Tuanze kukusanya ushuru wa taka kupitia TANESCO!

Tuanze kukusanya ushuru wa taka kupitia TANESCO!

Sasa mita moja wanatumia familia ya watu 20. Huoni hapo kuna hasara itajitokeza?

Hapo ishu ni serikali za mitaa, iwepo control number ya kila kata, wazabuni wachukue pesa serikali za mitaa na malipo yafanyike kupitia control number na sio cash.
Kila Kaya itapaswa itoe 3k ya taka kila mwezi.

Kila mtu akilipia control number pawe na mfumo wa kuweka namba ya simu na jina. Ili kumbukumbu zibaki kwenye mfumo. Aliyelipa na asiyelipa,, lini na kiasi gani itakuwa wazi.

Kuchoma taka iwe marufuku isipokuwa kwa kibali maalumu.
Kuna kitu cha msingi ambacho bila kufanyikika vitu vingi sana haviwezi kufanya kwa ufanisi i.e. Tanzania kuwa na database ya taifa. Yes, sizungumzii huu upuuzi wa NIDA au list ya wapiga kura. Nazungumzia serikali kuwa na database ya eletronic ambayo ina orodha ya watu wote wanaoishi Tanzania na wamehakikiwa. Unasajili tangu mtoto akiwa na eg mwezi mmoja mpaka uzeeni na akifariki inawekwa kwenye kumbukumbu. Ukishakuwa na database ya aina hii (ambayo haina gharama kubwa ku-create kama nia ipo) basi mambo mengine yote inakuwa rahisi kufanya. Kwa mfano ukienda kuomba passport badala ya kuambiwa kalete barua kutoka sijui wapi, unakuta jina lako lipo tayari. Ukienda benki wanaweza ku-retreive record zako. Ukishakuwa na hii hata kuelewa watu wote wanaoishi mitaani ni rahisi na vileviole kupanga huduma.
 
Sio kila mtu anamuda wa kufanya usafi. Ndio maana wengine wameajiri makampuni yanafanya kazi hiyo.
Sasa kwa vile serikali haina uwezo wa kulazimisha kila mwananchi aajiri kampuni la usafi. Ndio maana imebeba jukumu hilo la kutoa huduma hiyo kupitia wazabuni.

Kingine, ishu sio kufanya usafi. Ishu ni kubeba takataka. Wewe umefanya usafi. Takataka unatupa wapi?
Unaeneo la kutupa takataka au ndio utatupa kwa jirani?
Hayo makampuni ya usafi unafahamu ni madili ya watu Mtibeli?
 
Ili kuimarisha usafi wa mazingira yetu napendekeza tuanze kukusanya ushuru wa taka kupitia mita za luku.

Tsh 6,000 kwa mwezi kwa kila mita, sawa na wastani wa Tsh 200 kwa siku.
Tanesco wakishakusanya pesa hizi wazipeleke kwenye mkoa husika.

According to sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022. Kuna nyumba taribani milioni 12 hadi sasa.

Tukifanikiwa kukusanya fedha hizi kwa angalau nyumba milioni 10, tuna uwezo wa kukusanya Tsh bilioni 720 kwa mwaka.

Mikoa iwezeshwe kukopa mikopo ya kibiashara na kununua matipa (Howo/ Faw au Shacman), angalau tipa mbili kwa kila kata za mjini na tipa 1 kwa kata za vijijini.

Wizara ya tamisemi kwa kushirikiana na wizara ya mazingira waingie MOU na Tanesco ili zoezi la ukusanyaji wa ushuru wa taka kupitia mita za luku uanze mara moja.

Tukifanya hivi tutafanikiwa kuboresha usafi wa mazingira yetu
Hii ID itakuwa ya Mwigulu! Mr Tozo
 
Sio kila mtu anamuda wa kufanya usafi. Ndio maana wengine wameajiri makampuni yanafanya kazi hiyo.
Sasa kwa vile serikali haina uwezo wa kulazimisha kila mwananchi aajiri kampuni la usafi. Ndio maana imebeba jukumu hilo la kutoa huduma hiyo kupitia wazabuni.

Kingine, ishu sio kufanya usafi. Ishu ni kubeba takataka. Wewe umefanya usafi. Takataka unatupa wapi?
Unaeneo la kutupa takataka au ndio utatupa kwa jirani?
Unaibua issue ya "poor land tenure" hapa ambayo haina uhusiano na kuwatengenezea watu ulaji kwa kisingizio cha usafi.
 
Ieleweke hoja kuu ni suala la kufanya usafi na taratibu nzuri za usafi kuzingatiwa ila tunakataa utengenezaji wa mifumo ya upigaji chini ya mwamvuli wa usafi.
 
Kodi ya jengo plus taka mnataka kutuu na sukari eti? Mtakula ela na taka zitabaki paleplae mnashindwa kuweka usafi kipaumbele mnawaza maslahi kwanza mbwa ninyi!
Hela za taka mpaka sasa zinakusanywa huko mtaani lakini ukusanyaji wake umekuwa mgumu.
Tunachofanya hapa ni kuhamisha majukumu ya kukusanya fedha hizo kupitia Tanesco kwa kuwa kwao ni rahisi kuzikusanya.
 
Me naona vijana wa JKT, jeshi la zima moto pamoja na migambo kwa kuwa wapo katika MISTARI wa mbele wa kutoa misaada ya ulinzi Hawa katika kufanya usafi wa mitaa wanafanya vyema mfano MLANDIZI Kuna vijana wa RUVU JKT miaka ya nyuma walikuwa wanafika sokoni wanasafisha mitaro, barabara na pia kuziba zile barabara mbovu kwa usahihi hivyo serikali ingeongeza nguvu katika miaka miwili ya kujitolea kwa vijana zipatikane siku 90 za kufanya usafi na kukumbusha suala la usafi ni lazima na sio ombi ikiwa hivi tutawachungulia Kigali Rwanda kidogo
 
Hela za taka mpaka sasa zinakusanywa huko mtaani lakini ukusanyaji wake umekuwa mgumu.
Tunachofanya hapa ni kuhamisha majukumu ya kukusanya fedha hizo kwenda Tanesco kwa kuwa kwao ni rahisi kuzikusanya.
Issue ni usafi au hela za kufanyia usafi? Mbona kipaumbele tunakielekeza kwenye pesa kuliko usafi wenyewe?
 
Mkuu, lengo sio kumuumiza mtu bali lengo ni kuboresha mfumo wa ukusanyaji taka.
Tunataka ndani ya miaka miwili nchi yetu iwe safi kama Rwanda.
Kama ni hivyo mfano ulioutoa hawatumii njia hiyo kama kipaumbele "strict policy and laws" siyo mbambamba....enforcement Mkuu.
 
Unakimbilia ushuru
Kwani ushuru watu hawatoi!

Solve tatizo kwanini taka zinacheleweshwa kukusanywa/kupitiwa
Huko dampo mazingira miundombinu yako vp

Na kwa taarifa yako mvua zikija huko dampo hakuinguliki mtaakaa na msuchafu yenu ndani mpake mtie akili

Ova
 
Ili kuimarisha usafi wa mazingira yetu napendekeza tuanze kukusanya ushuru wa taka kupitia mita za luku.

Tsh 6,000 kwa mwezi kwa kila mita, sawa na wastani wa Tsh 200 kwa siku.
Tanesco wakishakusanya pesa hizi wazipeleke kwenye mkoa husika.

According to sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022. Kuna nyumba taribani milioni 12 hadi sasa.

Tukifanikiwa kukusanya fedha hizi kwa angalau nyumba milioni 10, tuna uwezo wa kukusanya Tsh bilioni 720 kwa mwaka.

Mikoa iwezeshwe kukopa mikopo ya kibiashara na kununua matipa (Howo/ Faw au Shacman), angalau tipa mbili kwa kila kata za mjini na tipa 1 kwa kata za vijijini.

Wizara ya tamisemi kwa kushirikiana na wizara ya mazingira waingie MOU na Tanesco ili zoezi la ukusanyaji wa ushuru wa taka kupitia mita za luku uanze mara moja.

Tukifanya hivi tutafanikiwa kuboresha usafi wa mazingira yetu
Hivi huwa unawaza kwa kutumia nini!hiyo 1500 ya kila mwezi ya kodi ya nyumba watu imetuaacha hoi halafu unaanzisha uzi wa kipuuzi hivi!unajua fika vijiji watu wanaishi nyumba za nyasi lkn wanatozwa hiyo kodi na je wananufaika nini kama siyo kuwanyonya.haya kuna magari yanayotoa uchafu vijijini?kwa nini umtize huyo mtu wakati hahusiki na uchafu wenu wa mjini!mnapojaliwa kuwa na maisha mazuri ni vema mkaangalia maisha halisi ya watu wa vijijini.shida nyie watu wa ccm kila siku mnawaza kuwaibia wananchi kwa kubuni tozo ili mzidi kubaki na vyeo vyenu.ni sawa inaendeshwa na kodi lkn uzoefu unaonyesha mto nchi hizi za kiafrika kodi hazitumiki ipasavyo bali zinatumika kutweza utu wa mtanganyika.
 
Hapana Mkuu.
Kwa mazingira ya mjini ulaji hauepukiki kabisa.
Hapa ishu ni ulaji wenye tija kwa watu.
Tija kwa watu inaonekana tunapoweka " strict policy and laws" zinazopunguza mianya ya ulaji Mtibeli, kinyume na hapo tutajikuta tukifanya lobbying kuwasaidia wapigaji badala ya " public interest"
 
Badala ya kukusanya lundo la uchafu, kujengwe incinerators kwaajili ya kuchoma taka
R.png
 
Ili kuimarisha usafi wa mazingira yetu napendekeza tuanze kukusanya ushuru wa taka kupitia mita za luku.

Tsh 6,000 kwa mwezi kwa kila mita, sawa na wastani wa Tsh 200 kwa siku.
Tanesco wakishakusanya pesa hizi wazipeleke kwenye mkoa husika.

According to sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022. Kuna nyumba taribani milioni 12 hadi sasa.

Tukifanikiwa kukusanya fedha hizi kwa angalau nyumba milioni 10, tuna uwezo wa kukusanya Tsh bilioni 720 kwa mwaka.

Mikoa iwezeshwe kukopa mikopo ya kibiashara na kununua matipa (Howo/ Faw au Shacman), angalau tipa mbili kwa kila kata za mjini na tipa 1 kwa kata za vijijini.

Wizara ya tamisemi kwa kushirikiana na wizara ya mazingira waingie MOU na Tanesco ili zoezi la ukusanyaji wa ushuru wa taka kupitia mita za luku uanze mara moja.

Tukifanya hivi tutafanikiwa kuboresha usafi wa mazingira yetu
Usafi ni jukumu la uongozi wa miji ni huduma sio kodi
 
Suluhisho ni wazabuni wa kuzoa taka wawe na vifaa vya kisasa Road Sweeper,Road Vacuum Cleaner, Garbage Compactor trucks,Self Loading Garbage trucks, kila wilaya iwe na Garbage Incinerator na sehemu kubwa ya kufanyia waste recycling angalau 3
 
Back
Top Bottom