Mizimu,
ya Kiafrika ilishindwa kuhimili nguvu ya utandawazi na kupelekea kupotea siku hadi siku.
Mizimu
ilishindwa kuweka mamna ya ibada zao kwenye rekodi ya kimaandishi au sauti au picha ili kizazi kinachofuata kiweze kwenda nayo.
Ibada za mizimu
zilikuwa za kujifichaficha.
Ni watu wacheche walio chaguliwa kwenye jamii ndio walikuwa wanaenda polini peke yao kufanya ibada wengine walikuwa watazamaji wa matokeo tu.
Vijana na watoto walikuwa wakitengwa kwenye ibada za mizimu.
Mizimu
ilijitambulisha kwa kuogofya hivyo kupelekea wengine kuogopa kujihusisha nayo.
Baadhi ya maeneo mizimu ilikuwa ikitolewa sadaka za watu hivyo watu wengine waliamua kutoroka nyumbani kwao ili wasije wakaifikia zamu ya kutolewa kafala.
Mizimu
ilichangia sana katika kuifanya jamii zinazo iabudu kuwa masikini sana, sehemu nyigi kulikofanywa ibada za mizimu ziliambatana na umasikini uliokithiri.
Mizimu
ya kiafrika ilionekana haina nguvu ilipopambanishwa na mfano, na Mungu aliyeabudiwa na Wakristo.
Wamisionari kila walipoweka kambi palikuwa na msukumo mkubwa wa maendeleo matokeo tunayaona hadi hii leo.
Wamisionari walipoulizwa siri ya kufanya maendeleo walisema Mungu wanayemwabudu ndiye anaye wapa akili na nguvu ya kuendeo, na ananguvu kuliko mizimu yetu.
Baadhi ya wamisionari walibomoa vilinge vya kuabudia mizimu na mizimu haikuwadhuru tofauti na tulivyo aminishwa na waabudu mizimu kuwa ikibomoa kilinge chao utadhurika.
Mizimu
ilishindwa kujitetea iliposhambuliwa na wamisionari wa kigeni.
Ilikuja julikana pia kuwa wachawi waliroga watu wakisingizia ni adhabu za mizimu.
Mizimu ilikuwa inawahangaisha sana wanaoiabudu lakini ilileta matokeo hasi.
Wangoni na wahehe waliiomba sana mizimu ili iwasaidie vita dhidi ya wajerumani, ikawadanga kuwa watashida,
Kinjeketile Ngwale akadanganywa kuwa risasi ya mjerumani itageuka maji. Risasi haikugeuka maji, Jeshi la Wangoni likaangamia kizembe kabisa kwenye Vita ya Majimaji, mizimu akakaa kimya.
Mifano iko mingi sana ya udhahifu wa mizimu ya kiafrika.
hii ilipelekea Waafrika kiitupilia mbali mizimu ya mababu zao na kurithi ibada za Wageni.
Hit
Mizimu ya Kiafrika imejiangusha yenyewe baada ya kuonesha udhaifu mkubwa kwenye jamii zilizoiabudu.
Mizimu ikawa ndio chanzo cha matatizo mengi tu kwenye jimii za kiafrika.
Ndio maana jamii hizo zikaamua kuitupilia mbali.
Tumeitupilia mbali.