Tuamke, tuwaamshe mizimu wetu, katika nyakati za hatari watusaidie

Tuamke, tuwaamshe mizimu wetu, katika nyakati za hatari watusaidie

Kitu cha kwanza ni kukataa utumwa wa hizi dini na kujifungua minyororo yao mawazoni mwetu.

Bila hivyo, tutafikiri ndani ya mipaka waliyotuwekea tu.
Sasa kiranga usha anza kuni furaisha karibu.
 
Hata sala ya kiislamu pale wakimaliza kusoma Surat fattha wana malizia kwa kusema Ameeeen kwa sauti ya juu kabisa kisha wana sujudu.
Asee mbona mnapotosha watu kweupe hivi?siyo amen inatamkwa Aamin kwa kizungu ndiyo inaandikwa amen na maana ya hili neno ni "Na Iwe" na mara nyingi hutamkwa baada ya dua au maombi au kivingine hutumika kama kiitikio baada ya ombi(dua) ila hakuna lugha yeyote iliotanabahisha maana hiyo mnayotaka
 
Maana ya neno Aamiin (آمين) ni kwamba Mungu tukubaliye, na ni neno lilitotokana na semetic languages hutumika baada ya kumuomba Mungu, nadhani ndiyo neno pekee linalotumiawa na dini hizi 3 (Yahudi, Nasara(Christian) na Islam), halina uhusiano na hayo mambo mnayotaka kuwasadikisha watu.
Sijui nyinyi watu mna ajenda gani? Nadhani hata kwenye mizimu hampo bali mna kitu mnachotaka, anzisheni tu imani zenu mtawapata wa kukufuateni kunako kuzimu, kwani kuna waliyolala usingizi hasa.
Hii mitandao inasaidia sana lakini upande mwingine inapotosha sana usipokuwa makini ukawa wa kubebabeba tu kila unachosoma unasadiki kiukweli ni rahisi kupotea na kuangamia sijui tunawasaidiaje ndugu zetu hawa maana tayari kwa mujibu mada hii ni kama kuna watu aidha wanataka kuanzisha dini yao ama wamepotoshwa na mitandao...inasikitisha sana lakini pia juhudi kubwa zinahitajika kuwaokoa wandugu hawa
 
Starehe yeyote ile kwa mujibu Wa uislamu ni Dhambi.
Unapotoa hoja uwe unatoa na reference hizo ni imani za watu huwezi tu ukapotosha bila kuwa na reference wapi ambapo Uislamu unasema starehe zote ni dhambi,dhambi ni chochote utakachofanya kwa kuvunja kanuni na sheria ambazo Mungu asie na mfano ameziweka na ukiangalia kiuhalisia dhambi yeyote pia ina athari kwa jamii mfano ambao wewe ulipaswa kuweka nakusaidia hapa kuweka sote tunafahamu starehe kubwa duniani ni kujamiiana lakini kujamiiana hukohuko kunaweza kukawa dhambi au ibada kivipi...rejea ukifata kanuni alizoweka Mungu kwa maana ya ndoa kujamiiana huko ni utapata starehe,ibada na thawabu lakini ukivunja kanuni kwa maana utazini utapata starehe ya muda mchache,majuto na dhambi pia inaweza kusababisha madhara katika jamii kamavile kupatikana watoto wasiokuwa na uhakika wa baba na kupelekea watoto wa mitaani...
NB:tunaposoma mambo katika mitandao basi tujaribuni nasi kutumia fikra zetu kuyachambua na si kila lililoandikwa huko ni la kubeba
Asante
 
Ukiamini Uislamu, Ukristo, Uyahudi, umeshakubali kuwa mtumwa wa Wayahudi.

Na huwezi kunasuka na utumwa huo kwa ideologies za matawi ya juu bila kuondokana katika imani zenye mizizi hi.

Hii ni moja ya sababu kila siku napambana na habari za Mungu huyu wa Wayahudi.

Wayahudi wamewadanganya Wazungu kwenye Renaissance kwamba Mungu hataki wawe bankers, ni kazi ya dhambi.

Kisha wao Wayahudi wakachukua kazi zote muhimu za banking Renaissance Venice, Florence, Rome etc.

Na mpaka leo hawajaachia.

Sasa ukikubali dini yao (ambayo matawi yake ni Ukristo na Uislamu), utajikomboaje kama Muafrika?
mkuu hebu nisaidie kunidadavulia uislamu unafungamanaje na uyahudi japo kwa muhtasari
 
mkuu hebu nisaidie kunidadavulia uislamu unafungamanaje na uyahudi japo kwa muhtasari
Uislamu umeanzishwa kama movement ya Waarabu baada ya Waarabu kuwaonea gele Wayahudi wana dini yao ya kitabu na Waarabu hawana. Ukisoma Quran inaongelea "People of the Book" maana yake Wakristo na Wayahudi.

Kipindi cha mwanzo cha Uislamu, misikitini watu walikuwa hawaelekei Kibra Mecca, walikuwa wanaelekea Jerusalem.

Mitume na watu wengi sana walioelezwa jatika vitabu vya Wayahudi, kuanzia Adam, Musa, Ibrahim mpaka Yesu (Isa bin Mariam) wanatambulika katika Uislamu kama mitume. Musa katajwa kwenye Quran kuliko mtu mwingine yeyote.

Uyahudi, Ukristo na Uislamu zote zinaitwa "Abrahamic" religion kwa sababu zinachangua historia moja. Uislamu umesukumwa sana na Uyahudi katika misingi yake, sheria na kazi zake.

For more, see this Wiki

Islamic–Jewish relations - Wikipedia
 
umeshafanya utafiti wa kutosha juu ya msingi wa imani ya uislamu?,sababu kwa mujibu wa imani ya uislamu haijaanza na muhammad(s.a.w) sisi tunaamini kuwa dini ya uslamu ndio dini ya kwanza kabisa ambayo aliiamini adam,ibrahim,mussa,yesu mpaka kwa muhammad(s.a.w) sisi hatuamini kuwa musa alikuwa mfuasi wa imani ya kiyahudi bali muislamu.so huo uyahudi ndio dini mpya na sio uislamu.
 
Hii mitandao inasaidia sana lakini upande mwingine inapotosha sana usipokuwa makini ukawa wa kubebabeba tu kila unachosoma unasadiki kiukweli ni rahisi kupotea na kuangamia sijui tunawasaidiaje ndugu zetu hawa maana tayari kwa mujibu mada hii ni kama kuna watu aidha wanataka kuanzisha dini yao ama wamepotoshwa na mitandao...inasikitisha sana lakini pia juhudi kubwa zinahitajika kuwaokoa wandugu hawa
Ni lazima tujue wapi tunachukua elimu zetu, hususan za dini, kwani kila mtu anafanya kitu kutokana na niya yake, na ni vigumu kujua niya ya mtu. Na sisi tumejificha nyuma ya pc au smart phone tunaandika tuyatakayo kama vile hatutakuwa accountable kwa tunayoyafanya, ni ombi langu kubwa tuitumie hii neema ya mitandao katika kuleta umoja, upendo na amani, tunaweza tukatofautiana kifikra na kimtazamo lakini tutabaki kuwa tunahitajiana katika maisha.
 
Uislamu umeanzishwa kama movement ya Waarabu baada ya Waarabu kuwaonea gele Wayahudi wana dini yao ya kitabu na Waarabu hawana. Ukisoma Quran inaongelea "People of the Book" maana yake Wakristo na Wayahudi.

Kipindi cha mwanzo cha Uislamu, misikitini watu walikuwa hawaelekei Kibra Mecca, walikuwa wanaelekea Jerusalem.

Mitume na watu wengi sana walioelezwa jatika vitabu vya Wayahudi, kuanzia Adam, Musa, Ibrahim mpaka Yesu (Isa bin Mariam) wanatambulika katika Uislamu kama mitume. Musa katajwa kwenye Quran kuliko mtu mwingine yeyote.

Uyahudi, Ukristo na Uislamu zote zinaitwa "Abrahamic" religion kwa sababu zinachangua historia moja. Uislamu umesukumwa sana na Uyahudi katika misingi yake, sheria na kazi zake.

For more, see this Wiki

Islamic–Jewish relations - Wikipedia
Wewe kweli ni kiranga kama jina lako likivyo, unaleta ushahidi wa wikipedia hapa? A u serious? Wikipedia ipo chini ya israel elite.
Hebu tuwe serious kam huku ndio kujulikomboa bora tufanyekazi ili tusaidie familia zetu na baa la NJAA.
 
umeshafanya utafiti wa kutosha juu ya msingi wa imani ya uislamu?,sababu kwa mujibu wa imani ya uislamu haijaanza na muhammad(s.a.w) sisi tunaamini kuwa dini ya uslamu ndio dini ya kwanza kabisa ambayo aliiamini adam,ibrahim,mussa,yesu mpaka kwa muhammad(s.a.w) sisi hatuamini kuwa musa alikuwa mfuasi wa imani ya kiyahudi bali muislamu.so huo uyahudi ndio dini mpya na sio uislamu.
Hao ndio easaka tonge, wanataka kuaminisha watu uchawi kama ndio njia sahihi ya maisha.
 
Wewe kweli ni kiranga kama jina lako likivyo, unaleta ushahidi wa wikipedia hapa? A u serious? Wikipedia ipo chini ya israel elite.
Hebu tuwe serious kam huku ndio kujulikomboa bora tufanyekazi ili tusaidie familia zetu na baa la NJAA.
Ushahidi wa Wikipedia ukoje?

Unaelewa tunajadili hoja na si hoja imetoka wapi?

Unaelewa hata saa iliyosimama inakuwa sawa mara mbili kila siku?

Unaelewa hoja inapingwa kwa hoja na si kwa ad hominem attack?

Unaelewa kwamba Wikipedia imeletwa kama sehemu ya kuanzia mjadala na si kumalizia?

Unaelewa kwamba hiyo Wikioedia unayoikandia ina sources mbalimbali ambazo hujawahi kuzisoma?

Unaelewa nimeandika habari za Quran, Old Testament na Jewish scriptures ambazo zilikuwepo kabla internet haijafikiriwa?

Unaelewa kwamba umeshindwa kupinga hoja kwa hoja na umeleta kiroja?
 
Binadamu anapozaliwa tu, anajikuta yupo chini ya utawala wa Mama.
Mama anaamua amnyonyeshe au la, na kama hivyo ni muda gani.
Mama ndiye anayeamua akunyonyeshe hadi ushibe au kabla.
Mama ndiye Malkia na kamwe binadamu huyo mdogo hawezi kujitoa chini ya utawala wa huyo Malkia.
Yeye ataamua binadamu huyu ni muda gani, alale,aamke, ale, aoge, avae nk.
Hapa inapita miaka kadhaa kabla ya kujikuta chini ya utawala wa Malkia na Mfalme Baba.
Hawa watawala watammiliki huyu binadamu kwa kipindi fulani pia.
Katika kipindi hicho binadamu inampasa kufuata sheria zote anazopangiwa na hao ma mjamaa, la sivyo kuna adhabu zitamfika, kama kuchapwa viboko, makofi, kufinywa, kunyimwa chakula, kutishwa na hawezi kujinasua nao.
Binadamu huyu anazidi kukua, Baba na mama wananza kuona kuwa kijana anapata uwezo unaolingana na wao, wanaanza kuogopa kumchapa kama hatafuata wanavyotaka, wanaamua jambo lingine nalo ni kumkabidhi kwa Jamii.
Kijana anakabidhiwa kwa Jamii au taasisi zake.
Anaanza kupelekwa Shule, ili kafunzwe ustaraabu zaidi, hapo akiwakosea wazazi hawamchapi tena, wanamwogopa, watachukua hatua ya kumuonya na ikishindikana wanampeleka Polisi.
Juhudi zote hizo wanataka kijana afuate sheria fulani fulani ambazo zinazunguka ndani ya jamii husika.
Kijana kwakuwa sasa anapaswa kuwaacha wazazi na kwenda Shule, au taasisi nyingine ya kijamii, ambako atakutana na watu wenye mafundisho mengine, wazazi wanaamua kumlinda kwa kumkabidhi kwa taasisi za Ki imani.
Ili kuirutubisha akili yake isimtume kijana kufanya matendo ambayo hayakubaliki na jamii hiyo.
Kijana anapokuwa mtu mzima haraka haraka anakabidhiwa wake wa jinsia nyingine kwa Amri ya Ndoa ili asilale peke yake, asije akalala Bar.
Katika ndoa nako kuna sheria kibao za kuzifuata, kijana analazimika kusaini mkataba wa ndoa, na anaambiwa kabisa hakuna kuvunja ndoa kirahisirahisi. Kwa kujiamlia tu asubuhi unapoamka.
Hapo mke au mume anakuwa sio mpenzi tu, bali Polisi pia.
Polisi wa kumlinda kijana ili asikengeuke
Kijana lazima umsirikishe huyu Mpenzi Polisi katika kila jambo unalo amua kufanya.
Hata ukitaka kuondoka nyumbani lazima umuage huyu Mlinzi wako.
Ni lazima umtii huyu Mpenzi kumbe ni Mlinzi.
Na kwakuwa mko peke yenu lazima na nyinyi wote mlindwe na Mlinzi Mwingine msije mkakengeuka wote wawili ikawa badala ya kulala Nyumbani mjalala Kasino.
Hapa sasa mnakabidhiwa kwa walinzi wawili, Jirani na Serikali.
Mkigombana tu mlinzi wa kwanza anawajia ( jirani) atajaribu kuwa suluhisha mkiwa wabishi anaripoti kwa mlinzi wa tatu, Polisi, Serikali.
Hapo ukiendelea kuwa mbishi Polisi anajua pa kukupeleka, na unaweza ukapotea moja kwa moja kama hutajirekebisha.
Sasa basi
Tunaona kila hatua ya binadamu kuna ulinzi unamfuatilia, upo nyuma yake ambao tunauona kwa macho.
Swali linalobaki huyu mlinzi atalindwa na nani ?
Ili kumfanya asimwonee binadamu anapo taka, yaani mlinzi, mke au mume, mlinzi jirani, mlinzi polisi, mlinzi Serikali, nk.
Ili mlinzi mmoja asimwonee mwenzake hapa ndipo anapojitokeza mlinzi mkuu.
Jamii inampa cheo, cha Uungu, huyo ndiye Mungu, huyo anajulikana kuwa ni Alfa na Omega. Muweza wa yote, Almighty.
Katika kila jamii ukiitembelea ina Mungu wake.
Nenda Uchina, nenda Brazil nenda kokote duniani utamkuta huyo Mungu ambaye jamii inamwogopa na kumheshimu sana sana, na kulazimika kumtii kwa kila anachosema.
Ukikosea kimtii jamii inaweza kukuadhibu, sehemu nyingine unakatwa kichwa kabisa kwa kumkose, au Kumkufuru, huyo Mungu.
Tanaona hadi leo, Serikari ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikitaka kuanza kutunga sheria zake Bungeni, lazima kwenye ufunguzi wa kikao kuna Kusali uli kupata baraka zake, huyo Mungu.
Ref. Sala ya Bunge.
Iko pia sala ya Taifa, ambayo inajulikana kama Wimbo wa Taifa.
Humo Mungu hutajwa sana, ili aibariki Nchi, Viongozi na Watu wake.
Yaani vyoote hivyo ni vyake, mali yake, yeye ndiye aliyevitengeneza, na hana mshirika.
Leo tunaona Viongozi wa Serikali wakiwa wanawaonea Raia wanaowaongoza, wanakaripiwa vikali na Wafanyakazi wa huyo Mungu, wanaojulikana kama Watumishi wa Mungu.
Wana vyeo kama vile, Shehe, Imamu, Padri, Askofu, Mchungaji nk.
Wanaionya Serikali kwa Nyaraka na Matamko, na kuitisha kuwa wataishitaki kwa Mungu, nayo Serukali inaogopa na kujirekebisha kiasi fulani fulani.
(Hapa nilikuwa nadadavua uhalisia wa kimaisha wa Binadamu)
Binadamu anazungukwa na walinzi kila kona. Kila dakika kila sekunde, walinzi wanaoonekana na wasioonekana.
Uhuru wa wa kifikra utapatikana wapi kwa binadamu ?
maana ukiwa huru kifikra unakuwa huru kimatendo pia.
Toka anazaliwa hadi anakufa Binadamu hayuko huru kuamua au kutenda anachotaka mwenyewe binafsi.
Kwa mfano.
Hapa Tanzania mtu akiamua kutumia madawa ya kulevya anakamatwa, akitaka kupanda Bangi shambani mwake ili aitumie anakatazwa na hata kutishiwa kufungwa na Mlinzi Serikali.
Hapo uhuru uko wapi ?
Bangi navuta mimi wewe
Inakuhusu nini ?
Mbona unaiingilia uhuru wangu mimi binafsi ukichukulia sivuti hadharani bangi yangu ?
Mwenyewe napenda kuvuta huku nikiimba
" Bangi Nibangue nilime hadi kuleee "
Bangi usiyovuta yakuwashiani ?
Kuna uhuru hapo ?
Uhuru gani wa kulazimishwa kutii sheria alizotunga mtu
mwingine ? Au Mungu ?
Maana ya Uhuru ni Kuwa Huru Kifikra na Kimatendo pia.
(To Be Total Free)
Je unaweza kujikomboa kwenye mikono ya hawa walinzi wote nilio wataja ukianzia na Mama mzazi ?
Anafuata, Mke au Mume, Jirani, Serikali, na Mungu ?
Au unataka usimtii mmojawapo kati ya hao walinzi ?
Ndipo ujulikane kuwa uko huru ?
Hit.
Binadamu hawezi kuwa huru,
kwani analazimika kutii sheria alizowekewa na waliomtangulia, la sivyo atakumbana na adhabu kali zinazoweza hata kumtoa uhai wake, kama ataendele kuwa mkaidi.
Hello to Free Men.
 
Ushahidi wa Wikipedia ukoje?

Unaelewa tunajadili hoja na si hoja imetoka wapi?

Unaelewa hata saa iliyosimama inakuwa sawa mara mbili kila siku?

Unaelewa hoja inapingwa kwa hoja na si kwa ad hominem attack?

Unaelewa kwamba Wikipedia imeletwa kama sehemu ya kuanzia mjadala na si kumalizia?

Unaelewa kwamba hiyo Wikioedia unayoikandia ina sources mbalimbali ambazo hujawahi kuzisoma?

Unaelewa nimeandika habari za Quran, Old Testament na Jewish scriptures ambazo zilikuwepo kabla internet haijafikiriwa?

Unaelewa kwamba umeshindwa kupinga hoja kwa hoja na umeleta kiroja?
Kiranga kaka labda hujanielewa, nilibase kwenye ushahidi wako wa wikipedia.
Wikipedia ni miongoni mwa search engine ambayo ipo chini ya watu ambao ni maadui zetu, kivipi wataandika ukweli kaka, ni hilo tu.
 
Tuendelee kujikomboa kwa kuangalia weakness zetu tukimlaumu mzungu sijui muyahudi mara dini nk. Tutatoka vipi katika utumwa huu wa fikra stop blaming bhana unataka tuifuate mizimu bado tutakuwa tumefungwa na fikra za mizimu ambayo they have nothing to do with our existance and our life. In order to be free we have to focus within ourselves na si kuanza kuleta blah blah za uyahudi na uzungu mara dini nk as if we are struggling to have superiority status. Hii siyo battle ya ubora na nguvu ya race fulani. Tunamjadili muyahudi wa kazi gani unaelezewa uislaM n ukristo for what purpose? Mungu kaumba kila race na ability strength intelligence etc tufocus kurealize our ability our stregth as a black race, lets rise up this domant power within ouselves, let us ground ourselves without being dependent to any race.

Nimejaribu kuchangia tu ni mawazo yangu ya kile ninachoamini ni ukweli
 
Back
Top Bottom