Tuamke, tuwaamshe mizimu wetu, katika nyakati za hatari watusaidie

Ndio maana jamii hizo zikaamua kuitupilia mbali.
Tumeitupilia mbali.
Unasahau kazi ya msikiti na kanisa, unasahau sanaa na ufundi wa hati, hisabati na kumbu hifadhi vilianzia hapa....kwamba tulikuwa tuna evolve, ndio wakaingilia kati na kuchomeka misumari katika mkufu utuunganishao, ndio Chinua Achebe akakwambia THINGS FALL APART
 
Wangoni na wahehe waliiomba sana mizimu ili iwasaidie vita dhidi ya wajerumani, ikawadanga kuwa watashida,
Kinjeketile Ngwale akadanganywa kuwa risasi ya mjerumani itageuka maji. Risasi haikugeuka maji, Jeshi la Wangoni likaangam
We mbona husemi awali wajerumani walichapwa na mkwawa?? Na hiyo usemayo ni historia changa ya juzi, Africa ilikuwepo tangu enzi na enzi, ni sisi tulianza kwenda Asia na Ulaya, tofauti ni kwamba, wakati sisi tulipeleka mwanga kule, wao ndio walioleta giza huku
 

Mkuu nahisi kama umeenda chaka, mbona sijaona popote mtu akipinga uhalali wa Mungu? Au mimi ndiye niko chaka au sijui kusoma?
 
Nimeifukunyua hii kutoka Maktaba!

HISTORIA YA AFRIKA ILIYOFICHIKA - Na Mwl. Matteo E. Mwita

Kumekuwa na historia iliyopotoshwa kuhusu Bara letu la Afrika, historia hiyo imekuwa ikituelezea sisi waafrika na bara letu kama watu tulikuwa nyuma sana kimaendeleo, watu ambao hatuna chochote cha maana. Bara na watu tuliokuwa tumeghubikwa na kila aina ya ushenzi, kwa muda mrefu tumekuwa tukiaminishwa kuwa bila ya ujio wa wazungu tusingefikia hatua ya kimaendeleo tuliopo leo, chakusikitisha baadhi ya waafrika wamekuwa wakiamini ghiliba hizo kutoka kwa wazungu. Vitabu vingi vya kihishtoria vilivyo ndikwa na wanazuoni wa kimagharibi vimejaribu kulipaka matope bara letu, vimetulaghai kiasi cha sisi kujidharau na kujiona hatukuwa na cha maana. Ila kuna baadhi ya vitabu kama when we ruled: The Ancient and Medieval History of Black civilization na How Europe Undeveloped Africa, vimekuwa na mitazamo tafauti kuhusu bara letu na kujaribu kuonyesha mafanikio ambayo tulikuwa tumeyafikia kama bara kwa karne kadhaa nyuma hata kabla ya ujio wa wageni. Makala haya yanaangazia kwa ufupi mafanikio ya eneo mmoja la Afrika zama hizo.

Je, ulipata kujua kuwa karne ya kumi na nne mji wa Timbuktu uliopo Afrika Magharibi ulikuwa na ukubwa mara tano zaidi ya jiji la London na ulikuwa ni mji tajiri zaidi ulimwenguni? Leo hii London ni kubwa mara 236 kwa Timbuktu. Mji huo hauna chochote kinachoweza kuonesha kuwa ni mji wa kisasa, idadi ya wakazi wake imepungua kwa mara mbili ya idadi ya wakazi karne tano zilizopita, mji umezingirwa na mitaa michafu iliyojaa ombaomba. Timbuktu hauna uwezo tena wakutunza hata makavazi na majengo yake ya asili.

Katika karne ya 14, sehemu tatu tajiri kabisa duniani zilikuwa China, Iraki/Irani na Himaya ya Mali inayopatikana Afrika Magharibi kati ya maeneo hayo matatu, sehemu ambayo ilikuwa huru na inashamiri ni himaya ya Mali. Uchina na eneo lote la mashariki ya kati yalikuwa chini ya utawala wa Genghis Kan. Himaya ya Mali ilikuwa chini ya utawala wa mtu aliyepata kuwa tajiri katika historia ya mwanadamu aliyepata kuishi hapa duniani Mansa Musa I, iliyokuwa inatawala maeneo ambayo kwa leo ni nchi za Mali, Senegal, Gambia, na Guinea. Hadi anafariki mwaka 1331, Mansa Musa alikuwa na utajiri wa dola bilioni 400. Kipindi hicho Mali ikizalisha zaidi ya nusu ya dhahabu na chumvi iliyokuwa inazalishwa duniani.

Mansa Musa alivyokwenda hija Mecca mwaka 1324 alibeba na kugawa dhahabu nyingi kiasi cha kuporomosha bei ya dhahabu duniani kwa miaka kumi mfululizo katika hija hiyo alifuatana na watu 60,000. Alianzisha maktaba ya Timbuktu, maandishi maarufu ya Timbuktu yalioandika kwa upana juu ya maarifa mbalimbali ya ulimwengu huu, yaliandikwa wakati wa utawala wake.

Mashuhuda wa mafanikio na ukuu wa Himaya ya Mali walitoka sehemu mbalimbali za dunia. Sergio Domian msomi na mhandishi wa Italia aliandika yafuatayo kuhusu utawala wa Mali. “kipindi hicho: ndipo ulipoanzia ustarabu wa miji, wakati wa uongozi wake, Mali ilikuwa na miji ipatayo 400 na eneo la Delta lilikuwa ni eneo lenye wakazi wengi sana.” Mji wa Mali wa Timbuktu katika karne ya 14 ulikuwa na idadi ya watu waliofikia 115,000, mara tano ya wakazi wakipindi hicho wa London.
Hivi karibuni National Geographic imeuelezea mji wa Timbuktu kama paris ya zama za kati. kwa utamaduni wake wa uwanazuoni na usomi wanafunzi takribani 25,000 walihitimu masomo ya chuo kikuu katika mji huo. Familia nyingi za kale za Afrika Magharibi zilikuwa na maktaba binafsi. Mji wa Chinguetti na Oudane uliyopo Mauritania una idadi ya vitabu 3,450 vilivyo andikwa kwa mkono enzi ya zama za kati. Inakisiwa kuwepo vitabu zaidi ya 6,000 hivi sasa katika mji wa Walata, baadhi vikiwa na vimeandikwa karne ya 8 AD. Kuna vitabu 11,000 katika makavazi binafsi Niger. Leo hii Timbuktu kuna vitabu zaidi ya 700,000 vilivyo andikwa zama hizo, kwa lugha za Mande, Suqi, Fulani, Timbuctu na Sudani. Maudhui ya vitabu hivyo yanajumuisha hisabati, utabibu, ushairi, sheria na unajimu. Ensaiklopidia ya kwanza duniani iliandikwa Mali katika karne ya 14, kabla ya wazungu kupata hilo wazo karne nne baadaye. Kwa msomi wa Afrika Magharibi wa karne ya 16, vitabu 1,600 vilikuwa ni maktaba ndogo sana kwake. Professor Ahmed Baba wa Timbuktu alinukuliwa akisema alikuwa na maktaba ndogo zaidi ya walizokuwa nazo rafiki zake, yake ilikuwa na vitabu 1600. Imam wa Timbuktu kwa mfano alikuwa na mkusanyiko wa maandiko ya kisayansi yanayo onyesha sayari zinavyo lizunguka jua. Huo ni ushahidi anuwi kuwa wasomi wa Timbuktu walijua vingi zaidi ya wenzao wa kimagharibi.

Katika karne ya kumi na tano, wataalamu wa hisabati wa Timbuktu walikuwa wanajua kuhusu mzunguko wa yasari, kupatwa kwa jua, walijua vitu vilivyowachukua wazungu miaka 150 kuvijua, hadi pale Galileo na Copernicus walipo andika kuhusu dhana hizo.

Mabaharia wa Mali walikanyaga aridhi ya Marekani mwaka 1311 AD, miaka 181 kabla ya Columbus. Msomi mashuhuri wa Misri zama hizo Ibn Fadl Al- Umari alipata kuandika juu ya hilo mwaka 1342, Katika sura ya kumi kwenye kitabu chake ameongelea mashua kubwa mbili zilizotumwa na mtangulizi wa Mansa Musa, mfalme alierithi kiti cha ufalme mwaka 1312. Huyo mfalme hakuandikwa na Al-Umari, ila wasomi wa zama hizi wameweza kumtaja kama Mansa Abubakari II.

Matukio hayo yalikuwa yanatokea wakati Ulaya kama bara ilikuwa imeghubikwa na zama za giza totoro, likishambuliwa na maradhi ya tauni na baa la njaa, wakiuwana wenyewe kwa wenyewe kwa ukabila na udini.

Miji mbalimbali ya kale iliharibiwa na uvamizi wa wageni, mji kama Kilwa uliopata kuwa mji tajiri na mashuhuri katika Pwani ya Afrika Mashariki katika karne ya 11 ulivamiwa na kuharibiwa vibaya na wareno. Wavamizi mbalimbali wa magharibi walivamia na kuharibu miji mbalimbali Afrika na kuharibu kabisa historia ya maendeleo waliokuwa wamejijengea waafrika kipindi hicho. Itoshe kusema hakuna maendeleo wazungu walioleta Afrika zaidi ya uharibifu, wizi na unyonyaji
 
Hadi ugonjwa wa ukimwi, ni kutudhoofisha, madawa ya uzazi wa mpango, kuwa makini sana, tunawekewa sumu
Katika pita pita zangu nimekutana na watu wanaosema wameponywa huu ugonjwa na waganga hawa hawa tunaowadharau....
Tukijitambua hata hospital hatufia kwenye foleni.
 
Kuwa huru ni kazi sana
 
Ahsante sana.
 
Eti Michael Jackson, yule wal izika 2008, kwanza familia ya Michael Jackson hawakuhudhuria msiba, tunataarifa na ushahidi, ilikunyamaza kimya, familia ya Michael Jackson, walilipwa pesa ndefuuuuuuu
Ni June 2009 sio 2008
 
Jamani bado tu tuingie kazini, tunataka ukombozi.... African Culture mbele kwa mbele.
 
michael time hizo alikuwa in riptide hiyo ilikuwanga first sign of warning, wonder shall never end ile alikuwanga amepanga show yake ya mwisho ili dunia ijue siri aliyoko nayo but bofore They Day dated, they put him down
Mmmh mbona tunaambiwa huyo alikuwa fake sasa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…