kuwa kati ya Bayern Munich vs Manchester united mwaka 1999 usiku wa kukumbukwa kwa timu ya Manchester.

Hii mechi mpaka inaenda dk ya 90 ilikuwa Bayern anaongoza goli 1 kwa bila Ferguson alifanya sub za dakika ya mwishoni mpaka mwamuzi wa mchezo aliona Ferguson anapoteza tu muda huku mashabiki wa Bayern wakishangilia kuwa uefa tayari ni mali yao.

Bayern hawakuamini macho yao kwa magoli ya dk za lala salama ya ted 91 ole guna 93 na mchezo ukawa umeisha hapo.

Mpaka leo kichapo chochote Bayern akimpa man u bado anaona akitoshi kulipiza kisasi icho.
 
Mkuu mimi kipundi hicho nilikua na jamaa yangu ni shabiki wa Liverpool alinifunga shati kama wanavyofungwa wafungwa wawili asee ilikua na tension kubwa sana.
 
Hizo za 90 uliziona au uliona marudio
1994 kombe la Dunia lilichezwa Marekani na mechi zilikuwa zinaanza saa 8:30 usiku. Mnalala kwanza kisha mnaamka mnaangalia mechi. Nikiwa Shinyanga kipindi hicho mechi zinaonyeshwa Bitiama Hotel na Bwalo la Polisi.
1999 nyumba nyingi zilishanunua TV tukitumia madishi makubwa. Hii niliiangalia nyumbani kwangu sebleni kwenye TV niliyonunua mwenyewe.
Umenielewa Mkuu?
Mimi nimeanza kuangalia live kombe la Dunia 1990 ushindi wa Germany dhidi ya Argentina kwa goli la penati ya Andreas Brehme.
 
Sawa mkuu
 
Alafu extra aliingia marcelo upande mmoja di maria upande mwingine marcelo atletico aliita maji mma ila ni kweli walionewa lile goli la ramos la kusawazisha lilikua offside
Ulisimuliwa au ulitazama mwenyew. Alisawazisha kwa kona sasa offside itokee wapi.
 
National team fainali yangu bora ni ARGENTINA na france.

France tuliwafanya mbaya na hawatosahau, wamecheza na timu bora na mchezaji bora kuwahi kutokea.
 
UEFA 98/99
The competition was won by Manchester United, coming back from a goal down in the last two minutes of injury time to defeat Bayern Munich 2–1
 
1. Brazil vs France 1998 nililia
2. Senegal vs France 2002 nililia
3. Senegal vs Uturuki 2002 nililia
4. Arsenal vs barca 2006 niliumia

2005 ac milan na liver/ 2021 liver na barca hizi mechi mbili kwangu ni bora sana sababu nilikuwa emotional sana yaan saut ilikata kabisa mechi nyingi ile ya simba na nkana nilijuwa uwanjan saut ilikata

Ila mechi ya man u vs madrid ile ya 3-3 delima akitupia huku nestroy akitupia ndo mechi bora kabisa kuwah kuona sikutaka iishe sababu ya utam wa ball
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…